Hahah....kwahyo wewe unaamini binadamu wa kwanza aliishi pale Iraq miaka 6000 iliyopita?
Wakati kuna mafuvu yanapatikana ulimwenguni kote ya zamani kuliko hiyo? Hapa Bongo tu kuna fuvu la binadamu kama wewe pale Ngorongoro, huyo binadamu kaishi miaka zaidi ya laki 2 ilyopita.
Adam ni binadamu wa kwanza kwenye tamaduni za kiyahudi (ambazo wakristo na waislam walizirithi.)
ila ukienda India tu hapo kuna vitabu vya dini ambavyo vimeandikwa zamani kabla hata Adam hajazaliwa. (Vedas)
Ukiacha hiyo...kuna Miji ilikuwepo kabla hata adam hajazaliwa..Sehemu kama Mesopotamia zaidi ya miaka 7000 uko.
Haiwezekani Adamu yupo na Eva uchi kwenye bustani wanashauriana kula tunda muda huohuo kuna watu wameshaadvance wanalima ardhi, wanatengeneza miji, wanaandika maandishi,nk.
Ndomaana hata bible inasema Cain mtoto wa adam alipoemda mbali alikutana na mji wenye watu.