Mungu hana msaada wowote katika maisha yangu

Mungu hana msaada wowote katika maisha yangu

Afya ya akili haipo sawa...kujiona wewe ndio una matatizo kuliko watu wote ni shida ya akili inawezekana kabisa hayo matatizo uliyonayo ni madogo sana kulinganisha na hao wenzako unaosema wana Neema Tele.
Wahi kwa wataaamu wakusaidie.
Okay.
 
Kama MUNGU hana msaada wowote kwako,,hivi hiyo pumzi unayovuta unailipia kiasi gani kwa siku?

Yule anayekulaza na kukuamsha kila siku asubuhi unamlipa kiasi gani?

Viungo vyako vya mwili kuendelea kufanya kazi vikiwa salama unalipia kiasi gani?

Kama basi huna shukran kwa muumba wako inapasa kusema kwamba FIRAUNI na wafuasi wake bado wanaishi duniani.
Mbona hata sikumuomba anilete duniani? Hii pumzi Ina mwisho wake kwani unahisi nitaishi milele?
 
Mikosi, Kila kitu kibaya Mimi. Dhambi zangu hazijai hata kikombe lakini niliyoyapitia ni magumu kuliko umri wangu.

Lakini ukitazama wengine kwenye matendo maovu yote huwakosi, Ila wamejaa neema tele. Kila kitu kizuri kwao.

Ninapoelekea naenda kutokumwamini huyu kiumbe wa kuitwa Mungu. Maana kama kweli yupo ni mtesaji na mnyanyasaji kweli.
NIMEMALIZA.
Pole sana. Kupitia magumu ni maisha ambayo yanafikirisha sana, ila kunakuimarisha na kuwa mfano kwa wengine wa kutokata tamaa (kuwa mvumilivu) kunakotakiwa katika maisha. Kila mmoja wetu anapitia katika maisha fulani, ambayo anaweza kuyaona ni magumu kuliko ya watu wengine, na wakati huo huo wengine nao wanaoonekana wana maisha mazuri wanatamani wangeishi maisha tofauti na hayo. Mfano, wewe unaweza kuwa unatamani maisha ya X na X anatamani maisha ya Y na Y anatamani maisha ya Z, nk.

Niliwahi kuishi Malawi na jirani yangu alikuwa mtu mwenye maisha mazuri sana (kwa jinsi alivyoonekana): nyumba nzuri, gari zuri, mke mzuri na alikuwa akiwasaidia sana ndugu zake kutoka kijijini na hata watu wengine. Kama uko karibu naye na ukikwama ukimwomba msaada wa fedha anakuuliza "ungetaka nikupe cash au nikurushie kwenye simu"? Ukisema "cash" anakupa, na ukisema "nirushie" anakurushia kiasi ulichomwomba. Kwa hiyo, mimi na mke wangu nilimwona ni mtu mzuri na mwenye moyo wa kusaidia watu, lakini watu wa nyumbani kwake, akiwemo mkewe, walimwona mtu asiye mstaarabu na wakati fulani hata mkewe alimkimbia na kurudi kwao kwa madai kwamba anamnyanyasa na hakuona kama maisha wanayoishi ni maisha ya heri. Hata ndugu zake waliokuwa naye walikuwa hawana raha, hasa anapokuwepo nyumbani, labda kama yuko safarini au kazini. Kwa nini wakati ni familia iliyokuwa inaonekana mambo yanawaendea vizuri almost katika kila jambo na watoto walikuwa wakisoma shule nzuri - walikuwa wakifuatwa kwa gari na kurudishwa nyumbani kwa gari? Watoto wa watu wengine walikuwa wakitembea kwenda shuleni na kurudi nyumbani.

Kuna mfano mwingine pia, familia yenye uwezo kifedha ambayo familia nyingine zilikuwa zikitamani maisha yake, mke mtu alizaa na fundi aliyekuwa akifanya matengenezo nyumbani kwao, tena mara 2. Umeshawahi pia kuona baadhi ya watu wenye uwezo kimamlaka au kifedha wanavyolindwa! Unakuta mtu X ana nyumba nzuri sana iliyozungushiwa ukuta mrefu na juu ya ukuta ameweka nyaya za umeme, mageti imara kwenye lango kuu lna dogo la ukuta, na hata kwenye mlango wa nyumba na milango ya vyumbani, na ana walinzi wenye silaha na yeye ndani ana bastola na silaha nyingine pia.

Lakini unaweza kukuta mtu maskini kijijini, nyumba yake ni ya nyasi na mlango kaweka gunia na upepo ukivuma unaona hata kitanda chake au anaweza akawa ameweka mlango wa matete ambao kufuli lake ni kamba na hata kama amefunga kwa hiyo kamba unaweza kufungua na kuingia bila shida. Lakini je kati ya yule anayelindwa kwa silaha na huyu ambaye mlango wa nyumba yake ni gunia, ni nani unadhani anaishi bila wasiwasi wa maisha? Nani anaona hana usalama wa kutosha?

Hivyo, utagundua kwamba maisha unayoyatamani kuyaishi kwa sababu unaona mtu au watu wengine wakiyaishi vizuri, watu hao pia wanatamani maisha tofauti na kila mtu yuko hivyo. Hali hii yote inaonyesha maisha yetu wote - awe tajiri au maskini - yana upungufu fulani na tunatamani tufikie ukamilifu na huo ukamilifu tunaoutamani ndipo Mungu alipo au niseme ndiye Mungu mwenyewe na kila mmoja wetu anatamani hivyo. Kwa hiyo, hiyo hali unayokutana nayo kiuhalisia unatamani ukamilifu wa maisha yako, maana umeona kwamba maisha unayoyaishi hayatoshi, unatamani maisha tofauti na hata ukiwa na maisha tofauti na uliyonayo kwa sasa, bado utaona tu kuna mambo hayaendi hadi hapo utakapofikia ukamilifu wenyewe. Katika maisha ya ndoa tunapitia 'experience' hiyo pia.

Unapokuwa kijana ukimwona msichana fulani anakuvutia na unaona ni mzuri kuliko wengine na unatamani umwoe. Utakwenda kuwaambia wazazi na ndugu zako kwamba umepata mchumba, lakini baada ya kuoana utaona kwamba uzuri uliokuvutia hauko kwa huyo uliyemwoa, na utaanza kutamani umwoe msichana au mwanamke mwingine unayeona ni mzuri kuliko huyo uliye naye, na unaweza kuoa hata mke wa pili, ambaye unadhani ni mzuri zaidi ya huyo uliye naye. Ukishaoa, baadaye utaona si mzuri kama ulivyodhani, na utatamani mwingine uliyemwona mahali fulani na unaweza kufanya juu-chini umwoe huyo. Naye ukishamwoa, bado utaona kama mwanamke mwingine uliyekutana naye mahali hivi karibuni ndiye mzuri zaidi na ndiyo maana unakuta mtu kaoa/kaolewa, lakini anachepuka na mke/mume wa jirani...na hali hii itaendelea vivyo hivyo hadi wewe mwenyewe utakapoona kwamba huoi tena...na hii yote ni kuonyesha kwamba uzuri hauna mwisho na kila mara utaona ulichonacho si kizuri, bali cha mwenzako ndicho kizuri zaidi - hadi utakapofikia ukamilifu wa maisha yako, ambao ndiye Mungu mwenyewe.

Kuna mfano fulani kwamba mtu fulani aliona maisha yake ni magumu zaidi kuliko ya watu wengine. Siku moja katika kulalamika kwake alikutana na "Mungu" na akamwambia "kwa nini umenipa maisha kama haya tofauti na ya wengine?" Huyo "Mungu" akamuuliza, "una uhakika?" Akasema "ndiyo." Basi Bwana Mungu akamchukua ili akachague maisha anayoyapenda, kisha arudi duniani ayaishi. Maisha ya watu wote alikuwa ameyapanga kwa mfano wa msalaba. "Mungu" akamwambia achagua aina ya 'msalaba' ambao anaona ni mwepesi kwake. Aliponyanyua 'msalaba' wa kwanza akaona ni mzito sana, akaachana nao, akaenda kwa wa pili, nao akaona bado ni mzito.

Basi aliendelea hivyo, hadi akafika mahali akaona 'kamsalaba', alipokanyanyua, akaona kepesi, na akaona "haka kananifaa, maana ile misalaba mingine ni mizito sana.' Basi akamwendea Bwana Mungu na kumwambia "nimeridhika na haka kamsalaba." Bwana Mungu akamuuliza, "umejiridhisha kama kanakufaa, labda ungetafuta kengine!" Yeye akasema "kati ya misalaba yote, hako ndiko nimeona ni nafuu zaidi." Basi Mwenyezi Mungu akamwambia "safari njema". Huyo mtu alirudi duniani na alipofika kuanza kuishi akakuta "kale kamsalaba" alikokachagua ndiko kalikuwa "maisha yake ya awali".

Fundisho la simulizi hili ni kwamba, kila mtu ana maisha ambayo anaweza kuyamudu. Chukulia wewe ni mwanafunzi umepewa mitihani miwili ya kufanya (Hisabati): mtihani mmojajawapo (mtihani A) maswali yake ni rahisi sana na ungeweza kujaza hata umefumba macho na ulipoufanya ukapata 100% na mwingine wenye maswali magumu sana (mtihani B) na ulipofanya ukapata pia 100%. Je, ni mtihani upi utapenda kuwaonyesha rafiki zao kwamba umeufaulu vizuri zaidi? Ni mtihani A au mtihani B, na kwa nini? Asante.
 
Oya Babu kazi nafanya.
Hatujui kipato chako na matumizi yako...
Ila jitahidi kuweka akiba ili uweze kuanzisha chanzo kipya cha mapato...kumbuka akiba ni muhimu ila usijibane kula..., bana matumizi yasiyo ya lazima.
 
Mikosi, Kila kitu kibaya Mimi. Dhambi zangu hazijai hata kikombe lakini niliyoyapitia ni magumu kuliko umri wangu.

Lakini ukitazama wengine kwenye matendo maovu yote huwakosi, Ila wamejaa neema tele. Kila kitu kizuri kwao.

Ninapoelekea naenda kutokumwamini huyu kiumbe wa kuitwa Mungu. Maana kama kweli yupo ni mtesaji na mnyanyasaji kweli.
NIMEMALIZA.
MUNGU ni mwaminifu katika ahadi zake.
Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtaona, bisheni nanyi mtafunguliwa.

Ukiwa unasali, tamka na haya maneno, halafu nenda kapambane, utakuja kutoa ushuhuda humu, siku moja.

Mim siyo mwema sana, Ila ni miongoni mwa wale, waliofikia hatua za mwisho za kukata tamaa.
 
Hapana, wewe huelewi logical non sequitur fallacy unayoifanya tu.

Na huo ni uthibitisho Mungu hayupo.

Angekuwepo, asingeumba mtu mjinga kama wewe.
Thibitisha uwepo wako wewe mwenyewe umechemka, haya swali jepesi zaidi, thibitisha kuwa "wewe si mjinga"

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Thibitisha uwepo wako wewe mwenyewe umechemka, haya swali jepesi zaidi, thibitisha kuwa "wewe si mjinga"

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
Bado unafanya logical non sequitur fallacy.

Tatizo insonekana hujui logical non sequitur fallacy ni nini.

Hata nisipoweza kuthibitisha chochote, hilo halithibitishi Mungu yupo.

Thibitisha Mungu yupo.
 
Mikosi, Kila kitu kibaya Mimi. Dhambi zangu hazijai hata kikombe lakini niliyoyapitia ni magumu kuliko umri wangu.

Lakini ukitazama wengine kwenye matendo maovu yote huwakosi, Ila wamejaa neema tele. Kila kitu kizuri kwao.

Ninapoelekea naenda kutokumwamini huyu kiumbe wa kuitwa Mungu. Maana kama kweli yupo ni mtesaji na mnyanyasaji kweli.
NIMEMALIZA.
Mwenyezimungu anatupa mitihani viumbe wake ili kutupima imani zetu
 
Moja ya njia ya kutatua tatizo kubwa ni kulivunjavunja katika sehemu ndogo na kuzitatua hizo sehemu ndogo ndogo.

Suala la Mungu ni kubwa sana, na hata kum define tu Mungu ni tatizo.

Ndiyo maana nikaanza hapa, tumalize ngazi ya jwanza kabla ya kupanda ya pili.

Kwa hiyo tumekubaliana huyu Mungu mjuzibwa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote hayupo?

Tumalizane hapo kwanza kabla ya kwenda kwingine.
sijui kama yupo au hayupo!
 
Kwa mantiki hiyo Mungu haongozi maisha ya ulimwengu?
Nina wasiwasi haujanielewa.

Ila cha msingi kama unapitia changamoto hizo fuata tu huo ushauri utaona mabadiliko.

Fikilia kwanini unaviungo vyenye misuli yenye nguvu ni kwasababu ili uweze kufanya kazi katika mazingira ya hapa duniani.

Kwanini una viungo vya uzazi na wehenga wakakazia mficha uchi hazai, kwaiyo ili upate familia ni lazima ushughulike.

vivyo hivyo tumepewa Akili na ufahamu ni ili kupambana mambo kwa kadili ya changamoto na mazingira tunayokutananayo ukiona njia plani hii haifanikiwi unahadilisha nyingine.

Yaani design yote ya mwili wa viumbe hai ume dezainiwa mahsusi kwa kujitegemea na ndio lengo kuu.

Ukihisi kunajambo haiwezekani hapa duniani basi tambua kua ni fikra zako tu! Kutokana la kiwango cha ufahamu/mazingira uliopo na exposure uliopitia. Mambo yanawekana ni Juhudi /imani yako tu juu ya jambo husika ndio itakayoamua.

Fikilia wewe umeunda gari limekamilika mifumo yote iko vizuri gali linatembea bila shida yoyote, kutakua na haja yakulikokota tena, yaani uanze kulivuta inakua haina maana yakuliunda hilo gari. Ndio hivyo tulivyoumbwa. Kikubwa tufuate ile specification na user manual tuliopewa
 
Usikate tamaa kwa kuhisi au kuamini Mungu hana msaada na wewe.

Mungu anakupenda na kukuwazia yaliyo mema, ndiyo maana kakuumba na bado amekulinda hadi sasa uko hai.

Hayo mengine ni mapito tu na yana mwisho.

Omba rehema kisha mrudie kwa unyenyekevu na utiifu Mungu naye atakuvusha katika changamoto unazopitia.
Post ya juu yako na hii yako imenionesha aina mbili tofauti za binadamu at an instant

Post ya juu yako imejaa ukatili, jamaa hana huruma na mtoa mada hajajiweka kwenye miguu yake
Anajiita mtu wa Mungu na nadhani ni more problematic kuliko mtoa mada

Post yako imejaa utu , ubinadamu na hekima

Dunia ingekua sehemu salama sana kama ingekua na watu wengi kama wewe
 
  • Thanks
Reactions: K11
Ni sawa na useme mume wa jirani yangu Hana msaada na Mimi na ni TAJIRI, sasa huyo ni Mumeo? Lazima awe wako ndo akusaidie!

Mungu ana msaada kwa watu wenye mahusiano naye, na Kama ungewahi Kuwa na mahusiano naye usingeropoka na kumdharau!

Nani alikwambua watu wote wenye navyo wamepewa na Mungu unayemlaumu? Hata shetani utoa mafanikio yenye majuto!!! Why don’t you try him uone balaa Lake????

Angalia watu Kama Yusufu, Ayoub na wengine wengi kwenye Biblia, walipita balaa za kutosha, wakavumilia mwisho we wakamwona Mungu! Unajua kwa nini hawakukufuru Kama wewe ? Kwa Sababu wamamjua!

Yani watu Kama wewe wa naweza kufa huku wanatukana Mungu Mwenye uwezo wa kukusaidia; hauna mahusiano na huyu Mungu hata kidogo; kufa tu brother na laana zako na Umaskini!!!

Die hard brother Kama hutaki kumfaham na kumwelewa huyu Mungu namna ambavyo anafanya kazi zake ( He is a principled God ) go die, killl yourself, die baby die!
Upo sahihi kabsa
 
Mikosi, Kila kitu kibaya Mimi. Dhambi zangu hazijai hata kikombe lakini niliyoyapitia ni magumu kuliko umri wangu.

Lakini ukitazama wengine kwenye matendo maovu yote huwakosi, Ila wamejaa neema tele. Kila kitu kizuri kwao.

Ninapoelekea naenda kutokumwamini huyu kiumbe wa kuitwa Mungu. Maana kama kweli yupo ni mtesaji na mnyanyasaji kweli.
NIMEMALIZA.
Kwani kipimo cha kuwa na Mungu ni mali??
Mimi najua kipimo cha kuwa na ibilisi cha kwanza ni kutokuwa na shida yoyote ile,

Ukishakuwa mkristo halisi na wakweli basi jua kitambo upo kwenye mapambano,
Inamana wakinapetro,wafia imani,stefano nao wangelaumu kama wewe+?

Napia nakukumbusha wakati ambao kuna ukimya sanaaaa basi jua Mungu u ndio yupo karibu sanaaa.
Mimi ni shahidi wa hayo.

Badala ufurahi kuwa upo mbali sana kiimani ndomana mambo makubwa yanakupata
Maana imeandikwa jaribu halikumpata mtu kabla mungu hajalipima akaliruhusu
 
Back
Top Bottom