Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Uko sahihi...tajiri namba Moja duniani mfalme Suleiman alibarikiwa na Mungu...yeye ndo tajiri wa kwanza na WA mwisho kutokea duniani.... biblia inasema hatakuja kutokea tajiri kama yeye .kuna


Nimeelezea hapo juu mkuu
Nassupport
Luka 10:18 "Akawaambia, nilimwona shetani,akianguka kutoka mbinguni kama umeme"
 
Alichoeleza Mkuu hapa ni real kabisa wameelezea pia kitabu cha isaya 14:9-23
 
Swali langu ni vipi wanaojiita watumishi wa Mungu kwa vyeo vyao wawe wachungaji,mitume, manabii n.k wanaweza kufanya uzinzi na bado wanasimama madhabahuni? Ni Mungu yupi wanaemtumikia hawa maana bado huwa wanalitaja jina la Mungu na mwana wake(YESU) katika maombi yao.
 
Kuna hili andiko yoyote mwenye uelewa sio Nelson tu tusaidiane maarifa hapa
1 wakorintho 14:34 "wanawake na wanyamaze katika kanisa,maana hawana ruhusa kunena bali watii,kama vile inenavyo torati nayo" huwa linamaanisha nini?
vipi kuhusu wanawake walio wachungaji makanisani Wako kinyume nalo au sivyo ninavyowaza?
 
Daudi alikua mtakatifu sana na alimpenda sana Mungu lakini alianguka katika dhambi ya uzinzi alizini na mke wa uria mwanajeshi wake kisha akamuua uria Ili kuficha Siri maana tayari yule mwanamke alipata ujauzito.....Daudi alitambua makosa yake akaungama Ile dhambi Kwa kulia na kufunga na kuomboleza Mungu alimsamehe akamrejeza........ hujawai kuona mtu alikua mchawi gwiji la wachawi lakini Baadae akaachana navyo akatubu Mungu akamsamehe wengine majambazi ivyo......inshory hakuna mwanadamu asietenda dhambi hata watumishi pia hua wanatenda dhambi ...uzuri Mungu wetu ni mwenye Rehema ukiziungama dhambi zako anakusamehe haijalishi dhambi gani
 
1 yohana 1:9 "Tukiziungama dhambi zetu,Yeye ni mwaminifu na WA haki hata atuondolee dhambi zetu,na kutusafisha na udhalimu wote'"


Pia katika Mithali 28:13
"Afichaye dhambi zake hatafanikiwa,Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata Rehema"
 
Jana usiku nimemaliza maombi saa 8 nikaingia kulala nikaota nlikua kwenye ghorofa mara gafla watu wakaanza kutaharuki wakawa wanapiga kelele mara nikatoka ndani nikaenda nje kwenye cliff ya ghorofa mara nikaona mbwa mmoja akiwa anabweka anawakimbiza watu na Simba wawili wakubwa wakiwa wameachama midomo wanatoa ngurumo wanawakimbiza watu watu wakawa wanajirusha chini ya ghorofa kukwepa wale Simba lakini Simba wakawa wanawafata huko huko chini ya ghorofa walipojirusha ghorofa lilikua refu lakini watu walirusha chini kukwepa Simba ......nkawa nasema siwez kuruka chini Ili ghorofa ni refu sana nitavunjika na kuumia wale Simba wawili wakawa wananikaribia na yule mbwa nikawa niwafukuza Kwa mkono wakawa wanazid kunifata wakanisogelea kabisa wakawa wamesimama kama hatua 3 wananiangalia lakini hawanioni mara ghafla nikaona mlango nikakimbilia ule mlango nikatoka kwenye wale Simba mara nikakutana na rafiki yangu tukawa tumekumbatiana tunafarijiana na kutiana Moyo tumeokoka na wale Simba na kujirusha chini ghorofani.............
 
Tengeneza na Mungu wako na kua na imani nae.Walokole hulindwa kwa imani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…