Mungu wa kweli hahitaji haya tunayoaminishwa

Hizo amri za Mungu tunazopaswa kuzishika tutazipata wapi boss?

Nenda hata kwa wasiojua ukristo au Uislam uniambie wao wanaishije. Amri za Mungu ni amri za asili
 
Haloooo,!!!, Nyoka mweusi, vipi??, unashindwaje kuelewa hekima ya zaka??, unapotoa sadaka na ikatumika katika njia ya Mungu kwa namna yoyote, mfano kumlipa mshahara kiongozi wa dini au kumpatia mwenye shida hiyo ni sawa na kumpa sadaka Mungu, kwa maneno mengine hao watu ndio njia ya Mungu kupokea sadaka.

Au wewe ulitaka umuone Mungu mwenyewe "physically" na umpatie mkononi??!!, hilo halitawezekana.
 
Dini zina kila sababu ya kutimiza matakwa ya wanadamu

Hewezi kushindwa kujua kuwa ni kazi za njemba fulani wachache yenye matokeo chanya

Ni kama vile elimu, siasa na michezo.
 
Yameandwika wapi hayo?
 
Joka ni kiumbe wa Mungu kama ulivyo wewe, mbuzi, paka na ngedere. Acha kukariri maisha Mkuu. Kila kiumbe kimheshimu kiumbe mwenzake

Kama ni hivyo kila kiumbe kimuheshimu mwenzake, kwanini wewe unachinja (unaua), kuku, bata, mbuzi, samaki, ng'ombe nk halafu unapika nyama zao na unawala "heshima" iko wapi hapo, mbona wao hawakuchinji.
 
Mkuu kila kitu ni kazi ya Mungu. Kufundisha ni kazi ya Mungu, kulima ni kazi ya Mungu, kutibu wa gonjwa ni kazi ya Mungu, kuendesha watu ni kazi ya Mungu. Kuhudumia watu, au kuutengeza ulimwengu zote ni kazi za Mungu. Unachoshindwa kuelewa ni kitu kimoja ambacho ndicho viongozi wengi hukitumia. Huujui ukweli wa maisha.

Watu waache kumsingizia Mungu anashida ya mambo ya kibinadamu. Kwani walishindwa kutafuta neno jingine. Mbona huko mashuleni watu wakiambiwa watoe hela za waalimu na kujenga mashule wanafanya tuu bila tabu.
 
Kama ni hivyo kila kiumbe kimuheshimu mwenzake, kwanini wewe unachinja (unaua), kuku, bata, mbuzi, samaki, ng'ombe nk halafu unapika nyama zao na unawala "heshima" iko wapi hapo, mbona wao hawakuchinji.

Huo ni utaratibu kama ulivyowekwa. Na kumbuka nimetolea mfano. Mkuu nitakupa elimu zaidi maana naona kuna mambo huyaelewi
 
Nenda hata kwa wasiojua ukristo au Uislam uniambie wao wanaishije. Amri za Mungu ni amri za asili
Kwani kabla ya Abraham/ibrahimu na kizazi chake kuwepo watu waliishi vipi..!?

Anaweza kujibu hilo.? mpaka jambo la amri liwe habari kuu..!
 
Huo ni utaratibu kama ulivyowekwa. Na kumbuka nimetolea mfano. Mkuu nitakupa elimu zaidi maana naona kuna mambo huyaelewi

Sielewi nini hapo, kwani unapochinja hao wanyama wao wanapenda kuchinjwa??!!😁😁 na mbaya zaidi huwa wanapiga kelele kwa uchungu lakini binadamu bila huruma anawapiga kisu, na anakula nyama zao utasikia " loo, nyama ya huyu kuku imenona kweli kweli" lakini kasahau kwamba kabla ya kuchinja alikuwa ni kiumbe mwenye roho kama yeye.😁😁😁
 
Kama ni hivyo kila kiumbe kimuheshimu mwenzake, kwanini wewe unachinja (unaua), kuku, bata, mbuzi, samaki, ng'ombe nk halafu unapika nyama zao na unawala "heshima" iko wapi hapo, mbona wao hawakuchinji.
Na ndio maana tumeamua kuwa vegeterian kwa kuwa mahindi maharage na Matunda yapo

vikikosekana sio samaki tu hata simba ni supu nzuri tu
 
Na ndio maana tumeamua kuwa vegeterian kwa kuwa mahindi maharage na Matunda yapo

vikikosekana sio samaki tu hata simba ni supu nzuri tu

Wewe nawe vipi???!, mbona unachekesha, kwani umeambiwa na nani kwamba Maharage, Mahindi, na matunda au mimea haina UHAI??!,

Huwezi kula mchicha hadi uuchume kutoka shambani kabla hujauchuma unakuwa ni KIUMBE HAI. soma Biology mkuu.
 
Labda hujaeleweka unakazia nini

kwahivyo hutaki chenye uhai kiguswe..!?
 
Labda hujaeleweka unakazia nini

kwahivyo hutaki chenye uhai kiguswe..!?

Mimi nakula kila kifaacho kuliwa mimi sio vegetarian, na wewe nakushauri ule nyama pia achana na vegetarianism.
 
Mimi nakula kila kifaacho kuliwa mimi sio vegetarian, na wewe nakushauri ule nyama pia achana na vegetarianism.
Wewe una pepo sio bure inaelekea hata kitabu chako cha dini yako husomi

Nanalolifanya mimi hata mungu wako analilidhia kwa kuwa anajua ndio asili ya mwanadamu
 
Mungu yupo Mkuu. Ila wajanja ndio wanamfanya asiwepo kwa kumshushia heshima na kumfanya aonekane Mungu mwenye shida, Mungu asiye na huruma ilhali anahuruma.
Mkuu ukweli wa mambo Mungu ana sifa zote ANAANGAMIZA na KUPONYA , hili lazima mlikubali ndio ukweli
 
Wewe una pepo sio bure inaelekea hata kitabu chako cha dini yako husomi

Nanalolifanya mimi hata mungu wako analilidhia kwa kuwa anajua ndio asili ya mwanadamu

Vipi mkuu ManchoG, mbona umegeuka mbogo!!, umesema wewe ni vegetarian kwa sababu unaona "huruma" kutoa roho za wanyama na kula nyama zao kinyume chake huwa unakula maharage, mahindi na matunda, mimi nikakuambia hata hivyo navyo vinao UHAI yakupsa uwe na "huruma" kwao, ukataka kujua kiliwe kitu gani!!, mimi nikakuambia nakula chochote kinachofaa kuliwa kasoro kiti moto. Halafu nikakuusia uachane na "vegetarianism". Sasa mkuu nimekosea wapi hadi useme nina pepo!!??. Likemee basi 😁😁😁
 
Sasa kama umeamua kula vyote kwanini iwe kasoro kitimoto..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…