Nikili tu ya kuwa Huu uzi umenifanya nikue kiimani
Maana umenikumbusha mambo mengi sana sana tangu nikiwa mtoto mpaka kijana.
Kuna wakati nilipokuwa nimetekwa kupelekwa mererani kutolewa kafara,
Kuna mambo ya ajabu niliona yakishuka angani kwa macho yangu, kuna siku nikipata muda nitaweka, wakati huo nikiwa mtoto wa miaka 8.
Sio tu hili, nilipishana na makundi ya wanyama hatari kama Nyati, majoka makubwa ambayo yalikuwa yanauwezo wa kunimeza kwa dakika 0, simba, chui, lkn hawakuweza kunidhuru, nilikuwa najiona nipo kwenye kundi la watu wenye moto mkali ambao pumzi zao zinawasukuma na kuwapumbaza wale wanyama. Rohoni nilikuwa nina amani kubwa mnoo japo kuwa nipo katikati ya hatari.
Kupitia andiko hili sasa nimejua mengi
Asante mwandishi[emoji91][emoji91][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]