Mungu Yuko wapi?

Nimekuambia tayari.

You do not pay attention, you just want to preach your Bible and God.

Soma posts #489 - #493, halafu respond point by point.

Sitaki mahubiri, nataka majibu yenye mantiki.
Nitakapokuwa na Bible karibu, nitafanya hivyo. Maandiko ya Biblia hujibiwa kwa Maandiko ya Biblia.

Nitafanya hivyo baadaye kidogo.

Hata hivyo, ujue, whatever the case, "GOD LOVES YOU"
 
Nitakapokuwa na Bible karibu, nitafanya hivyo. Maandiko ya Biblia hujibiwa kwa Maandiko ya Biblia.

Nitafanya hivyo baadaye kidogo.

Hata hivyo, ujue, whatever the case, "GOD LOVES YOU"
You are still preaching.

First prove God exists, then we can talk about whether God loves me or not.

Hujathibitisha Mungu yupo usharukia ananipenda?
 
You are still preaching.

First prove God exists, then we can talk about whether God loves me or not.

Hujathibitisha Mungu yupo usharukia ananipenda?
Nithibitishe Yupo kwa manufaa ya nani?
 
Nithibitishe Yupo kwa manufaa ya nani?
Manufaa ya wote tunaofuatilia mjadala tujue kwamba yupo kweli ili tujue kwamba anaweza kunipenda.

Kwa sababu, kama hayupo, haiwezekani anipende.

Mungu ambaye hayupo atanipenda vipi?
 
MUNGU ni muumbaji, yuko hapo ulipo na anataka roho yako!!,,roho yako mikiwa safi anaisitiri,ikiwa chafu anaichoma kama takataka yoyote ile!!!
 
Manufaa ya wote tunaofuatilia mjadala tujue kwamba yupo ili tujue kwamba anaweza kunipenda.

Kwa sababu, kama hayupo, haiwezekani anipende.

Mungu ambaye hayupo atanipenda vipi?
Ni wewe na wenzako wachache ndiyo mnaofikiria huenda suala la uwepo wa Mungu ni dhana ya kufikirika tu. Lakini wengine wote wanaamini kuwa Mungu Yupo, na wengine wameenda hata mbali zaidi kwa kuelezea jinsi walivyotendewa na Mungu maishani mwao.

Labda kama unataka kumwamini Mungu ili na wewe uweze "kumwona", useme ili usaidike.

Wapo watu wengi wanaomjua Mungu na wapo tayari kumsaidia yeyote anayetaka kumjua Mungu kwa kumaanisha.

Unataka kusaidiwa katika eneo lipi hasa?
 
Kusema ni mimi na wenzangu wachache ndio tunaofikiria kuwa uwepo wa Mungu ni dhana ya kufikirika tu, na wengi wanaamini Mungu yupo kweli, hata kama ni kweli - which is debatable -si hoja ya msingi kimantiki.

Hii kimantiki ni logical fallacy, inaitwa "appeal to popularity".

Kwa msingi wako huo, kama Mungu yupo kweli, halafu watu wote wakakubali kwamba hayupo, Mungu atakuwa hayupo?

Unaweza kusoma zaidi hapa Appeal to Popularity

Nataka uthibitishe Mungu yupo ili uondoe mahubiri ya kiimani, hujathibitisha Mungu yupo.
 
NIMESOMA HILI BANDIKO huku nikiwa natetemeka na wadau wengi wamekuwa wak8mkashfu jaman punguzen mihemko twende mshikaji yy anataka kumuona MUNGU

Sssa hapa naomba tumsaidie na si kumkashifu tu

iko hv kwenye kuamin kitu kipo ni mawil moja ukione au upate evidence za kuaminika mfano wanasayansi wanasema dunia inazunguka rotation na revolution mmmh amazing rotate mmmmh kwann nikiruka juu sisogei mbele wakatoa evidences zao ambazo zina mashiko na mwisho watu wakaamin ni km ile issue ya dunia ni duara ilikuja kumalizwa na kufunga mjadala baada ya satelite kutoka nje ya dunia na kupiga picha dunia sasa hv ukianzisha hoja dunia ni flat unaonekana kilaza


TURUD KWENUE MADA mkuu mm nakuelewa sn tena sana unavhokitaka zipo evidence nying ambazo zinaonesha dunia and universe was created lkn km utataka kupata iman thabit nakushauri kasomee uchawi uchawi wa kisomi pitia uzi wangu
 
Hata kama watu woooote wasingeamini kuwa Mungu Yupo, bado angebaki wa kuaminiwa kwa sababu yeye Mwenyewe asingeacha kujiamini.

Ujue tu Mungu hana njaa ya kuaminiwa. Lakini ukimwamini ni kwa faida yako na ukiamua kutokumwamini ni kwa hasara yako.

Your belief that I am committing fallacy cannot alter the fact that God does exist.

The fact remains fact. You can't alter.

Uwepo wa MUNGU ni KWELI ISIYOPINGIKA.

By the way, wewe uko huko uliko na mimi niko huku niliko. Unaweza kunithibitishia kuwa mama yako au baba yako au mjomba... yupo?

Kumbuka sikufahamu kwa sura, hivyo na ndugu zako pia siwafahamu. Unaweza kunithibitishia kuwa ndugu zako wapo?
 
Kwa hiyo habari yako ya kusema Mungu yupo ndiyo maana watu wengi wanaamini Mungu ni pointless, siyo?
 
umejibu vyema sn kisa wengi wanaamin na sisi tuamin kisa sisi ni wachache basi hoja yetu haina mashiko we need the truth ukienda kanisan kila ukiuliza swali majibu wanatoa katika kitabu kilichochapishwa na binadamu na bado wakatulazimisha tuamin kile kitabu k8meandikwa na MUNGU

mm npo apa mpaka uzi uishe wachawi pia mje uku waganga mje
 
Sijakuekewa mkuu! Unamaanisha nini hasa?
Uliandika hivi.

"Ni wewe na wenzako wachache ndiyo mnaofikiria huenda suala la uwepo wa Mungu ni dhana ya kufikirika tu. Lakini wengine wote wanaamini kuwa Mungu Yupo, na wengine wameenda hata mbali zaidi kwa kuelezea jinsi walivyotendewa na Mungu maishani mwao."

Hoja ya watu wengi au wachache kumuamini Mungu katika mjadala wa kuangalia Mungu yupo au hayupo ni ya msingi au ni ya ujinga tu?

Ikiwa Mungu yupo, halafu wengi hawaamini yupo, wachache wanaamini yupo, je, hiyo idadi ya wengi wanaosema Mungu hayupo itamfanya awe hayupo?

Ikiwa Mungu hayupo, halafu wachache wanasema hayupo, wengi wanasema yupo, hao wengi wanaosema yupo watafanya Mungu awe yupo kweli kwa sababu wengi wameamini Mungu yupo?
 
Naam,

Kitabu kimoja nimehoji ukweli wake posts #489, #490, #491, #492 na #493.

Mpaka sasa hizo posts hakuna hata moja niliyoona imejibiwa.
 
Mkuu, nashukuru kwa ufafanuzi wako wa kisomi. Nimeelewa Sasa ulichomaanisha.

Ni hivi, suala la Mungu kuwepo hauamuliwi na utashi wa wanadamu. Watu wote wakikubali au kukataa, hakumwongezei wala kumpunguzia Mungu chochote. Hamtegemei mwanadamu. Mwanadamu ndiye anayemhitaji.

Mungu anaweza kuwepo pasipo mwanadamu, lakini mwanadamu hawezi kuwepo bila Mungu.

Hata kama watu wote wangedai kuwa Mungu hayupo, kusingemfanya asiwepo. Na watu wote wangeamini kuwa Yupo, kusjmgemwongezea Mungu chochote.

Wingi niliouzungumzia ni katika huu uzi tu. Wengi wa wanaofuatilia wanaamini wanaamini katika uwepo wa Mungu kuliko wanoupinga.

Na hata kama wote wangekubaliana nawe, japo isingewezekana, bado kusingemwathiri Mungu kwa namna yoyote ile.
 
Kwa hivyo habari nzima uliyoileta ya kusema tusioamini Mungu ni wachache, wengi sana wanaamini Mungu, ni upuuzi tu. Unakubali?
 
Naam,

Kitabu kimoja nimehoji ukweli wake posts #489, #490, #491, #492 na #493.

Mpaka sasa hizo posts hakuna hata moja niliyoona imejibiwa.
Kiongozi, usiwe na haraka! Utapata majibu ya maswali yako.

Hata kama wadau wengine hawatafanya hivyo, Mimi nitajitahidi kuyajibu maswali uliyouliza, lakini kwa kutumia Bible. By saa Sita Mchana huu, naamini nitakuwa na fursa ya kufanya hivyo.

Nitaketi na Bible na kukupatia majibu unayoyatafuta.

Kuwa mvumulivu mkuu. Si unajua mambo mazuri hayahitaji haraka?

Good things are coming soon!!!
 
Nyie pia mmesema Yesu atarudi maelfu ya miaka yamepita hajarudi.

Wewe ukiwa unajibu, jibu tu. Mimi sitaki ahadi za kujibu, nataka majibu.

Usije kunisubirisha kama watu wanavyomsubiri Yesu arudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…