Mungu wa walokole ana nguvu sana 1997- 2019! Kumbukumbu zangu

Kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 2019 nilikua kwenye research binafsi ya mambo yasiyoonekana kwa macho ya kawaida. Nimefanya mahojiano na watu wa fani hii,kuanzia watu wa kawaida mpaka viongozi wa fani hii katika nyanja mbalimbali.

Mambo yasiyoonekana kwa macho,watu wanaita""UCHAWI""na ni fani yenye kuchanganya kidogo sababu inajumuisha imani za dini za wanadamu na imani za dini zisizo za wanadamu. Pia inajumuisha watu ambao wanaitwa bin-adamu na inajumuisha watu wale wengine ambao hawana undugu na hawa watu wanaoitwa bin-adam.Nielezee kidogo hao watu wengine,nimewaita watu sababu wana maumbo kama binadamu ila vimo vyao vipo tofauti na wapo katika jamii mbili tofauti.

Kuna ile jamii ya wanaokaa angani ambapo bila ruhusa yao huwezi kuwafikia,na kuna ile jamii ambayo hata bila ruhusa yao unaweza kuwafikia na wanakaa chini ya bahari au mito au maziwa makubwa(Lakes).Ngoja nifafanue kidogo jamii za hawa watu.

Jamii ya watu wa angani inashuka sana duniani na sijui waga wanakuja kufanya nini ila mara nyingi wanajishugulisha na wale binadamu mnaowaita walokole,na ili uzungumze nao inategemea umekutana nao katika hali gani kwenye ulimwengu usio wazi kwa macho ya kawaida,kiasili sio waongeaji sana ila sura zao zinaakisi mwanga kwa namna ya tofauti na unaweza kujiuliza wanavaa mavazi gani, kwa mavazi wanavaa hizi nguo mnaita kanzu ila ni bwanga afu ndefu mpaka miguuni na ni nyeupe.

Jamii ile nyingine ya watu wasio na asili na binadamu ila wamefanana na binadamu kimuonekano lakini wana vimo vikubwa ni ile inayokaa chini ya bahari,maziwa(Lakes) na mito.Hii jamii wao ni wazungumzaji sana afu miili yao haiakisi mwanga na wanakuja sana duniani na unaweza kuwaona bila ridhaa yao kwa kufuata utaratibu wanaokupa wafuasi wao au wanajimu wa nyota mbao ni binadamu wa kawaida,na mavazi yao ni kanzu pia ila za rangi mbalimbali zaidi ya nyeupe.Na watu wanaojishugulisha nao sana ni wale watu ambao nyinyi binadamu mnawaita wanajimu na washirikina au wachawi ila inategemea ushirikina na uchawi wa wapi maana dunia ni kubwa kutoka bara moja mpaka lingine na ushirikina au uchawi unatofautiana.

Binadamu kuna vitu huwezi kuviona mpaka either uwe mshirika wa jamii mojawapo kati ya jamii hizo mbili nilizokutajia hapo juu.Lengo langu leo ni kuzungumzia mkuu wa jamii ile ya wale watu wa angani ambao wanapenda kushirikiana na walokole au watu wa kulia lia,maana huyo mkuu ana vitu vya tofauti kidogo ndio maana nikasema pale juu kua "Mungu wa walokole ana nguvu sana".

Katika utafiti wangu ndani ya ulimwengu usio,onekana inaonyesha kua walokole wanapendelewa sana na huyo mkuu wao,maana kuna vitu anawapa vya ziada wao hawavitumii sijui kwanini niligundua hilo huko mbele katika utafiti wangu.Nimemuita Mkuu au Mungu wa walokole sababu kila walokole wanapoanza kulialia""Kusali""wale watu wa jamii ya kuakisi mwanga wengine wana mabawa na wengine hawana wakitokea kwa mkuu wa walokole ama nilivyokuja kujua baadae huko huko angani wanawajia na wanawazunguka hawaondoki na lile eneo husika linakua na mwanga unaweza kupofusha macho (Ni kama mwanga wa jua au radi au shoti za umeme zile cheche) ila walokole waga hawawaoni nadhani waga wanalia(Kusali) kwa imani zaidi namaanisha meditation.

Nilisema hapo juu kua mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao ana nguvu sana maana wale walokole baada ya kulia kwa mkuu wao huwezi kuwasogelea katika hali ya nje ya ubinadamu au katika hali ya ushirika na jamii nyingine za kiroho zaidi ya mkuu wao na wale watu wa kuakisi mwanga.Kila mlokole anakua na yule mtu wa kuakisi mwanga na yule mtu haongei ila macho yake ni ishara tosha kua usimsogelee mlokole aliyenae.Cha ajabu wengi ya walokole hao katika hali ya ubinadamu wa kawaida hawana habari yoyote ile unawakuta sokoni au kwenye daladala au barabarani au ofisini au kwenye nyumba zao za ibada.

Sasa ikabidi nifanye uchunguzi juu ya huyo mkuu (Mungu) wa walokole,yupoje na ni nani, wale watu wa jamii ya kuakisi mwanga wanaishi nae vipi maana wana ushirika nae.Sababu ukitoka nje ya mwili kupitia(meditation) huwezi kuwasogelea hawa watu wa jamii ya kuakisi mwanga au hao walokole.Nikajikuta napata hamu ya kuchunguza mambo ya ulimwengu usionekana na hasa jamii za wale watu warefu wa angani na walokole hasa wale wa kulialia sisi binadamu tunaita kusali ila wao walokole wanaita kunena kwa lugha,na ni lugha ambayo inawafanya wawasiliane na wale watu warefu wa kuakisi mwanga.

Udadisi wangu ulijikita katika mambo makuu matano(5)
Mosi: Kwanini walokole wana uhusiano na wale watu wa kuakisi mwanga wanaotokea kule juu kusikofikika hata ukitoka nje ya mwili na kusafiri nje ya mzunguko wa sayari za kawaida kwa maelekezo ya wanajimu wa nyota?

Pili: Kwanini mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao ana uhusiano wa moja kwa moja na wale watu wa kuakisi mwanga na sio ile jamii ya chini ya bahari?

Tatu: Kwanini katika jamii za nje ya mwanadamu au mtu, hasa ile jamii ya watu wa kuakisi mwanga ina nguvu sana kuliko jamii za wale watu wanaokaa chini ya bahari na wasioakisi mwanga wa jua na mwezi?

Nne: Mkuu wa walokole kwanini yeye na wale watu wa kuakisi mwanga,hawana ukaribu na Mkuu wa wale watu wa jamii inayokaa baharini na chini ya maziwa na mito(Maana nayo ina mkuu wake) na hataki wafuasi wake wa dini yake wawe na ukaribu na walokole kwa namna yoyote ile?

Tano: Kwanini mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao pamoja na nguvu zoote ila hawapi utajiri wa kibinadamu hao walokole ila ukitoka nje ya mwili hawa walokole wana nguvu sana mpaka uñashindwa kuwaelezea labda uone kwa macho.Tofauti na mkuu wa ile jamii nyingine ambayo karibia robo ya wafuasi wake wana access ya kupata mali za dunia hii tunayoishi binadamu wote.

Basi nikajikuta naanza utafiti kufuatilia nguvu za mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao.Ni nani na yupoje na anaishi wapi..Utafiti wangu ukanipelekea kuja na kichwa cha habari hapo juu kua Mungu wa walokole ana nguvu sana maana nilishuhudia mengi kumuhusu huyu Mungu wa hawa watu wa kulialia mnawaitaga walokole.

Safari yangu ya utafiti ilinikutanisha na wazee wa kibantu,wanajimu,viongozi wa dini za wanadamu zinazoonekana na zisizoonekana na watu wa jamii zile za nje ya ulimwengu wa mwanadamu.

ITAENDELEA
safi sana mkuu
 
Walokole mmekuja na mbinu mpya kuwateka akili wajinga wajinga.

Mwisho wa simulizi utaweka namba watu wakufate kanisani kwako. Unasema uongo mchana kweupe na wajinga wenzio wanakusupport.

Hakuna watu wenye akili ndogo duniani kama walokole.
hahahaha, daah! Kwa mkasa wako wewe na vumilia,,niliamini ulibadilika na kuwa mtumishi kabisa, lakini kwa oni lako hili inaonesha we bado ni mshirikina wa kutupwa...
 
Inazungumzia,

Ili uwe miongoni Mwa Watu WA Mungu ,waliokubalika Mbele ZAKE uwe na haya,

Imani timilifu
Upendo WA Agape
Utakatifu kamilifu

Maombi Yako,yatawaliwe na nguvu ya Roho mtakatifu

Hivyo unatakiwa uwe navyo siku zote,maishani mwako,

Ila A-Z ya maelszo nimeweka kimtiririko wote,
Pia link hio

Main point ni nini Kwa Sisi wavivu kusoma
 
Summary hii apa,
Mada inahusu,

Watu waliojikabizi KUWA Mali ya Mungu ,Kwa NJIA ya umwamini ujumbe WA mwanae aliye mtuma duniani,

Ili uwe miongoni Mwa Watu WA Mungu ,waliokubalika Mbele ZAKE uwe na haya,

Mwamini mwanae aliyemtupa kwakuupokea ujumbe wake aliotumwa kuleta duniani ,Kwa kupokea moyoni Kwa NJIA ya kuamini ujumbe huo na kufuata,maisha yako yote,

Mada imegusia sana, Vitu hivi 3, vita wale maishani mwankila aliyejikabizi Kwa Mungu,

Vitu hivyo ambavyo muandishi nelson mtafiti akizungumzia ni,

1.Imani timilifu
2.Upendo WA Agape
3.Utakatifu kamilifu

Maombi Yako,yatawaliwe na nguvu ya Roho mtakatifu

Hivyo unatakiwa uwe navyo siku zote,maishani mwako,

Ila A-Z ya maelszo nimeweka kimtiririko wote,
Pia link hio

BAADA YA KUANZA HII SIMULIZI NILIPITIA MENGI,,,,,,UNAJUA MUNGU WA WALOKOLE HAITAKIWI WATU WA DUNIANI WAMJUE NA NDIO MAANA NIKAPITIA CHANGAMOTO MPAKA NIKAKAA PEMBENI KIDOGO JAMII FORUM....!!!LAKINI NAMSHUKURU HUYU MUNGU WA WALOKOLE AMBAE NI MKUU WA ANGA ZA JUU NA NI MUNGU MMILIKI ALINIAMBIA MANENO HAYA
MOSI: MIMI NI MUNGU NINAESAMEHE NA HAKUNA MUNGU KAMA MIMI UKITAKA KUTOA USHUHUDA WATU WANIFAHAMU USIOGOPE MATOKEO SABABU MIMI NI ROHO IWAKAYO MOTO NA WANAONIAMINI WANANIAMINI KATIKA ROHO NA UJASIRI WA IMANI WAOGA HAWANA NAFASI.
PILI: ANASEMA YEYE NI MUNGU MWENYE WIVU KWA WATU WAKE HASA WAMJUAO (HAPA NAMAANISHA WALOKOLE) NA ANAWALINDA KWA HIYO WASIOGOPE KUMTAJA.
KWA HIYO BAADA YA MANENO HAYA NA CHANGAMOTO ZA KIROHO ZILIZONIANDAMA TAKRIBANI MWAKA NIMERUDI TENA KUMZUNGUMZIA MUNGU WA WALOKOLE.YULE MUNGU MWENYE USHARIKA NA WALE WATU WAREFU WA NURU WENYE MABAWA NA AMBAE MTOTO WAKE WA KIPEKEE NDIE MFALME PEKEE WA ULIMWENGU WA KIMWILI NA ULIMWENGU WA KIROHO.
MKUBALI AU MKATAE ILA KWENYE ULIMWENGU WA KIROHO,,HUYU MTU MREFU MWENYE ALAMA YA ALFA NA OMEGA KIFUANI WALOKOLE WANAMUITA YESU AU IMANUELI AMBAE WALOKOLE WAKILIA ANATUMA WALE WATU WAREFU WENYE KUAKISI MWANGA WA JUA KUWALINDA,NDIE MUNGU WA KWELI NA ULIMWENGU WOTE WA KIROHO UNAJUA HIVYO.
MIMI BINAFSI WAKATI NAANDIKA KUHUSU MUNGU WA WALOKOLE NILIAMUA KUMSUJUDIA MAANA LEO NI MWAKA WA KENDA YUPO ANANITIZAMA TU KWA MACHO YA REHEMA..PAMOJA NA DHAMBI ZANGU BADO NINAISHI KWA REHEMA ZAKE ZA ULE USO WA KUNGAA NA KWA REHEMA ZA BABA YAKE AMBAE ANAWAKA KAMA JUA NA BILA KIBALI PENDEKEZI WALOKOLE WANAITA(UTAKATIFU) HUWEZI KUMTIZAMA AU KUMSOGELEA.
HAKUNA KITU KINATISHA KAMA KUMZUNGUMZA AU KUMUONGELEA MUNGU WA WALOKOLE ANATISHA MAANA ANA GRAVITY'S YA AJABU SANA INAKUTETEMESHA ROHO NA MWILI.NILIPOAMUA KUMZUNGUMZIA MUNGU WA WALOKOLE NILIPATA VITISHO VYA KIROHO ILA NIMERUDI TENA KUMZUNGUMZIA HUYU MUNGU MAANA NIMEMUONA KATIKA UKUU WAKE NA SI KWA MACHO YA NYAMA BALI MACHO YA KIROHO
MUNGU WA WALOKOLE YUPO HAI NA ANASHUKA DUNIANI KWA WASJIRIKA WAKE MDA WOTE NA KAMA AMEGAWANYIKA MAANA MAHALI POPOTE YUPO NA KAMA WALOKOLE MNGEFUNGULIWA MACHO YENU YA KIROHO BASI HAKUNA HATA MLOKOLE MMOJA AMBAE ANGEACHA USHARIKA NAE..YEYE NI MUNGU WA NURU NA VIUMBE VYOOOTE VYA KIROHO VINAMUABUDU NA ANA WASHIRIKA ZAKE WATU WAREFU WENYE KUAKISI MWANGA WA JUA WANAOWALINDA WALOKOLE NA MAPANGA YA MOTO POPOTE WAENDAKO.
KABLA SIJAENDELEA NAOMBA WALOKOLE POPOTE MLIPO MNIOMBEE ILI NIPATE KIBALI MBELE YA MUNGU WENU NIENDELEE KUWALETEA USHUUDA HUU KUMUHUSU YEYE AMBAE NI MUNGU MMLIKI WA ULIMWENGU WA KIROHO NDANI NA NJE YA MFUMO WA SAYARI ZA ULIMWENGU.
MUNGU WA WALOKOLE ANA NCHI YAKE SAYARI ZA MBALI AMBAYO NI WALOKOLE TU WENYE NEEMA YAKE MNAITA UTAKATIFU NDIO WATAFIKA HUKO.
 
Summary hii apa,
Mada inahusu,

Watu waliojikabizi KUWA Mali ya Mungu ,Kwa NJIA ya umwamini ujumbe WA mwanae aliye mtuma duniani,

Ili uwe miongoni Mwa Watu WA Mungu ,waliokubalika Mbele ZAKE uwe na haya,

Mwamini mwanae aliyemtupa kwakuupokea ujumbe wake aliotumwa kuleta duniani ,Kwa kupokea moyoni Kwa NJIA ya kuamini ujumbe huo na kufuata,maisha yako yote,

Mada imegusia sana, Vitu hivi 3, vita wale maishani mwankila aliyejikabizi Kwa Mungu,

Vitu hivyo ambavyo muandishi nelson mtafiti akizungumzia ni,

1.Imani timilifu
2.Upendo WA Agape
3.Utakatifu kamilifu

Maombi Yako,yatawaliwe na nguvu ya Roho mtakatifu

Hivyo unatakiwa uwe navyo siku zote,maishani mwako,

Ila A-Z ya maelszo nimeweka kimtiririko wote,
Pia link hio

Mkuu huu utafiti umenifanya kwa sasa nimsujudie Mungu wa walokole ambae katika ulimwengu wa kiroho ana gravity kubwa mno siwezi kuielezea na kile kitabu walokole wanaita biblia,sio kitabu kile kwa macho ya kiroho bali ni pumzi na maneno ya Mungu wa walokole na kina uhai wa pumzi za moto ndani yake
 
Kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 2019 nilikua kwenye research binafsi ya mambo yasiyoonekana kwa macho ya kawaida. Nimefanya mahojiano na watu wa fani hii,kuanzia watu wa kawaida mpaka viongozi wa fani hii katika nyanja mbalimbali.

Mambo yasiyoonekana kwa macho,watu wanaita""UCHAWI""na ni fani yenye kuchanganya kidogo sababu inajumuisha imani za dini za wanadamu na imani za dini zisizo za wanadamu. Pia inajumuisha watu ambao wanaitwa bin-adamu na inajumuisha watu wale wengine ambao hawana undugu na hawa watu wanaoitwa bin-adam.Nielezee kidogo hao watu wengine,nimewaita watu sababu wana maumbo kama binadamu ila vimo vyao vipo tofauti na wapo katika jamii mbili tofauti.

Kuna ile jamii ya wanaokaa angani ambapo bila ruhusa yao huwezi kuwafikia,na kuna ile jamii ambayo hata bila ruhusa yao unaweza kuwafikia na wanakaa chini ya bahari au mito au maziwa makubwa(Lakes).Ngoja nifafanue kidogo jamii za hawa watu.

Jamii ya watu wa angani inashuka sana duniani na sijui waga wanakuja kufanya nini ila mara nyingi wanajishugulisha na wale binadamu mnaowaita walokole,na ili uzungumze nao inategemea umekutana nao katika hali gani kwenye ulimwengu usio wazi kwa macho ya kawaida,kiasili sio waongeaji sana ila sura zao zinaakisi mwanga kwa namna ya tofauti na unaweza kujiuliza wanavaa mavazi gani, kwa mavazi wanavaa hizi nguo mnaita kanzu ila ni bwanga afu ndefu mpaka miguuni na ni nyeupe.

Jamii ile nyingine ya watu wasio na asili na binadamu ila wamefanana na binadamu kimuonekano lakini wana vimo vikubwa ni ile inayokaa chini ya bahari,maziwa(Lakes) na mito.Hii jamii wao ni wazungumzaji sana afu miili yao haiakisi mwanga na wanakuja sana duniani na unaweza kuwaona bila ridhaa yao kwa kufuata utaratibu wanaokupa wafuasi wao au wanajimu wa nyota mbao ni binadamu wa kawaida,na mavazi yao ni kanzu pia ila za rangi mbalimbali zaidi ya nyeupe.Na watu wanaojishugulisha nao sana ni wale watu ambao nyinyi binadamu mnawaita wanajimu na washirikina au wachawi ila inategemea ushirikina na uchawi wa wapi maana dunia ni kubwa kutoka bara moja mpaka lingine na ushirikina au uchawi unatofautiana.

Binadamu kuna vitu huwezi kuviona mpaka either uwe mshirika wa jamii mojawapo kati ya jamii hizo mbili nilizokutajia hapo juu.Lengo langu leo ni kuzungumzia mkuu wa jamii ile ya wale watu wa angani ambao wanapenda kushirikiana na walokole au watu wa kulia lia,maana huyo mkuu ana vitu vya tofauti kidogo ndio maana nikasema pale juu kua "Mungu wa walokole ana nguvu sana".

Katika utafiti wangu ndani ya ulimwengu usio,onekana inaonyesha kua walokole wanapendelewa sana na huyo mkuu wao,maana kuna vitu anawapa vya ziada wao hawavitumii sijui kwanini niligundua hilo huko mbele katika utafiti wangu.Nimemuita Mkuu au Mungu wa walokole sababu kila walokole wanapoanza kulialia""Kusali""wale watu wa jamii ya kuakisi mwanga wengine wana mabawa na wengine hawana wakitokea kwa mkuu wa walokole ama nilivyokuja kujua baadae huko huko angani wanawajia na wanawazunguka hawaondoki na lile eneo husika linakua na mwanga unaweza kupofusha macho (Ni kama mwanga wa jua au radi au shoti za umeme zile cheche) ila walokole waga hawawaoni nadhani waga wanalia(Kusali) kwa imani zaidi namaanisha meditation.

Nilisema hapo juu kua mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao ana nguvu sana maana wale walokole baada ya kulia kwa mkuu wao huwezi kuwasogelea katika hali ya nje ya ubinadamu au katika hali ya ushirika na jamii nyingine za kiroho zaidi ya mkuu wao na wale watu wa kuakisi mwanga.Kila mlokole anakua na yule mtu wa kuakisi mwanga na yule mtu haongei ila macho yake ni ishara tosha kua usimsogelee mlokole aliyenae.Cha ajabu wengi ya walokole hao katika hali ya ubinadamu wa kawaida hawana habari yoyote ile unawakuta sokoni au kwenye daladala au barabarani au ofisini au kwenye nyumba zao za ibada.

Sasa ikabidi nifanye uchunguzi juu ya huyo mkuu (Mungu) wa walokole,yupoje na ni nani, wale watu wa jamii ya kuakisi mwanga wanaishi nae vipi maana wana ushirika nae.Sababu ukitoka nje ya mwili kupitia(meditation) huwezi kuwasogelea hawa watu wa jamii ya kuakisi mwanga au hao walokole.Nikajikuta napata hamu ya kuchunguza mambo ya ulimwengu usionekana na hasa jamii za wale watu warefu wa angani na walokole hasa wale wa kulialia sisi binadamu tunaita kusali ila wao walokole wanaita kunena kwa lugha,na ni lugha ambayo inawafanya wawasiliane na wale watu warefu wa kuakisi mwanga.

Udadisi wangu ulijikita katika mambo makuu matano(5)
Mosi: Kwanini walokole wana uhusiano na wale watu wa kuakisi mwanga wanaotokea kule juu kusikofikika hata ukitoka nje ya mwili na kusafiri nje ya mzunguko wa sayari za kawaida kwa maelekezo ya wanajimu wa nyota?

Pili: Kwanini mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao ana uhusiano wa moja kwa moja na wale watu wa kuakisi mwanga na sio ile jamii ya chini ya bahari?

Tatu: Kwanini katika jamii za nje ya mwanadamu au mtu, hasa ile jamii ya watu wa kuakisi mwanga ina nguvu sana kuliko jamii za wale watu wanaokaa chini ya bahari na wasioakisi mwanga wa jua na mwezi?

Nne: Mkuu wa walokole kwanini yeye na wale watu wa kuakisi mwanga,hawana ukaribu na Mkuu wa wale watu wa jamii inayokaa baharini na chini ya maziwa na mito(Maana nayo ina mkuu wake) na hataki wafuasi wake wa dini yake wawe na ukaribu na walokole kwa namna yoyote ile?

Tano: Kwanini mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao pamoja na nguvu zoote ila hawapi utajiri wa kibinadamu hao walokole ila ukitoka nje ya mwili hawa walokole wana nguvu sana mpaka uñashindwa kuwaelezea labda uone kwa macho.Tofauti na mkuu wa ile jamii nyingine ambayo karibia robo ya wafuasi wake wana access ya kupata mali za dunia hii tunayoishi binadamu wote.

Basi nikajikuta naanza utafiti kufuatilia nguvu za mkuu wa walokole namaanisha Mungu wao.Ni nani na yupoje na anaishi wapi..Utafiti wangu ukanipelekea kuja na kichwa cha habari hapo juu kua Mungu wa walokole ana nguvu sana maana nilishuhudia mengi kumuhusu huyu Mungu wa hawa watu wa kulialia mnawaitaga walokole.

Safari yangu ya utafiti ilinikutanisha na wazee wa kibantu,wanajimu,viongozi wa dini za wanadamu zinazoonekana na zisizoonekana na watu wa jamii zile za nje ya ulimwengu wa mwanadamu.

ITAENDELEA
Kumbe kuna Mungu wengi, eeh? Wa walokole wa wasabato, wa waislamu nk? Hahahahaha......
 
Back
Top Bottom