Mungu maana yake ni nini? Au Mungu ni nini?

Mungu maana yake ni nini? Au Mungu ni nini?

Kama bado sayansi inachunguza na kutafiti na hakuna anayefahamu chanzo cha ulimwengu ni nini haswa,

Hii conclusion ya kwamba ulimwengu ulifanyika huoni kwamba tayari haina ukweli?

Huoni kwamba kuhitimisha kwamba ulimwengu ulifanyika ni madai, makisio na mafikirio ya watu tu yasiyo na uthibitisho wowote ule?

Kama hujui chanzo cha akili ni nini, Utasemaje akili ndio chanzo cha kila kitu?

Huoni kwamba unafosi tu mawazo yako bila uthibitisho wowote ule?
Hivi kiuhalisia mkuu, kitu kinaweza kuwepo bila ya kufanyika, mfano ulimwengu?
 
Kwa nini unadhani kwamba ulimwengu ulifanyika?

Kwa nini hudhani kwamba ulimwengu upo tu wenyewe pasipo kufanyika.

Una thibitisha vipi kwamba ulimwengu ulifanyika?

Eleza ni wakati gani kulikuwa hakuna ulimwengu, Kisha ulimwengu ukafanyika?

Na kabla ulimwengu hauja

Kwa nini unadhani kwamba ulimwengu ulifanyika?

Kwa nini hudhani kwamba ulimwengu upo tu wenyewe pasipo kufanyika.

Una thibitisha vipi kwamba ulimwengu ulifanyika?

Eleza ni wakati gani kulikuwa hakuna ulimwengu, Kisha ulimwengu ukafanyika?

Na kabla ulimwengu haujafanyika, Huko ulikokuwa kulifanyika na nini?
Unadhan kabla hujazaliwa, ulikuwa wapi
 
Hivi kiuhalisia mkuu, kitu kinaweza kuwepo bila ya kufanyika, mfano ulimwengu?
Ndio kinaweza kuwepo.

Ulimwengu upo tu bila kufanyika.

Kama kila kitu kilichopo kinahitaji kufanyika, Hata aliyefanya vitu kufanyika atahitaji kufanyika vilevile.

Na pasiwepo kitu chochote kile kilicho jitokeza chenyewe pasipo kufanyika.

Yani kutakuwa na process za "kufanyika" zisizo na mwisho.

Na kama haiwezekani ulimwengu kufanyika wenyewe, Hata Mungu haiwezekani afanyike mwenyewe tu.
 
Umewahi kusikia au kusoma bailojia?

Unajua bailojia nini? Inaeleza vizuri unaweza kujifunza.
Nimesha kwambia hapo kwamba binadamu sio mnyama ila ana baadhi ya sifa za wanyama hata hiyo baiolojia ina eleza hivyo.

Kusema kwamba binadamu ni mnyama kwa kulinganisha sifa chache tunazo fanana na wanyama, Ni sawa na kusema wanyama ni binadamu kwa vile binadamu wanasifa za wanyama.
 
Inawezekana, kwa upande mmoja vitabu vitakatifu na mapokeo kama msingi mkuu wa mafundisho ya dini vimeibua maswali mengi kwa baadhi ya watu kuhusu Mungu.

Na kwa upande mwingine, Ukana Mungu ambao msingi wake ni kutokuwa na uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu umewavutia watu wengi katika mwelekeo huo kwa sababu ya kutokujua kama ambavyo ilivyo pia kwa wafuasi wengi wa dini.

Kile kinachoweza kuonekana kama kutoelewana - wengine wakikubali kuna Mungu na wengine wakikana hakuna Mungu, kimeendelea hata wakati ambao kuna ukuaji mkubwa wa maarifa ya sayansi na teknolojia. Na kwa kweli ni kama, kwa baadhi wasio na uelewa wa imani na sayansi, na walio na uelewa wa imani na sayansi, sayinsi imeimarisha mwelekeo wao.

Si kweli kwamba sayansi haibainishi kweli za akili, yaani kweli zilizotufikia kwa njia ya imani: mfano kuna Mungu na tokeo la uhai na ulimwengu, kwanini kuna ouvu duniani, nini hutokea baada ya kifo, nakadhalika.

Hatahivyo, pamoja na sayansi kuweka wazi mambo mengi ya imani (dini), ni dhahiri watu wengi bado hawajaelewa, na hivyo wanajiuliza:-

Je , ni kweli Mungu yupo au hayupo? Au Je, ni kweli Mungu yupo mahali pote (omnipresent)? Je, Mungu anauwezo wote (omnipotent)? Je, Mungu anajua yote, ana ujuzi wote; ana maarifa yote (omniscience)?

Na kama ni kweli! Kwa nini Mungu ambaye ni upendo, anauwezo wote, anajua yote, ana maarifa yote, ana nguvu na mamlaka yote, aumbe na aruhusu dunia ambayo inawezekana uovu kufanyika?

Kimsingi mjadala huu au maswali hayo hayawezi kuwa na maana au kujibika kama hatujui msingi wa neno Mungu, (au Hali hiyo) ambaye Ndiye mjadala wenyewe na ambaye Ndiye maswali yanaelekezwa kwake, umetokana na ni nini.

Ndugu zangu:-

Ni nini hutufanya tuseme Mungu? Yaani ni nini tunakirejelea tunapoita Mungu? Neno Mungu au wazo Mungu; au wazo kuna Mungu tumelitoa wapi? Sababu gani zimetusababisha kusema kuna Mungu; au wazo Mungu limesababishwa na nini?

Aidha, wazo hakuna Mungu limetoka wapi na limetokana na sababu gani? Na linapendekeza au linaelezea nini vitu vilivyopo?

Lakini pia, hii elimu tunayokwenda kusoma shuleni na vyuoni: kufundishwa na kusoma, (fizikia, hisabati, bailojia, kemia, jogorafia, sheria, uraia, historia, lugha, uhandisi, taalimungu (theology), elimu ya mtima (phycology), nakadhalika), imetoka wapi? Nani aliileta? Nani aliipangilia na kuiweka katika utaratibu huo? Kwa nini?

Kwa sababu kama ikiwa kila binadamu anapelekwa shule na chuo kujifunza na kusoma, maana yake hayo masomo tunayo kwenda kusoma au hiyo elimu tunayofundishwa shuleni na vyuoni hatukuwa tunaijua au tunaifahamu. Na hii maana yake ni kwamba kuna mtu aliyeijua hiyo elimu ambayo sisi tunakwenda kusoma na kufundishwa.

Sasa basi, huyo mtu aliipata wapi hiyo elimu au hayo masomo tunayofundishwa shuleni na vyuoni yalitoka wapi?

Na je, ni kweli kwamba hiyo ndio elimu (yaani hayo masomo) na kwamba hakuna kitu kingine bora zaidi au utaratibu mwingine wa kupima na kuelewa ulimwengu, ila isipokuwa kwa masomo au elimu hiyo tu?

Unauelezeaje ulimwengu: vitu vyote vilivyopo

Kadiri ya ufahamu wako na kadiri ya unavyoona na unavyoelewa, unaona vitu vilivyopo (ulimwengu ) vimefanyika kwa akili au havijafanyika kwa akili? Na je, unagundua hilo kwa jinsi gani? Je, ni baada ya kufundishwa au ni kabla? Au hugundui hivyo, badala yake unagundua nini?

Na hali hiyo ya vitu vya asili kuwa au kufanyika hivyo vilivyofanyika, inaashiria nini au unaieleza kuwa ni hali gani: yenye ufahamu au haina ufahamu?

Kwa binadamu, vitu vyote vilivyopo angalau vitu vyote anavyoweza kuviona akiwemo na mtu mwenyewe, anaona kuwa vitu hivyo au viumbe hivyo kuanzia na miundo yao ya nje na ya ndani, mpangilio wao, na jinsi yao ya utendaji kazi; ama ni kiungo kimoja kimoja katika kitu au kiumbe kimoja; au ni vitu mbalimbali, vinaonekana kufanyika kwa akili nyingi na upatano wao ni wa hali ya juu sana.

Kwa lugha rahisi, binadamu anaona ulimwengu kuwa umefanyika kwa akili nyingi na upatano wao ni wa hali ya juu sana. Hali hiyo ya mtu ya kufikiri au ya kuona kuwa ulimwengu, yaani vitu vyote vilivyopo vinaonekana kuwa na kufanyika kwa akili nyingi na akijiangalia na yeye mwenyewe - asijuwe ni hali gani hiyo imesababisha vitu sio tu kuwa kwa akili lakini na kwa jinsi gani, anajitiisha na kutambua hali hiyo kwa kuiita "Mungu".

Tunapojiuliza kuna Mungu au hakuna Mungu, tunapaswa kimsingi kufahamu kuwa neno hilo (Mungu) tunaita uwepo wa hali ya akili ambao hauonekani lakini tumeufahamu au tumeujua kwa jinsi tunavyoona vitu vyote vya asili vilivyofanyika kwa akili nyingi na upatano wao ulivyo wa hali ya juu sana.

Hivyo basi, "Mungu", ni nini? Au Mungu maana yake ni nini? Mungu maana yake ni, Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili. Kumbe, tunaposema Mungu au tunaposema kuna Mungu, ni Neno tunaloita "Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili". Na maana hii inatokana na jinsi tunavyoona na kustaajabia vitu vya asili vilivyofanyika kwa akili nyingi na upatano wao ulivyo wa hali ya juu sana.

Tunasikia mara zote watu wakizungumza juu ya akili na kuhusu akili. Kwa hakika watu huzungumza kuhusu akili wakielezea mpangilio na miundo na ufanyaji kazi wa vitu na upatano wao jinsi ulivyo na unavyoeleweka, mkamilifu na wenye matokeo chanya.

Na tunasema akili kuelezea uwezo wa hali ya juu wa kujua, wa kufahamu, wa kuelewa, wa ujuzi, wa maarifa na wa kufanya vitu, yaani kutatua matatizo na kufanya mageuzo yenye maendeleo. Lakini hatahivyo akili ni nini? Je, akili ipo wapi? Je, akili inaonekana?

Akili ni kipawa kinachomwezesha mtu kufikiri kujifunza, kuwasiliana kuamua na kutatua matatizo. Kwa maneno mengine, akili ni ufahamu. Kwa kuchukua wanyama na hata mimea kama viumbe wenye ufahamu tunaweza kuelewa akili ya wanyama na mimea, akili ya binadamu, na tunaposema Mungu - Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili.

Kimsingi wanyama wote wana ubongo ambamo mna ufahamu yaani akili. Lakini hatahivyo, wote tunakubali kwamba ubongo wa binadamu una akili kuliko ubongo wa wanyama wengine.

Kwa hiyo hatuwezi kuhitimisha kuwa akili ni shughuli au kazi za ubongo kwa sababu ubongo wa wanyama wengine nao vile vile unafanya shughuli za ufahamu. Lakini hatahivyo, wanyama wameendelea kubaki katika mstali wa ulalo (horizontal) wanadamu wako katika msatali wa wima (vertical).

Na kwa kweli binadamu pia anaweza kutokuwa na akili. Akabaki tu na ufahamu wa kawaida kama wanyama. Akawa tu kama wanyama anatekeleza kile mwili unamuasilishia kupitia milango yake mitano ya fahamu.

Kimsingi, akili ni ile hali ya kuwa na ufahamu wa kina wa mambo jinsi yalivyo na elimu ya vitu, yaani maarifa kamilifu au ushahidi wao wa ndani, na hivyo akili ni tofauti na ufahamu unaotokana na unaotegemea mwili, yaa milango mitano ya fahamu, ambao huo hautupatii maarifa kamilifu ya kitu au vitu, ya jambo au mambo jinsi yalivyo na yanavyotakiwa kuwa. Lakini hatahivyo, kama bado tungali hapa duniani tunahitaji mwili (hali safi ya ndani na ya mwili), ili kuunganika na Mungu, yaani Uwepo wa Hali ya Juu Wenye.

Unaweza kujiuliza au kufikiri ni nini kinakufanya uone au usema kitu hiki au jambo hili au hali fulani ni ya kiakili au imefanyika kwa akili; au jambo hili haliingii akilini? Unaposema kwa mfano, kitu hiki au jambo hili haliingii akilini unakuwa unajaribu kueleza nini?

Pengine wewe mwenyewe unaweza usijue jinsi mwili wako ulivyofanyika na unavyofanya kazi, labda ni vigumu sana. Lakini fikiria kwa mfano, kama umewahi kuona mitambo mbalimbali iwe ni ya viwandani au hospitalini ilivyotengenezwa na inavyofanya kazi, ni hali gani hiyo, na unaweza kuielezeaje?

Iwe ni mashine rahisi mpaka tata. Vivyo hivyo kuanzia na viumbe vidogo kabisa mpaka vikubwa kabisa vinaeleza hali ambayo mtu anaona na anaiita akili. Ingawa hakuna aliyeona akili ila ubongo ambao ni mahali pa ufahamu lakini hatahivyo, tunakubali kuwa vitu vyote vilivyopo vinaonekana kuwa na kufanyika kwa akili nyingi na upatano wao ni wa hali ya juu.

Kwa hiyo kama hivi ndivyo binadamu anaona ulimwengu, yaani vitu vyote vilivyopo vinaonekana kuwa na vimefanyika kwa akili, na sayansi haikatai hilo la vitu vya asili kuonekana kufanyika kwa akili nyingi na upatano wao kuwa wa hali ya juu isipokuwa inatafuta hali hiyo, na kwa jinsi gani.

Basi wazo kwamba kuna Mungu (idea that there is God is absolutely true), ni la kweli na hakika kwa sababu ambazo ni wazi na bayana. Kwanza vitu vya asili vilivyofanyika kwa akili nyingi na upatano wao kuwa wa hali ya juu. Na Pili mtu alivyo bora angalau katika viumbe wanaoonekana. Ubora huo ndio unaoelezwa katika biblia ikimtaja mtu kuwa "amefanyika kwa mfano na sura ya Mungu."

"Mfano na sura ya Mungu", mwandishi wa simulizi hilo la kweli za akili anamaanisha kuwa mtu amefanyizwa kwa mwili na roho - anayo hali ya akili hivi kwamba anaweza kuunganika na Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili, yaani Mungu.

Dini inafundisha kuwa Mungu ndiye amesababisha uhai na ulimwengu kuwepo na kwamba Yeye ndiye tokeo la uhai na ulimwengu na ulimwengu unatawaliwa na uwepo Wake. Sayinsi inasema mianzo ya vitu vilivyopo: ulimwengu, umesababisha na mlipuko mkubwa uliotokea zamani. Nadharia hii ambayo ni msingi mkuu wa nadharia zote za sayansi na ambayo inakubalika na wanasayansi wengi jinsi vitu vilivyotokea inafundisha kuwa vitu vilitokana na nishati au nguvu (energy).

Kwa sababu sayansi inashughulikia jinsi vitu vilivyopo vilitokea, katika muktadha huo imetusaidia sio tu kuelewa ulimwengu, lakini pia kumjua Mungu. Na hivyo kwa sababu inashughulika na vitu vinavyoonekana na vinavyoweza kupimika, sayansi haitufundishi kwamba nishati hiyo ambayo imesababisha vitu kutokea ni kama nishati tunayoitumia kwa mitambo au inayopatikana kwa vyakula, jua nakadhalika. Lakini (Sayansi) inatufundisha kwamba nishati hiyo ni zaidi ya hali tunayoweza kuielezea kama mlipuko au kama nishati inayoupa mwili nguvu, au inayowezesha mitambo kufanya kazi au jua kustawisha na kuwezesha uhai wa viumbe duniani, ni Nishati Yenye Ufahamu wa Hali ya Juu wa Akili.

Kitabu cha Mwanzo kinasema kuwa Mungu aliumba ulimwengu pasipo kutumia kitu chochote. Simulizi hilo linachoeleza ni kuwa ulimwengu uliumbwa au ulifanyizwa kwa kutumia akili. Na hii ni sayansi iliyowazi kwamba vitu vyote vilivyopo vinaonekana na vimefanyika kwa akili.

Kwa jinsi ufahamu wetu ulivyo na unavyotokana na kujifunza au kusoma au kufuatilia vitu vilivyopo kwa karibu yaani maarifa yetu yanayotuwezesha kuelewa na hatimaye kupima ulimwengu, haiwezekani kukataa au hata kukana kwamba ulimwengu yaani vitu vyote vilivyopo havionekani kuwa na kufanyika kwa akili nyingi na upatano wao ni wa hali ya juu sana.

Labda kama kutakuja utaratibu mwingine, yaani elimu au ufahamu au uelewa mwingine, ambao utaeleza kwa namna nyingine isiyo hii tunayoiona au tulionao kwamba, ulimwengu kuonekana na kufanyika kwa akili nyingi na upatano wao kuwa wa hali ya juu, unaashiria Uwepo wa Hali ya Juu Wenye Akili tunaouita Mungu.
Kwahyo Mungu maana yake ni uwepo wa hali ya juu wenye akili?
 
Nimesha kwambia hapo kwamba binadamu sio mnyama ila ana baadhi ya sifa za wanyama hata hiyo baiolojia ina eleza hivyo.

Kusema kwamba binadamu ni mnyama kwa kulinganisha sifa chache tunazo fanana na wanyama, Ni sawa na kusema wanyama ni binadamu kwa vile binadamu wanasifa za wanyama.
Nadhani tatizo ni uelewa.

Binadamu ana mwili na wanyama wengine vilevile wana mwili. Binadamu ana milango mitano ya fahamu na wanyama wengine vilevile wana milango mitano ya fahamu.

Ubora wa binadamu sio kwamba si mnyama au hana sifa zinazofanana na wanyama wengine, bali ubora wa binadamu ni ubongo wake kuwa na akili kuliko ubongo wa wanyama wengine.

Wacha nifafanue kwa kukuuliza hivi:

"Kwa nini hakuna kiumbe mwingine yeyote anayefanya uchunguzi kwenye sayari nyingine, kuzalisha chanjo za kuokoa maisha, kutunga mashairi nakadhalika, ila binadamu peke yake?

Kimsingi swali hilo halijaribu kusema wanyama wasio binadamu hawana akili. Kwa hakika wanayo. Hatahivyo akili -utambuzi au ufahamu wa wanyama wengine, ni utambuzi au ufahamu unaotokana na unaotegemea milango ya fahamu.

Neno akili tofauti na ufahamu unaotokana na unaotegemea milango ya fahamu, ni hali inayomwezesha mtu kuwa na maarifa kamilifu ya kitu au vitu, ya jambo au mambo (ushahidi wao wa ndani) jinsi yalivyo na yanavyotakiwa.
 
Nadhani tatizo ni uelewa.

Binadamu ana mwili na wanyama wengine vilevile wana mwili. Binadamu ana milango mitano ya fahamu na wanyama wengine vilevile wana milango mitano ya fahamu.

Ubora wa binadamu sio kwamba si mnyama au hana sifa zinazofanana na wanyama wengine, bali ubora wa binadamu ni ubongo wake kuwa na akili kuliko ubongo wa wanyama wengine.

Wacha nifafanue kwa kukuuliza hivi:

"Kwa nini hakuna kiumbe mwingine yeyote anayefanya uchunguzi kwenye sayari nyingine, kuzalisha chanjo za kuokoa maisha, kutunga mashairi nakadhalika, ila binadamu peke yake?

Kimsingi swali hilo halijaribu kusema wanyama wasio binadamu hawana akili. Kwa hakika wanayo. Hatahivyo akili -utambuzi au ufahamu wa wanyama wengine, ni utambuzi au ufahamu unaotokana na unaotegemea milango ya fahamu.

Neno akili tofauti na ufahamu unaotokana na unaotegemea milango ya fahamu, ni hali inayomwezesha mtu kuwa na maarifa kamilifu ya kitu au vitu, ya jambo au mambo (ushahidi wao wa ndani) jinsi yalivyo na yanavyotakiwa.
Pamoja na vyote ulivyo andika hapa lakini binadamu sio mnyama tunashea sifa tu na wanyama.

Na hiyo haitufanyi tuwe wanyama, bado tunabaki binadamu.

Uki elewa hili, utaacha kumlinganisha binadamu na mnyama kwenye kila kitu.
 
Kwa lugha nyingine na rahisi, akili imefanyika na nini? Hili ndilo swali lako.

Ni jambo ambalo sayansi inachunguza na kutafiti. Hadi sasa hakuna anayefahamu si tu hiyo hali au hiyo nishati au hiyo akili ikoje au inafananaje, bali pia ilifanyika au haikufanyika? Na kama ilifanyika imefanyika na nini?

On the other hand, it's like to ask: What is thoughts is made up of? Yaani mawazo au fikira yakoje na yamefanyika na nini
Hakika, akili wazo lenye akili ndio tunachotafuta na ndicho sie wenyewe tulicho.
Mkana wazo la Mungu mara nyingi kama sio zote hukana pia yeye kuwepo. Hukana kila kitu, atakana uhakika, atakana muda, atakana akili, atakana upendo. Ni watu wakumbatiao na kupendelea kutokuwepo kiasi kwamba mwisho wakiyapata mauti 'wanafurahia' kwerikweri. Maana ndicho walichokipigania maisha yao yote.

Mada moja inayojitambua sana broh.
 
Nguvu/Akili/ Mungu, Vyote hivi havipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika vipo kwa vile ni dhana za kufikirika tu zisizo katika uhalisia.
Hahahaaaaah! 😆. Seee! Nyie jamaa mnaamini sana katika kutokuwepo (kifo) na ndicho mnakipigania siku zote.

Huwa inaniacha na maswali hivi ni kwa namna gani mtu anakuwa na utayari na utamani wa kifo kwa kiwango hicho? Inashangaza sana.

Ndiyo maana wanadamu tunaaswa kuwa kamwe tusijidhanie kujua kile mtu mwingine anataka. Tutabashiri kitu kingine kumbe yeye anataka kitu kingine kabisa kinyume na hicho.

Na ndio maana Mungu akasema sitawachagulia mimi, basi ninaweka mbele yenu UZIMA na MAUTI....... Mifano ya uzima na mauti kwenye miili yetu ya nyama ni uhai na kifo....... Je? haitakishangaza mtu kuchagua kifo hapa duniani? Sasa ndugu ndio unafanya hicho katika roho, kuchagua mauti (KUTOKUWEPO)🤯🤯🤯.
 
Hahahaaaaah! 😆. Seee! Nyie jamaa mnaamini sana katika kutokuwepo (kifo) na ndicho mnakipigania siku zote.

Huwa inaniacha na maswali hivi ni kwa namna gani mtu anakuwa na utayari na utamani wa kifo kwa kiwango hicho? Inashangaza sana.

Ndiyo maana wanadamu tunaaswa kuwa kamwe tusijidhanie kujua kile mtu mwingine anataka. Tutabashiri kitu kingine kumbe yeye anataka kitu kingine kabisa kinyume na hicho.

Na ndio maana Mungu akasema sitawachagulia mimi, basi ninaweka mbele yenu UZIMA na MAUTI....... Mifano ya uzima na mauti kwenye miili yetu ya nyama ni uhai na kifo....... Je? haitakishangaza mtu kuchagua kifo hapa duniani? Sasa ndugu ndio unafanya hicho katika roho, kuchagua mauti (KUTOKUWEPO)🤯🤯🤯.
Huyo Mungu alisema wapi?

Mungu huyo mnahangaika sana kumwelezea na kumuongelea kwa vile Hayupo kujiongelea mwenyewe.
 
Pamoja na vyote ulivyo andika hapa lakini binadamu sio mnyama tunashea sifa tu na wanyama.

Na hiyo haitufanyi tuwe wanyama, bado tunabaki binadamu.

Uki elewa hili, utaacha kumlinganisha binadamu na mnyama kwenye kila kitu.
Hicho kinachomfanya binadamu (mtu) kuwa wa kipekee kati ya wanyama wengine (akili) ndio wewe unakana.

Kwa maneno mengine, wewe mwenyewe unajikana huna ufahamu. Pia hata ujuzi wa kuandika, au kuunda au kutunga maneno, unavyoandika hapa unaukana.
 
Huyo Mungu alisema wapi?

Mungu huyo mnahangaika sana kumwelezea na kumuongelea kwa vile Hayupo kujiongelea mwenyewe.
Kiukweli hata sasa Mungu anasema na wewe kupitia KWELI hizi unazosoma humu Jf

Aepm na mie na wengine wakitype ukweli basi ujue ni Mungu anasema kupitia wao. Unanakili??
 
Back
Top Bottom