Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 24,831
- 45,154
Kwa miaka mingi kumekuwa na jitihada za kuhadaa umma kwamba watu wanaotukana serikali na viongozi ni Wapinzani.
Ukifatilia kwa umakini utaelewa kuwa wapinzani kazi yao imekuwa ni kukosoa, kushauri, kupendekeza na inapobidi kutekeleza na kutoa majibu ya Changa moto mbali mbali zinazoikabili Nchi yetu.
Lakini baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM na serikali wamekuwa wakitaka kudanganya umma kwamba wapinzani ndio wabaya na wanapinga kila kitu pale wanaposhindwa kujibu hoja zao.
Mh Tundu Lissu amekuwa Target in the list licha ya Mwanasiasa huyu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa na aliyekuwa Rais wa Tanganyika Law Society kujikita kwenye mambo mtambuka, magumu na mazito yanayohitaji fikra pevu. Wapinzani wake wakimtuhumu kuwa anatukana serikali.
Sasa hatimaye kama waswahili wanavyosema Muda ni Mwalimu, sasa muda umeongea.
Wamegundua kuwa Tundu Lissu si mbabaishaji bali wenyewe kwa wenyewe wanageukana.
Hoja nyingine ni kuwa viongozi badala ya kujikita na kuweka nguvu nyingi kupambana na mambo ambayo sisi wananchi tunayaita UDAKU ni bora kujikita kuwatafuta watu wanaoiba mali na fedha za serikali, wanaopora maliasili za Taifa na kutumia ofisi za umma kwa masalahi binafsi.
Maswala ya upotevu wa fedha nyingi za Taifa ndani ya chama na serikali wameyafumbia macho na hatujajawahi kuona kiongozi yeyote wa juu wa chama au serikali akitishia kuwataja Mafisadi na wanyonyaji hawa.
Sasa leo kuwataja watukanaji wa mitandaoni ina tija gani kwa Wananchi wanaohangaika na changamoto mbali mbali kama kukosekana kwa misingi ya haki na utawala bora, Njaa, kupanda bei za bidhaa, mafuta kuadimika, umeme wa kusuasua na ubovu wa miundombinu ya Barabara na majitaka?
Mungu wa Tundu Lissu ni Mungu aliye hai. Na Mwenye nguvu.