Mungu na Shetani: Nani kaua zaidi?

Mungu yupi unamzungumzia mkuu?
Maana Kuna Watu watajua unamzungumzia YESU
 
Kwani hiyo Mana waliomba Mungu awape au Mungu ndo akiamua kuwapa Aina hiyo chakula ?
Je unafikiri Mungu hakujua umuhimu wa hiyo Mana kulingana na mazingira waliokuwa nayo ?
Waliomba chakula, wakapewa mama. Wamekula miaka na miaka..wamechoka,.wakataka kitu cha tofauti..Mungu akawaua kwa kutaka kitu tofauti na mana.
Wewe unaona ni sahihi?
 
Mungu na shetani wote hawapo. Hawa ni wahusika tu katika hadithi ya kutungwa na watu.

Ila, kama tunalinganisha wahusika katika hiyo hadithi, kama tunachambua riwaya, Mungu kaua zaidi.

Hutakiwi kumlinganisha mtu aliyeumba kifo, aliyekiruhusu kiwepo, na mwingine anayeua tu.

Huyo Mungu aliyeumba kifo, aliyekiruhusu kiwepo, siku zote atakuwa ameua zaidi.

Kwa sababu anahusika katika kila kifo, yeye ndiye chanzo cha vifo vyote, asingeruhusu kifo kiwepo, kungekuwa hakuna kifo. Hakuna ambaye angeweza kuua.

Vhagar
 
Tunalinganisha katika muktadha wa hadithi tu.

Japo tuna mchanganyiko.
Wengine tunachanganua hadithi na characters wake, ila wapo wengine wanatetea imani zao.
 
Kama kifo Ni adhabu,
Kwanini watoto wachanga wanafariki?
Wametenda kosa gani mpk wauwawe?
Wamekaidi maagizo gani mpk awaue?

Kama hawana kosa, Basi uyo Mungu wako Ni GAIDI.

Yaani TERRORIST
 
Tunalinganisha katika muktadha wa hadithi tu.

Japo tuna mchanganyiko.
Wengine tunachanganua hadithi na characters wake, ila wapo wengine wanatetea imani zao.
Imani wanaruhusiwa kuamini, ni haki yao ya kikatiba na kibinadamu.

Ila, wakianza kuitetea kama ukweli inabidi tuende kwenye uhakiki wa fact.
 
Umewahi kusoma philosophy of religion, formally or informally, na kukutana na kitu kinaitwa "the problem of evil" au "Epicurean Paradox" ?
 
Kama kifo Ni adhabu,
Kwanini watoto wachanga wanafariki?
Wametenda kosa gani mpk wauwawe?
Wamekaidi maagizo gani mpk awaue?

Kama hawana kosa, Basi uyo Mungu wako Ni GAIDI.

Yaani TERRORIST
Kifo ni chaguo na matokeo ya Adam na uzao wake wote aliyachagua kwenye bustani ya Eden
Kwa hiyo Kama mtoto mdogo ni uzao wa Adam hayo ndo maisha aliyochagua baba yao haijalishi umri
 
Umewahi kusoma philosophy of religion, formally or informally, na kukutana na kitu kinaitwa "the problem of evil" au "Epicurean Paradox" ?
Wewe ambae huamini hata uwepo wa Mungu Sina haja kukuelewesha
 
Your totally confused and you will never understand nothing
 
Wewe ambae huamini hata uwepo wa Mungu Sina haja kukuelewesha
Unajuaje kwamba wewe ndiye utanielewesha mimi na si mimi ndiye nitakuelewesha wewe?

Huyo Mungu hata kuthibitisha yupo unaweza?
 
Your totally confused and you will never understand nothing
Wewe jifunze kuandika Kiingereza kwanza kabla ya kujishaua mengine.

"Your totally confused" ndiyo nini sasa?

Unaharibu lugha ya watu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…