Mungu maana yake ni nini? Au Mungu ni nini?

Mungu maana yake ni nini? Au Mungu ni nini?

Huo mchakato wote (observation na majaribio) mpaka ugunduzi wa mitambo unafanyika au inategenezwa, ni jambo la ufahamu au sio jambo la ufahamu?
Ni ufahamu katika ulimwengu unao onekana na kuthibitishika upo.

Ni ufahamu unao tokea ndani ya ulimwengu unao onekana na unaoweza kufanyiwa observation na majaribio..
 
Ulimwengu hauna chanzo, Ulimwengu ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo.
ninyi wajuaji sana mnajitekenya na kucheka wenyewe.
kubalini kwamba Mungu yupo kama anavyosimuliwa na Biblia na qorani ikanakili hivyo
Mungu hana chanzo ,alikuwepo na ataendelea kuwepo
huwezi amini za kufikirika, ukakataa ukweli uliosimuliwa
Malaki 3:6 na Waebrania 13:8 zote mbili zinatangaza kwamba Mungu ni yeye yule siku zote na habadiliki kamwe. Yeye ni mzuri kila wakati, mwenye upendo kila wakati, mwenye nguvu zote. Haijalishi jinsi ulimwengu huu unavyobadilika karibu nasi, tunaweza kuamini kwamba Mungu ni thabiti. Ni yeye yule jana, leo, na hata Milele!
 
Huyo Mungu mnahangaika sana kumwelezea na kumuongelea kwa vile Hayupo kujiongelea mwenyewe wala hawezi kujidhihirisha kwamba yupo.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
 
Uwepo huo wa hali ya juu wenye ufahamu ndio huo ulimwengu wenyewe.

Kuita uwepo huo mara sijui nguvu/ Akili/ Mungu ni kupachika pachika tu majina uchwara.

Uwepo huo wenye ufahamu wa hali ya juu ndio ulimwengu.
Nimekueleza hili awali na nafikiri ama unachanganya au hujaelewa.

Unachochanganya ni ulimwengu. Kwamba, kwa upande mmoja, ulimwengu ni vitu vyote vilivyopo, na kwa upande mwingine ni Uwepo wa Hali ya Juu Wenye ufahamu.

Ulimwengu ni nini?

Jibu au fuatilia ulimwengu maana yake ni nini?
 
Nimekueleza hili awali na nafikiri ama unachanga au hujaelewa.

Unachochanganya ni ulimwengu.

Ulimwengu ni nini?

Jibu au fuatilia ulimwengu maana yake ni nini?
Ulimwengu ni kila kitu na kila kitu ni sehemu ya ulimwengu.
 
Ni ufahamu katika ulimwengu unao onekana na kuthibitishika upo.

Ni ufahamu unao tokea ndani ya ulimwengu unao onekana na unaoweza kufanyiwa observation na majaribio..
Kwa maneno mengine unakubali kuwa observation na majaribio, ni mambo yalio na yanayofanyika kwa akili; na ugunduzi au mitambo ni pia mambo ya akili.
 
Yanafanyika na binadamu sio akili.

Akili ni neno la kutungwa tu, kuonyesha ufanyaji kazi wa ubongo.
Binadamu ni mnyama au sio mnyama?

Je, binadamu ndiye kiumbe mwenye ubongo peke yake kati ya wanyama wote waliopo?

Je, ubongo wa wanyama wengine haufanyi kazi?

Je, ufanyaji kazi wa ubongo wa wanyama wengine, ni tofauti na ufanyaji kazi wa ubongo wa binadamu?
 
Binadamu ni mnyama au sio mnyama?
Binadamu sio mnyama ila ana baadhi ya sifa zinazo fanana na mnyama.

Ni sawa na kusema Twiga(mnyama) ni binadamu kwa vile binadamu ni mnyama.

Ila Twiga hawezi kuwa binadamu, Anabaki kushea baadhi ya sifa chache tu za kibinadamu.
Je, binadamu ndiye kiumbe mwenye ubongo peke yake kati ya wanyama wote waliopo?
Hapana ubongo upo kwa kila kiumbe, ila ubongo wa binadamu ndio wenye uwezo mkubwa wa ufanyaji kazi ambapo uwezo huo ndio uliitwa Akili.
Je, ubongo wa wanyama wengine haufanyi kazi?
Unafanya kazi ila si kwa kiwango kikubwa kama ulivyo ubongo wa binadamu.

Kwa sababu binadamu sio mnyama, tunashea sifa chache tu za wanyama.
Je, ufanyaji kazi wa ubongo wa wanyama wengine, ni tofauti na ufanyaji kazi wa ubongo wa binadamu?
Ndio ni tofauti kwa sababu binadamu sio mnyama...

Binadamu hushea sifa chache za wanyama.

Kumwita binadamu mnyama kwa vile tu hushea sifa chache na wanyama ni sawa na kusema Twiga ni binadamu kwa vile binadamu ni mnyama.

Lakini kiuhalisia kuna utofauti mkubwa sana wa binadamu na mnyama na huwezi kuwafananisha kwenye kila kitu.
 
Kitu kinawezekana kuwepo pasipo kufanyika au kutengenezwa?
Ndio kinawezekana.

Kama kila kitu kilichopo lazima kiwe na mtengenezaji wake, Hata mtengenezaji wa kila kitu atahitaji awe na mtengenezaji wake.

Na kama sio lazima kila kitu kiwe na mtengenezaji wake, Basi hata ulimwengu na vitu vyote vilivyomo ndani yake, Havihitaji kutengenezwa.
 
Ndio ni tofauti kwa sababu binadamu sio mnyama...

Binadamu hushea sifa chache za wanyama.

Kumwita binadamu mnyama kwa vile tu hushea sifa chache na wanyama ni sawa na kusema Twiga ni binadamu kwa vile binadamu ni mnyama.

Lakini kiuhalisia kuna utofauti mkubwa sana wa binadamu na mnyama na huwezi kuwafananisha kwenye kila kitu.
Umesoma bailojia au hata umejinza bailojia?

Unajua maana ya mnyama?
 
Isaya 40:28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.

Sasa utawezaje kumuelezea mungu? kwasabab akili zake hazichunguziki nizahali ya juu mfano wa hizi akili hakuna mwana sayansi mwenyeuwezo wakutengeneza mnyama mwenye uhai na mnyama akifa hawezi kurudi kwenye uhai wake ki science na nikwann haiwezekani kwann kwa vitu vingine kuna recycling ya uwepo wake na unaonekana mfano mimea utakula embe utachukua kokwa utapanda je binadam ukifa je ww unaenda wap je ndio mwisho? Kwann jina mungu linatajwa spontaneously hata kwa mpagani hata mtu asipoonesha kukili hapa kutambua uwepo wa mungu
Kitu kinawezekana kuwepo pasipo kufanyika au kutengenezwa?
 
Ni sawa na kusema Twiga(mnyama) ni binadamu kwa vile binadamu ni mnyama.
Je, twiga hana milango ya fahamu? Na binadamu hana milango ya fahamu?

Ni kiungo gani muhimu ambacho binadamu anacho lakini twiga hana?

Kwa jinsi gani kiumbe kiwe na sifa ya kufanana na mnyama lakini kisiwe mnyama?
 
Majibu ya maswali ya mleta mada yote yapo kwenye Qur'an pekee.

Qur'an 17:110. Sema: Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolote mnalo mwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri. Wala usitangaze Sala yako kwa sauti kubwa, wala usiifiche kwa sauti ndogo, bali shika njia ya kati na kati ya hizo.
 
Je, twiga hana milango ya fahamu? Na binadamu hana milango ya fahamu?

Ni kiungo gani muhimu ambacho binadamu anacho lakini twiga hana?

Kwa jinsi gani kiumbe kiwe na sifa ya kufanana na mnyama lakini kisiwe mnyama?
Na kwa jinsi gani kiumbe kiwe na sifa ya binadamu lakini kisiwe binadamu?

Kwa nini Twiga sio binadamu?
 
Back
Top Bottom