wewe unasema siku hizi hakuna manabii, wakati Neno la Mungu linasema "na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri"
ndio nimekuuliza, unaueleweje mstari huo?
1Wakorintho 12:4 “Basi pana tofauti za KARAMA; bali Roho ni yeye yule.
5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.
6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.
8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa NENO LA HEKIMA; na mwingine NENO LA MAARIFA, apendavyo Roho yeye yule;
9 mwingine IMANI katika Roho yeye yule; na mwingine KARAMA ZA KUPONYA katika Roho yule mmoja;
10 na mwingine MATENDO YA MIUJIZA; na mwingine UNABII; na mwingine KUPAMBANUA ROHO; mwingine AINA ZA LUGHA; na mwingine TAFSIRI ZA LUGHA;
11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye”.
MDO 2:17-21
Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri. Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi. Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri. Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.
HITIMISHO
Inayofanya kazi ni ile ROHO MTAKATIFU ya Mungu aliyowavuvuia watu wake WAUME kwa WANAWAKE na si jinsia yao.Binadamu hutazama mambo kibinadamu ,yasiyowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu yanawezekana.Mtu yeyote awe ME au KE aliyejazwa ROHO wa Mungu,Roho ile ya Mungu itendayo kazi ndani yake inaweza kutenda kazi bila kujali jinsia yake,na moja ya kazi ni UNABII ,kwa maandiko haya mwanamke anaweza kuwa NABII.,walikuwepo ,wapo na wataendelea kuwepo manabii wa jinsia zote.