Mungu kama upo unapaswa kuniomba msamaha

Mungu kama upo unapaswa kuniomba msamaha

Kila mtu ana safari zake za peke ake kutafuta amani ya kuishi hapa duniani.

Usikate tamaa.
 
Duh! Mungu baba msamehe huyu hajui alitendalo, Usidhani ww ndo unaepitia magumu sana, kuna sisi wengine tunapambana kwa jasho na damu ila hatuoni mwangaza mbele na nyumbani tumetoka zamani sana na hatujui kama huko nishaesabiwa nishakufa ila sina budi kwa kumshukuru Mungu kwa afya aliyonijalia na familia ninayohaso nayo kwani naamini ipo siku yangu japo kipato nacholipwa ni kidogo hata hakitoshi kutunza familia....hebu tubu mwambie Mungu me ni mkosefu kwa kauli hiyo,
 
Kila mtu yupo duniani kwa kusudi flani usikate tamaa mkuu ht kama unapitia magumu kiasi Gani kesho yako huwezi jua
 
Habari wanajamiiforums?
Leo nina kesi na Mungu, Kama yupo kweli anapaswa aniombe msamaha.

Sijawahi kumkosea kwa chochote ila yeye amenikosea mara nyingi zaidi.

Pia, Sikumuomba anilete duniani, ila yeye alinileta bila ridhaa yangu kisha aninyime kila ninachostahili.

Mungu toka ulipo uje uniombe msamaha.
Hizi mada za kipumbavu zitawagharimu siku moja. Shauri yenu
 
Umekufuru utubu kabla hasira ya Mungu haijawakaa juu yako
 
Nachangia huu uzi kwa tahadhari ila kuna vitu nimejifunza kuhusiana na Mungu.

Ni kwamba katika maongezi yako na maombi na yeye, kama kweli unajiona wewe msafi au ukishajitakasa unaweza kuongea naye kwa kumshawishi kama mshkaji wako tu ila heshima bado iwepo na umpatie utukufu wake.

Yakobo si alipigana mieleka na Mungu hadi Mungu akambariki?

Kuna siku nikitulia nitakuja na mada hii ya jinsi ya kumshawishi Mungu ili akubariki au akupe kile unachotaka.
 
Maisha hayawahi kuwa perfect Mimi n wewe Tupo ktk nchi isiyo na vita lakini kuna wengine wapo Syria huko wapo Ukraine huko wanakufa kama vifaranga vya kuku Au sisimizi , Ukitaka Kuya fahamu maisha na dunia usiangalie ktk upande wako pekee itazame dunia nzima Ilivyo kisha tafakari
Hiyo ni balance of nature maisha yapo hivo hivoo huyu anapata huyu anakosa
 
Back
Top Bottom