Mungu haponyi ni juhudi za madaktari na wewe binafsi, lakini je ameshamaliza kuumba?

Mungu haponyi ni juhudi za madaktari na wewe binafsi, lakini je ameshamaliza kuumba?

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
25,968
Reaction score
36,044
Je Mungu alishamaliza kuumba ?


Tunatambua Mungu aliumba ulimwengu kwa siku 6 na ya saba akapumzika, sasa je baada ya hapo hakupumzika tena mpaka leo imekuwa tu mwendo wa kuumba viumbe wapya kuanzia binadamu ,wanyama, wadudu ,mimea nk?

Au ameset kila kitu kwenye automode kiwe kinajiendesha tu mpaka ulimwengu utakapofika tamati ?

Tunatambua ila baada ya sekunde kadhaa mimba mpya zinatungwa kutoka kwa watu wa sehemu mbalimbali duniani ,nyingine zinaendelea kukua , kuna wadudu wapya, wanyama, mimea nk sasa je systems zinajiendesha automatically au bado anaumba tu?


Kuhusu suala la uponyaji sidhani kama Mungu anaponya, ingekuwa Mungu anaponya kusingekuwa na sababu watu kwenda hospitali kutafuta matibabu yao ya kiafya badala yake wangeshinda na kuomba kwenye nyumba za ibada.

Leo hii ukiona mtoto kazaliwa na mapungufu fulani (Congenital abnormalities) asilimia kubwa inatokana na mzazi kuanzia life style yake, family history, genetics nk.

Mfano mtoto kazaliwa na kichwa kikubwa (hudrocephalus) au mgongo wazi (spinal bifida) ,hiyo haisababishwi na Mungu ni uzembe wa mama kutokuwa folic kipindi cha ujauzito.

Ukiona mtoto ni mzito mzito kuelewa mambo /kilaza asilimia kubwa tatizo limetokana kipindi anazaliwa huenda kuna makosa yalifanyika imepelekea mtoto kupata delayed milestone na kumuathiri ukubwani.

Hata tukiwaangalia wagonjwa wanaoishi na VVU wasipokunywa dawa zao ndani ya muda mfupi wanafariki, hivyo suala la kusema Mungu anaponya sio kweli, bali ukweli ni juhudi za madaktari na umakini wa mgonjwa kuzingatia maelekezo sahihi anayopewa na daktari aliyemuhudumia.
 
Sifa kubwa ya Mungu haonekani kama umbo . Yy yupo kila sehemu, kwenye majeraha yupo, kwenye kifo yupo, kwenye maji, yupo ndani ya mwanadamu, na cell zake zote za mwili. Na yy ndiye Chanzo cha kila kitu Kama unataka kumuona kama umbo ambalo madaktari wanao au wanyama wanao Kufa kwanza ndio mlango pekee wa kumuona Muumbaji.Ila kwa kifupi yy tupo hata kabla ya pumzi yako yuko karibu na ww kuliko pumzi yako.
 
Dunia ina miaka zaidi ya bilioni 4.5, Kuna ushahidi mzito zaidi wa evolution kuliko uumbaji.
 
Sisi ni matokeo ya matendo yetu wenyewe, mungu tunamsingizia Kwa Kila Hali kitu ambacho ni makosa...Binadamu ni kama roboti ambalo limetengenezwa na kuachwa lijiamulie mambo lenyewe...Roboti likifikia Hali mbaya Kwa namna zote basi divine intervention ya mtengenezaji inahusika.
 
Back
Top Bottom