Mungu maana yake ni nini? Au Mungu ni nini?

Hicho kinachomfanya binadamu (mtu) kuwa wa kipekee kati ya wanyama wengine (akili) ndio wewe unakana.

Kwa maneno mengine, wewe mwenyewe unajikana huna ufahamu. Pia hata ujuzi wa kuandika, au kuunda au kutunga maneno, unavyoandika hapa unaukana.
Ndio maana nikakwambia binadamu sio mnyama.

Sasa kama binadamu ana akili kama unavyodai, Utasemaje tena binadamu ni mnyama?

Huoni kwamba una jichanganya mwenyewe?
 
Nipo Kwa sababu nilizaliwa.

Na kabla sijazaliwa sikuwepo na nikifa pia sitakuwepo.
Kwanini wewe usiendelee kuwepo tu kama ilivyo madai yako kuhusu ulimwengu kwamba ulimwengu ulikuwepo na utaendelea kuwepo ??

Hukuwepo, Ukawepo, Then badae utadisappear ( Kufa )

Haya maswali umewahi kujiuliza ? Au wewe umeamua kuishi njia ya "mjinga" kwamba unaishi kwa kadri ya mambo unayoyafahamu tu
 
Hivi kama watu na viumbe wangekuwa wanaendelea kuwepo tu bila kufa, ulimwengu ungetosheleza ku accommodate population yote ya binadamu na viumbe wengine wote kwa wakati wote?

Ninyi ndio wajinga mnaoishi njia za kijinga mnaamini kuna mbingu yenye maisha bora ila kufa hamtaki.

Mnang'ang'ana kuishi kwenye ulimwengu huu huu.
 
Sasa kama binadamu ana akili kama unavyodai, Utasemaje tena binadamu ni mnyama?
Hii umemaanisha: binadamu ni binadamu na sio mnyama kwa sababu ya kuwa na akili.

Hatahivyo, wakati huo huo umesema akili ni dhana ya kufikirika tu, haipo.

Sasa, inawezekanaje binadamu asiwe mnyama kama hali yake ya akili ni ya kufikirika tu, haipo?
 
Hivi kama watu na viumbe wangekuwa wanaendelea kuwepo tu bila kufa, ulimwengu ungetosheleza ku accommodate population yote ya binadamu na viumbe wengine wote kwa wakati wote?

Ninyi ndio wajinga mnaoishi njia za kijinga mnaamini kuna mbingu yenye maisha bora ila kufa hamtaki.

Mnang'ang'ana kuishi kwenye ulimwengu huu huu.
Umepanick ? Mbona unaandika ambayo sijayasema
 
Hivi kama watu na viumbe wangekuwa wanaendelea kuwepo tu bila kufa, ulimwengu ungetosheleza ku accommodate population yote ya binadamu na viumbe wengine wote kwa wakati wote?

Ninyi ndio wajinga mnaoishi njia za kijinga mnaamini kuna mbingu yenye maisha bora ila kufa hamtaki.

Mnang'ang'ana kuishi kwenye ulimwengu huu huu.
Hata kwa hilo ilibidi ujiulize kuwa ni kivipi tunakufa ili kubalance population ulimwenguni kama maoni yako yanavyosema, kwanini tusingekuwepo tuu
 
Hii umemaanisha: binadamu ni binadamu na sio mnyama kwa sababu ya kuwa na akili.

Hatahivyo, wakati huo huo umesema akili ni dhana ya kufikirika tu, haipo.

Sasa, inawezekanaje binadamu asiwe mnyama kama hali yake ya akili ni ya kufikirika tu, haipo?
Akili ni neno la kutungwa linalomaanisha ufanyaji kazi wa ubongo wa binadamu au kiumbe chochote.

Hata wanyama wana huo ufanyaji kazi wa ubongo wao ambao kwa ujumla tunauita Akili.

Akili ni neno dhahania sawa na kusema pumzi, njaa, kiu, hofu n.k vyote hivi hata wanyama wanavyo.

Binadamu sio mnyama kwa sababu ufanyaji kazi wake wa ubongo (Akili) ni mkubwa sana na wa tofauti kuliko wa wanyama wengine..
 
Hata kwa hilo ilibidi ujiulize kuwa ni kivipi tunakufa ili kubalance population ulimwenguni kama maoni yako yanavyosema, kwanini tusingekuwepo tuu
Ndivyo nature ilivyo, ili wengine wapate kuishi lazima wengine wapungue kwa kufa.

Ulimwengu ambayo ndio nature yenyewe hujibalance wenyewe.

Na sisi binadamu na viumbe vyote ni sehemu ya hiyo nature..
 
Akili ni neno la kutungwa linalomaanisha ufanyaji kazi wa ubongo wa binadamu au kiumbe chochote.

Hata wanyama wana huo ufanyaji kazi wa ubongo wao ambao kwa ujumla tunauita Akili.

Akili ni neno dhahania sawa na kusema pumzi, njaa, kiu, hofu n.k vyote hivi hata wanyama wanavyo.

Binadamu sio mnyama kwa sababu ufanyaji kazi wake wa ubongo (Akili) ni mkubwa sana na wa tofauti kuliko wa wanyama wengine
Sawa.

Nini kimefanya ufanyaji kazi wa ubongo wa binadamu kuwa mkubwa na wa tofauti kuliko wa wanyama wengine?
 
Nature yenyewe.

Kwa sababu kila kitu ni sehemu ya nature.

Hivyo kila kitu kinafanyika chenyewe kwa vile kila kitu ni nature hiyohiyo.
 
Ndivyo nature ilivyo, ili wengine wapate kuishi lazima wengine wapungue kwa kufa.

Ulimwengu ambayo ndio nature yenyewe hujibalance yenyewe.

Na sisi binadamu na viumbe vyote ni sehemu ya hiyo nature..
Basi hii nature ndio ufahamu wa hali ya juu kuliko fahamu/akili zote ( Kufanyika )
 
Hata wewe ni sehemu ya hiyo Nature.

Na huwezi kujitenganisha na hiyo nature kusema kwamba kuna nature nyingine tofauti iliumba nature unayo iona na uliopo ndani yake..
 
Upo sahihi wala hujakosea,

Ila sisi watu ambao tunafahamu na tunatambua kuna nguvu kuu ( Nature/Mungu ) tunaamini ni nguvu ambayo ipo ndani yetu pia na ndio iliyofanya kuwepo kwa kila kitu kilichopo.
 
Hapo sawa.

Mimi ninacho pingana na watu sana sana ni kudai kwamba sisi binadamu tuliumbwa na hiyo nature ambayo kiimani mnaiita mungu, ilhali hata sisi binadamu wenyewe ni nature hiyohiyo.
 
Ndivyo nature ilivyo, ili wengine wapate kuishi lazima wengine wapungue kwa kufa.

Ulimwengu ambayo ndio nature yenyewe hujibalance yenyewe.

Na sisi binadamu na viumbe vyote ni sehemu ya hiyo nature..
Maana yake hapa kuna nature ambayo hii haifi badala yake inaendelea kufanya viumbe wengine na binadamu wengine wazaliwe na waendelee kuwepo.

Hapa unakiri kwamba kuna vitu na hali. Hali ni hiyo ulioiandika nature na vitu ni ulivyoandika viumbe na binadamu.

Kwa sababu viumbe na binadamu bila hiyo unayosema binadamu na viumbe ni sehemu yake (nature), vyote (viumbe na binadamu) wanabaki tu mwili, ambao wenyewe hufa na kuharibika.

Hivyo unatakiwa kujua nature ni nini na ulimwengu ni nini.
 
Nature ni nini?

Na,

Ulimwengu ni nini?
Asili ( nature ) ni chanzo cha jambo fulani . Kila kitu kina asili yake , hakuna kitu duniani au ulimwenguni kisichokuwa na asili .

Ulimwengu ( Catholic) ni mazingira ambamo mtu huzaliwa na kuishi .
 
Akili ni neno la kutungwa linalomaanisha ufanyaji kazi wa ubongo wa binadamu au kiumbe chochote.

Hata wanyama wana huo ufanyaji kazi wa ubongo wao ambao kwa ujumla tunauita Akili.

Akili ni neno dhahania sawa na kusema pumzi, njaa, kiu, hofu n.k vyote hivi hata wanyama wanavyo.

Binadamu sio mnyama kwa sababu ufanyaji kazi wake wa ubongo (Akili) ni mkubwa sana na wa tofauti kuliko wa wanyama wengine..
Maneno ya lugha yalitungwa au yaliumbwa ili tuyatumie katika kurahisisha kuweza kuwasiliana . Hata wewe maneno unayotumia kama Logical non sequitur na mengine yalitungwa pia .
 
Back
Top Bottom