Roboti Wa Nape
JF-Expert Member
- Nov 20, 2023
- 1,174
- 2,876
AiseeeeDini na UKIMWI are the two faces on the same coin.
Period
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
AiseeeeDini na UKIMWI are the two faces on the same coin.
Period
Kwahyo ukimkiri yesu afu ukawa unalawiti na kubaka watoto na kufanya unyanyasaji wa kingono Kwa wanawake na kuwadhulumu watu Mali zao na kuzini na wake za watu na Kila aina ya uchafu je utaenda mbinguni kwakuwa tu unamkir yesu 🤔 je Kuna dini inapeleka mtu mbinguni? Je kuwa tu muislamu au mkristo ni tiketi tosha ya kwenda mbinguni?🤔. Vitu vingine viko wazi tu Haina haja ya kukingiana vifua kutetea dini zetu zilizoletwa na wazungu na waarabu , kanuni kuu ya maisha ni kutomtendea binadamu mwenzako ubaya tu Yani vitu kama wizi ubakaji ulawiti dhuluma mauaji na machafu mengine yote ambayo sio ya kibinadamu yanawakwaza wengine. Kama Kuna dini inapeleka mtu mbinguni naomba kufahamu mana hata hizi dini zenyewe zinahimiza matendo maovu humpeleka mtu motoni . Anyway swala la Imani ni Kila mmoja ña nafsi yake wewe unatetea ukristo Kwa vile umezaliwa katka familia ya kikristo. Mfano nchi yetu dini zenye wafuasi wengi ni ukristo na uislam ila ukienda china asilimia kubwa ni Buddhist hii dini haiamini kabisa mambo ya kiroho ambayo hayaonekani mfano shetani ,MUNGU,uchawi na kadhalika pia kama ungezaliwa India ungejikuta upo ktk dini kuu za uko kma vile uhindu ,naagin na nyengne nyng tu .Duniani Kuna dini 4200 ambapo dini kuu zenye wafuasi wengi ni ukristo na uislam. Mi nna Imani kama hukumu IPO na MUNGU yupo basi hawezi kukukhukumu eti hukuwa mkristo au muislamu Bali utahukumiwa kulingana na matendo Yako full stop. Haiwezekani uwe mchungaji, padri au shehe afu unalawiti watoto na kutembea na wake za watu afu dini ikulinde ety Kwa kuwa ww n mkristo au muislamu basi utaenda peponi bila shaka yoyote Ile 😂 pia dini ni mfumo tu wa maisha watu kujumuika pamoja kumtafuta MUNGU muumba mbingu na nchi mfano kwny biblia Kuna mstari umeandika dini ya kweli ni Ile ya kuwasaidia wenye shida yatima Kwa wajane. Pia kwny biblia Kuna sehem inasema amri KUU nawapa nayo ni mapendo mpendane ko MUNGU anawaasa mpendane na Wala sio muanze kujibizana eti dini ipi ni sahihi . Ushauri wangu ni Kila mmoja aheshimu dini ya mwenzake kama ww mkristo unatakiwa uiheshimu dini zingine vile vile waislamu pia.Mwisho ata serikali Ina himiza uhuru wa kuabudu Kwa Kila raia ana haki ya kuabudu dini yoyote Ile ili mradi asikiuke Sheria kanuni na taratibu za nchi ko hizi mambo sijui za kukojolea au kuchoma moto vitabu vya dini biblia na Quran sio jambo zuri kabisa kwa muumba wa mbingu na nchi ndomana akasema AMRI KUU nawapa nayo ni MAPENDO mpendane ninyi Kwa nini . Tuache kujifanya wafia dini wakati dini tumezikuta na tutaziacha siku ya mwisho utakuwa ww mwnyw hautakuwa na dini hautazikwa na hiyo dini Yako na kama hukumu utahukumiwa kulingana na matendo Yako.Dini zote kama hazimkiri Yesu, wote wataenda motoni.
Kuzimu yupo mungu wao, na huyo allahu ni mmoja wa miungu ya huko.
Mungu ni MMOJA na YESU ndilo JINA lake.
Amen
Kama unapenda majini na mapepo na unayatumia kupata utajiri haramuAnaandika Robert Heriel,
Mtibeli.
Kuna Mungu Muumba wa mbingu na nchi halafu kuna miungu. Mungu Mkuu ambaye hajawahi kuonekana na kamwe hatokuja kuonekana Daima milele, hawezi kufanya wala kuwaza huo upuuzi wa kuchoma watu, hilo haliwezekaniki!
Miungu hii inayoabudiwa ndio inaweza kufanya hivyo, lakini yule Mungu wa miungu huo muda hana, na hawezi kufanya hivyo.
Mungu Mkuu ni Upendo, na kamwe upendo haulazimishwi. Yaani, ati Mungu aliyekuumba akulazimishe umpende (umuabudu) wakati alikuwa na uwezo wa kukuumba automatic ukawa unampenda!
Kwanza umpende (umuabudu) ili yeye apate nini? Halafu usipompende ati akuchome, wewe kosa lako lipo hapo? Yaani moyo wako haumpendi Mungu aliyekuumba, unapenda jambo jingine nini kosa lako, iko wapi haki hapo?
Mungu mwenye Upendo na muweza wa yote, anataka mtu apende anachokipenda! Kwanza yeye ndio aliyekufanya uwe hivyo ulivyo, upende unayoyapenda, achana na yale unayoyatamani na kuyachukia.
Huwezi lazimisha kupendwa bhana, na kamwe Mungu hawezi kukulazimisha umpende. Kukulazimisha haibadilishi ukweli kuwa haumpendi. Kumbuka Mungu ni Haki na Kweli.
Mchongo ukoje? Ipo hivi;
Jinsi uonavyo Ulimwengu wa nje (huu unaoonekana) ndivyo katika Ulimwengu wa ndani usioonekana, Ulimwengu wa Nafsi.
Itazame Dunia, Dunia ni moja lakini inamazingira tofauti tofauti, kuna sehemu zenye baridi kali mpaka barafu, kuna sehemu za jangwa, kuna sehemu za hali ya hewa ya kati, kuna sehemu zenye mvua nyingi, na zipo zenye mvua za Waarabu.
Kuna milimani na mabondeni, sehemu zenye maziwa, mito na bahati, sehemu yenye misitu mine, nyasi na vichaka, sehemu yenye wanyama wa aina hii sehemu nyingine hakuna.
Sasa ni uchaguzi wa mtu kutumia kile akipendacho, ukitaka kuishi kwenye baridi ni wewe, Mungu hawezi kukulazimisha uishi sehemu isiyo ya baridi wakati wewe unapenda. Haipo hiyo. Ukitaka kula chakula au wanyama fulani ni wewe mwenyewe.
Ila elewa kuwa vipo vitu ni sumu na cool vitu sio sumu. Ni wewe mwenyewe unachagua ule sumu au usile. Nasema ni wewe mwenyewe, ni kutokana na upendo wako.
Kama unavyoishi hapa Duniani kulingana na umri wako, jinsia yako, kipato na hadhi yako, mtazamo wako ndivyo nafsi yako itakavyoishi baada ya mwili wako kuondoka.
Mfano huwezi ishi Masaki, Mikocheni, Upanga wakati kipato chako na daraja lako ni kuishi kwa walalahoi huko.
Kunguru na njiwa hawawezi kaa pamoja, wanasema ndege wafananao huruka pamoja. Nenda hata wodini huko mahospitalini utaona kabisa kuwa mgonjwa wa akili hawezi lazwa wodi ya wazazi au mgonjwa aliyemahututi hawezi lazwa wodi ya wagonjwa wa meno.
Maisha ni uchaguzi wa mtu mwenyewe. Mungu kamwe hana huo muda wa kukuamulia nini chakupenda. Kuku hawezi zaa bata, kila mmoja atakaa sehemu yake. Vivyohivyo hata ukifa roho yako itaenda mahali inapopapenda, na wala hautachomwa moto.
Kama unapenda uzinzi na kuchukua wake za watu na kuua watu basi nafsi yako itaishi katika Ulimwengu wa watu wa aina yako ili mchukuliane wake na waume zenu kwa jinsi mpendavyo, ili muone utamu wa kile mnachokipenda.
Sheria siku zote sio upendo, Sheria hizi za nchi zipo kwaajili ya kudhibiti matendo ha mwili na sio nafsi. Upendo upo kwenye nafsi ya mtu wakati sheria ipo katika mwili wa mtu. Mtu anapoua akahukumiwa jela kinachoadhibiwa ni mwili wake lakini nafsi yake haiadhibiwi.
Utalipwa sawasawa na matendo ya nafsi yako, Dhamiri na utapelekwa kwenye Ulimwengu unaofanana na nafsi yako. Hiyo ndio tafsiri ya moto wa Jehanum na sio kuchomwa kama wengi walivyotafsiri au wanavyojua.
Mungu Mkuu hukupa na anatoa kitu kulingana na mtu au kiumbe husika, Ulimwengu wa wapenda haki, wapenda dhulma, wenye upendo, wenye chuki, wasema uongo na wauaji, ulimwengu wa wasema kweli na watoa uzima.
Ni wewe tuu unachagua wapi unapenda na hayo ndio yatakuwa maisha yako mpaka Mungu Mkuu atakapoona imetosha. Ukitaka kubadili vitu upendavyo ni wewe, lakini mpaka Mungu atakapoona inatosha, uende katika Ulimwengu mwingine.
Ni kama hapa Duniani, vile unavyoishi ndivyo ulivyoamua kuishi au wazazi wako walivyotaka uishi (kumbuka ulikuwa katika mwili wa wazazi wako). Hakuna kulaumiana wala hakuna wakumlaumu. Hayo ndio maisha!
Acha nipumzike sasa,
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.