Mungu sio mwema

Mungu sio mwema

Nina hoja ningependekeza kuileta mbele yenu wanajamvi..

Kama kichwa na habari kinavyojieleza "Mungu sio mwema"
Je ni kwanini ninasema haya.

Zingatia hili, katika mafundisho yote ya kiimani tunafundishwa kumchukia shetani na mabaya yake yote ili tumpokee kristu, ni kweli Jamaa ni muovu, wewe sasa!! maana yupo ndani yako...hii chuki tunayoieneza dhidi ya shetani inatutengenezea nini sisi kama wanakondoo?!

Ukiangalia Kwa ndani zaidi chuki dhidi ya shetani, inaleta nini zaidi ya visasi, malalamiko na kukata tamaa ?! Sasa je, sisi kama wanadamu tunanufaika vipi na hii chuki tunayoieneza dhidi ya shetani, zaidi ya kutuumiza kihisia na kufifisha silka ya kupambania uhai.

Au Kuna faida ambayo mimi siioni?
Haya sasa tuangalie matendo yaliyopo kwenye wema wa Mungu, submission, compassion, respect and unity.....haya matendo tuliyatoa Kwa Mungu au Kwa kondoo?!

Je haya matendo mema yana faida gani kwetu?! Mbona ni kama hatutaki kutumia macho na kukaa hapa Duniani. Na pia ukienda mbali zaidi utaona ni Kwa namna gani yanaendelea kudidimiza silka ya kupambania uhai, hakuna zawadi nyingine inayotolewa na haya matendo ya kondoo zaidi ya utukufu(udhaifu).

Tukimuona shetani mbaya tunaumia na wema wa Mungu unatupa udhaifu, matokeo yake tunaishia kuwa sick and perishing, ndio maana Kila mkristu na muislamu unayekutana nae barabarani anaumwa either Kwa kufikiria au Kwa mawazo, na moyo pia unaumia.

Je Kuna haja gani ya kuendelea na hii kelele ya mema na mabaya kama Kila upande unaharibu, Kuna haja?!!!!!!!
Yesu alikuwa mchunga kondoo,
Next time try to be there- budha teachings, terrestrial head, beyond good or evil
Maandiko yanasema, mpende adui yako!
Shetani ni adui. Mpende!
 
Kusali na kuomba kwa Bakhressa au hata iwe Billgate hakuthibitishi wema wa huyo Mungu.

Kusali na kuomba ni vitu common sana kama kula na kunywa ambavyo anybody can do that regardless of his financial status.

So hii point yako haina mashiko.

😁😁😁😁

Unambii kitu wewe ikiwa nabarikiwa hivi siwezi kukaa Mbali na Mungu ✊🏿
 
😁😁😁😁

Unambii kitu wewe ikiwa nabarikiwa hivi siwezi kukaa Mbali na Mungu ✊🏿
Ndio sikwambii kitu.

Lakini unapoleta habari za uongo kuhusu huyo Mungu lazima nikwambie na tuzikosoe.

Otherwise, Ukitaka nisikwambie kitu baki na hizo habari za huyo Mungu wako moyoni mwako sio kuja kumuongelea hapa kwenye open forum.
 
1 yohana 5:19 tunatokana na mungu lakini ilimwengu wote upo chini ya nguvu za yule muovu,.
Kwahiyo tunapitia magumu sababu mtawala wetu ni muovu.
 
Kiukweli sijakuelewa kabisa na sitaki kuamini kama hueleweki maana umejitahidi kuandika kisomi sana lakini daaah sijaipata hoja yako.
 
Mbona wewe amekuachaaa mkuu uishii mpaka leo.....acha ufalaaaa
 
Someni biblia nyie muelewe neno la Mungu linafanyaje kazi
Acha siasa, Mungu ni aina ya uhalisia (intersubjective reality kama ilivyo nchi na pesa) au sijui mwenzangu una maana nyingine.
Tena Leo ndio Kuna Mungu ila ukimsoma homer kwenye the Iliad and Odyssey utagundua ilikuwepo miungu, na kabla ya hapo ilikuwepo Imani Kwa wanyama(Eva na nyoka)

Goodbye fella
 
Back
Top Bottom