Mungu Yupo: Majibu kwa Wasioamini

Mungu Yupo: Majibu kwa Wasioamini

Status
Not open for further replies.
Hapa ndipo na mimi naungana na Mtoa mada kuwa kwa mujibu wa
tamko la dini yenu linalodai "Mungu hayupo" na nyinyi kukiri ni kinyume na hivyo ni kuikana imani yenu.

Naungana naye kwa sababu kitendo cha kutilia mashaka hata kile ambacho unaeleza kuwa kuna uwezekano kikawa kweli (rejea...Na ukiijua kweli itakuwa juu ya wanadamu wote?) inaonyesha jinsi gani umepofushwa na Tamko la dini yenu.

Maana kama utajua kweli kuna sheria iliyojuu ya wanadamu wote ...mashaka mengine yatatoka wapi ? vinginevyo unieleze pia kuwa imani yenu haotambui uwepo wa Ukweli na Uongo.

Sitaki imani, nataka kujua.
 
Kiranga tunasubiri ufafanuzi wako kwa swali hili toka kwa Stefano Mtangoo -"Why should things be uniform in random universe where things just run themselves through chance?"
 
the book that u so trust has a lot of inconsistency y would a rational person trust it??? even from early chapters lots of ambiguities!! kwa mfano wakat cain amemuua ndugu yake anafukuzwa akawa anamlalamikia mungu kua uko anakoenda anaogopa watu watamuua? swali ni kwamba nani hao watu anaowaogopa? kulikua na town ingine apart from eden? watu hao walitoka wapi? and funny enough uko alikoenda akapata na mke!!!

Hii hapa chini naona ilikupita. Naomba ufungue thread juu ya hilo. Mada tunayoongelea hapa iko wazi na pwenti zangu ziko wazi.
Kama tatizo lako ni kuwa huielewi biblia au unadhani kuna vitu viko hivi au vile then hicho ni kitu kingine. maswal yako ni marahisi sana lakini sitayajibu kuweka focus kwnye mada husika.

Kwa mara nyingine hujajibu hoja zangu na hivyo ukweli unabaki kuwa Kukana kwenu Mungu ni dini na wala haina uhusiano na sayansi wala mantiki. Mkiri hivyo na mwende kifua mbele kuwa hii ni dini na sio kujificha nyuma ya sayansi na mantiki ambazo hazikubaliani na tamko lenu la imani kuwa "Hakuna Mungu"

a. Ufafanuzi
Kabla sijaweka pwenti zangu ningependa kuweka msingi wa tunachokijadili hapa na mipaka yake. Suala la Mungu ni pana sana na hata vitabu vyote havitoshi kujadili, kwa hiyo kwa nafasi fnyu kama forum, tunahitaji kuweka mipaka.

Kwanza ninaposema Mungu ninaongelea "Mungu kama anavyoelezwa ndani ya Biblia". Hapa hatutazungumzia (ktk mada hii) kuhusu Biblia, ila Mungu wa Biblia. Usiniulize kuhusu imani nyingine maana mimi nakubali Mungu wa Biblia na ninaweza kukujibu kuhusu Mungu kama inavyoeleza Biblia. Kwa habari ya imani nyingine, subiri wafungue uzi au fungua kuwauliza watakujibu vizuri tu (ninaamini hivyo).
 
Kwamba kutokuwepo Mungu ni imani kama Uwepo wa Mwenyezi Mungu.

Hujajieleza vizuri.

Kutokuwepo kwa mungu, kama hayupo kweli, hakuwezi kuwa imani tu.

Labda uweke maneno yako vizuri, maana mambo mengine ni magumu kuyaelezea kwa sababu yanataka discipline kubwa katika maelezo.

Halafu waamini hawajanijibu kuhusu "problem of evil" bado.

Kama mungu mjuzi wa yote, muweza yote na mwenye upendo mkuu kauumba ulimwengu huu.

Kwa nini ameuumba ukiwa na mabaya mengi sana kwa viumbe wake? Kwa nini kakubali ulimwengu uruhusu watoto kuzaliwa na vilema kwa mfano?

Sijapata jibu la swali hili bado.
 
Is Uniformity one of the key elements to justify God's existence, siyo? Good, sasa hapo mwanzo biblia yako inatuambia hakukuwa na dhambi. Mungu Aliumba viumbe vyake vyote akiwemo Malaika Mkuu wake Lusifa a.k.a. Shetani wa leo akiwa mkamilifu. Ila ghafla bin vuu bwana mkubwa huyu akaota kiburi na kutaka kujifananisha na Muumba wake! Is this what you refer to be uniformity, one of your poor proofs of God's existence?
Give it another name, this is not what uniformity is. uniformity is well clarified in my post. So read it again!

Okay, following the same trend, Mungu Alijua kuwa Ulimwengu aliouumba baadaye ungetumbukia dhambini, sasa akaandaa mpango mkubwa, mgumu, wa gharama kubwa na tena usiofikirika eti wa kumkomboa mwanadamu kutoka dhambini! Sasa two issues to be addressed here:-Ikiwa ni kweli kuwa Mungu Alimpa mwanadamu uhuru wa kuchagua mema na mabaya (sawa na wewe Baba/Mama unavyoweza kumpa uhuru mwanao aende Mzumbe Secondary au Ikinabushu Secondary), iweje tena Baba/Mama huyu huyu aanze kumtishia mwanaye kuwa “ukichagua kwenda Ikinabushu Secondary nitakufukuza kwangu tena na kukuchoma moto”?

Umekosa kitu cha msingi hapa, acha nikusaidie. Upendo una maana ya chaguo. Ukioa (kama bado) utajua kuwa mke wako atakuwa ana chaguo la kufanya chochote, ikiwemo kukuacha wewe. Haya yote yamo ndani ya chaguo. Na akiisha kuchagua, madhara ya chaguo yanafuata. Hivi sio vitisho, ila ni madhara ya kimantiki kabisa ya chaguo husika. akikuacha kuna vitu atapoteza pia kama madhara ya chaguo lake.

Mfano rahisi kabisa huu nakupa. Una chaguo la kuruka toka ghorofa ya 17 PPF towers kama ukiataka au unaweza usiruke. lakini once ukiruka, madhara yake hayakwepeki. Huwezi sema "law of Gravity" inakutishia... la!

Next time usitumie mifano isiyoendana. Mfano uliotoa hauna moral implication a unaulinganisha na kitu ambacho kina moral implications. Absurd example!


Back to Uniformity: Kama mwanadamu naye alikuwa mkamilifu, baadaye akaasi na mpango wa kumuokoa kutoka dhambini ukasukwa, sasa tuna uhakika gani kuwa mwanadamu yule yule atakayekuwa ameokolewa dhambini hataasi tena ktk paradise/akhera/mbingu/dunia ijayo?
Simple! Mungu aliyeona na kujua kabla hayajatokea unayoeleza hapo juu ndiye aliyesema haitatokea. Na kwa kuwa anajua yote, "I rest assured". Wewe kwa upande wako huna cha kuegemea ila kutegemea bahati nasibu. Haua assurance yeyote kwa kuwa utupu hautegemewi.... you are doomed!

Kwa nini hapa usione kuwa kuna Non-uniformity katika plans za huyo Mungu wako? Iweje Duniani pa likuwa Patakatifu, Kisha Dhambi na Tunaambiwa Baadaye tena patakuwa Patakatifu lakini hatuelezwi kuwa yawezekana ikaja kuwa tena Dhambi na kufanya iwe Loop inayoonyesha hiyo Uniformity yako? Sasa Utakatifu >>> Dhambi >>> Utakatifu ndio hiyo Uniformity unayoizungumzia hapa?
What you are talking about is going in circle not uniformity. I cannot believe you do not understand what it is even after writing it in simple manner. Go and read it again!

Na ni nini mpango wa Mungu endapo tena mwanadamu atakuja kuasi akifika huko mbinguni? Maana hapo mwanzo Mungu Alijua kuwa kiumbe wake mkamilifu angeasi, akajiandaa, lakini this time tunaambiwa kuwa huko mbinguni hakutakuwa na dhambi wala kifo tena (just as it was in the beginning) lakini hatuambiwi nini kitatokea endapo hali ikigeuka kuwa ndivyo sivyo! Au wanadamu watakaokuwepo kule hawatakuwa tena na uchaguzi wa kuamua njia waitakayo kama wale wa awali walivyopewa fursa hiyo? If that is the case, ina maana huyo Mungu atakuwa amewafunga watu wake wasiwe na any other choice except him? Na kama hivi ndivyo basi huyo Mungu hajiamini, ni dikteta wa hali ya juu na hajali athari za mabavu yake kwa watoto wake mwenyewe maana kama angelikuwa na upendo basi asingewanyima uhuru wao kama ule aliowapa hapo mwanzo!

God who knows all have settled this issue once for all. Amesema hakutakuwa na uove tena baada ya dunia hii na mbingu hizi kupita. So you either trust Him or trust your limited thinking that ends no where. There is no other choice there. Sasa unataka Mungu aandae mpango wa kitu ambacho hakitatokea? What for? God is best at economics 🙂


By the way, wewe (Mungu) ni Mwalimu wa Sanaa (Arts), unafundisha wanafunzi, kutunga mitihani, kusahihisha na mwisho kutoa matokeo. Sasa iweje tena wewe huyo huyo ulazimishe kutoa matokeo ya wanafunzi waliofanya somo la Hisabati ilhali halikuhusu, hukusomea, hukuwafundisha na wala hukutunga mtihani huo? Maana yangu ni kwamba, kwanini Mungu asi-deal na wale wanaofuata sheria zake tu (yaani awalinde, awatunze, awahudumie na hatimaye siku atakayoona inafaa awapeleke anakotaka yeye basi) na badala yake ana-cross over na kuwafuata wale wasiomuamini na kujifanya ndiye Jaji wao? Kwanini wale wasiomuamini (kwa maana nyingine ni wafuasi wa Mzee Mzima Shetani) asiwaache nao walindwe, watunzwe, wahudumiwe na hatimaye wapelekwe kule ambako Master wao atataka wawe halafu mwishoni ndio atoe ushuhuda kuwa “Niliwaambia hamkusikia, oneni jinsi uchaguzi wenu ulivyowagharimu”? Hayo ya Ngoswe yanamhusu nini yeye huyo Mungu wenu? Mbona huyo Kiongozi wa hilo kundi lingine (Shetani) yuko kimya tu, hajatangaza adhabu kwa wale wasiomtii (kama wewe unayejidai ni mfuasi wa Mungu)? Iweje huyu muungwana (Shetani) asiwe na noma kwenu nyie mnaokesha na kumtukana mchana na usiku kucha lakini kinyume chake huyo Mungu wenu mnayempamba ni mwenye haki na upendo atangaze shari kwa wasiomfuata? Yaani ni sawa na Kikwete (Rais wa Nchi na Watz wote + M/Kiti wa Magamba) atangaze kiama na majanga kwa watu wote wasio wafuasi wa Magamba lakini Dr. Slaa/Mbowe/Lipumba/Cheyo/Mrema/Mbatia/Mtikila/et al wao wabaki kimya wala hawawalalamikii watu ambao hawawaungi mkono/ni wafuasi wa Magamba, sasa kati ya pande hizi mbili ni upi unaoonekana kutenda haki na uungwana kwa standards za kibinadamu? Sasa iwapo kwa stabdards za kibinadamu imekuwa hivyo, habari gani kwa standards za huyo Mungu? Kwanini isiwe hivyo?????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Mfano wako uko na matatizo lukuki. Nitakuelewesha kitu ambacho aidha hukijui au umefumbia macho. Mungu sio mwalimu wa sanaa,. Mungu ni Mfalme wa Ulimwengu na Hakimu wa Ulimwengu huu. Mungu ni mmiliki halali wa watu wote, mimi wewe na yule.

Akiwa kama mfalme ana haki ya kuamua chochote. Akiwa kama hakimu ana mamlaka ya kuhukumu wote bila kujali anamwamini au la. Na akiwa kama mmiliki ana mamlaka ya kufanya chochote na mali zake. Sheta si mfalme bali mi kiumbe chini ya Mfalme. Shetani si hakimu bali mhalifu, na wafuasi wake ni waasi, wahalifu tu. Shetani hana anachomiliki bali ni mwizi. Kumlinganisha shetani na Mungu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu sana!


Kwa hali ya kibinadamu, wanasema “wengi wape”. Ninyi licha ya Shetani kutolalamika wala kuomba kutukuzwa kama vile Mungu wenu anavyotaka atukuzwe mchana na usiku kucha, lakini hata hivyo watu wengi (naamini na wewe ukiwemo) mnaimba mko kwa Mungu lakini matendo yenu hayana tofauti na ya Mzee Mzima Shetani! Hata huyo Yesu wenu aliwahi kukiri, kuwa vinywa vyenu vinaimba Mungu lakini miondoko na midundo ya matendo yenu ni ya Mzee mzima ambaye mnakesha mchana kutwa mkimpiga vijembe! Hii ina maana gani?????? Maana yake ni kwamba huyo Mungu wenu kimantiki hayupo maana kaweka vigezo vigumu sana vya kumfikia, na hata yeye mwenyewe anakiri kuwa njia yake ni nyembamba na waionao ni wachache! Yohana aliona idadi ya watakaourithi ufalme wa mbinguni ni mia moja arobaini na nne elfu tu! Sasa kati ya Watu zaidi ya 2 billion tuliopo, wateule ni sawa na asilimia 0.0072 tu! Anyway, sasa kama hivyo ndivyo itakavyokuwa, kwa nini nisiamini kuwa kitendo cha Mungu kuamua kuja kuchoma moto dunia hii (na wakati wa Nuhu kugharikisha dunia nzima) ni wivu tu baada ya Sera zake kukataliwa na watoto wake wa kuumba yeye mwenyewe? Kwanini isiwe hivyo iwapo hata kule mbinguni alivyotaka kupima ubavu na Lusifa Mzee Mzima alijinyakulia theluthi 1 ya malaika wote tena kwa mkupuo pasipo kufanya kampeni? BY LOGIC: Iwapo hao malaika na hata Lusifa mwenyewe aliyekuwepo kule mbinguni na akawa karibu sana na huyo Mungu waliasi, habari gani wewe Mnyalukolo mwenzangu ambaye hukuwahi hata kwenda juu ya haya mawingu tunayoyaona ujiaminishe kiasi hicho kuwa Mungu wako unayemtumainia ni mwenye upendo, huruma na msamaha? Hivi mwanao akikaidi ushauri wako na akaamua kufanya maamuzi yake anayoona ni sahihi kwake utamwadhibu au utamsikitikia na kumuonea huruma kwa kitakachompata? Sasa iweje kwa standards za Mungu JEHANAMU ndio iwe kusudio kwa wale watakaomkataa badala ya kuwahurumia, kuwasikitikia na ikiwezekana kuwaepushia majanga hayo????? Hivi bado tu hujaona mantiki hapa, au unaendelea kuimba na kukariri tu kama ambavyo wajanja fulani waliwataka muendelee kuamini hivyo milele? Unachekesha aiseee!!!!!!!!!!!

Hapa basically kuna maswali mawili tu: Moja kwa Mungu hakuna kitu kama Wengi wape. Mungu sio Kaisari wa Rumi na mambo ya "vox populi, vox dei". Kwa Mungu hata wote tukaamua dhambi ni sawa kwake itabaki kuwa dhambi na wote tutahukumiwa tu!

Pili, hizo assumption zako sio kitu ambacho Biblia inafundisha. na kwa kuwa ni tatizo la kutafsiri vibaya, sitaendelea zaidi. kama unataka kujua nini hasa Biblia inasema, fungua uzi wake. uzi huu una malengo na sio "one stop" ya mambo yote ya Biblia. Stick to the topic


MWISHO: Eti kuna Mungu au Shetani ni nadharia tu zisizo na mantiki wala mashiko yoyote katika viwango viwavyo vyovyote vile, hata iwe ni kwa kutumia akili ndogo kabisa za kibinadamu maana hata yasemwayo kuhusu hao wawili hayawezi kuthibitishwa pasipo kuacha chembe ya shaka! So, what for? Leave this Topic alone, don't waste your precious time at all!


Waoo! Asante kwa kuhakikisha nilichosema ktk post yangu ya kwanza. Ya kuwa ninyi watu hamna ushahidi wowote wa kupinga uwepo wa Mungu, uwe wa kisayansi au kimantiki. Ila imani katika dini yenu ya "hakuna Mungu". Imani hii imewafanya mshindwe kabisa kufikiri sawasawa kwa hofu ya kukiuka misingi ya dini yenu hii na hivyo kutumia "rhetorics" kama kichaka cha kujificha.

Rudi katika uzi na ujibu hoja za msingi sana hizi. Kumbuka issue kubwa hapa ni kuwa Mungu yupo na kuna implications zake kama utamwamini na zawadi yake ya Wokovu au utamkataa. Kwa hiyo the bottom line is not arguments but consequencces of the choice....choose carefully!
 
The problem of evil remain unanswered.

I need not go further until this problem is solved.
 
Kiranga tunasubiri ufafanuzi wako kwa swali hili toka kwa Stefano Mtangoo -"Why should things be uniform in random universe where things just run themselves through chance?"

What is uniform? Which things are uniform? How big is the universe? How much of it have you observed? How much of it is observable?

Mimi sijajibiwa swali langu pia.

Kama mungu ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kwa nini kaumba ulimwengu uliojaa maovu?

Kwa nini karuhusu viumbe wake wateseke? Watoto wazaliwe na vilema?
 
Halafu waamini hawajanijibu kuhusu "problem of evil" bado
What is evil in the world where there is no standard to differentiate good from evil?
Are you saying you have standards?
What are they?
Who sets them?
By what authority?

Huwezi sema kuhusu mabaya na ilhali katika dini unayoamini ya "hakuna Mungu" hakuna jema wala baya.
Lazima ukubaliane uwepo wa Mungu ndipo uhoji habari ya maovu. Vinginevyo swali lako linakosa mantiki yeyote!

4. Watu hawa wasioamini Mungu yupo huamini kuwa kama Mungu angalikuwepo kusingelikuwa na magonjwa na maumivu haya yote. Hawa watu wanaamini kuwa magonjwa ni kitu kibaya, na hata maumivu. Lakini swali wanaloliruka ni kuwa ili utofautishe kati ya mazuri na mabaya lazima kuwe na sheria iliyo juu ya wanadamu wote (absolute law) iliyo juu ya wanadamu wote. viginevyo bay kwa huyu laweza lisiwe baya kwa yule. Na ili kuwepo na sheria hiyo lazima awepo mtunga sheria aliye juu ya wanadamu wote. Watu hawa wanamkataa mtunga sheria huyu (Mungu) na hivyo wanapoteza sheria yenyewe na kimantiki mambo yote yanapaswa kuwa na hali sawa (hakuna baya au zuri). sasa wanpolalamika juu ya magonjwa na matatizo wanapimaje ubaya na uzuri? Je watu hawa hawawezi kuwaza haya yote? Je ni wajinga? Hapana, ni werevu sana. Ila tamko la dini yao linadai "Mungu hayupo" na wao kukiri kinyume na hivyo ni kuikana imani yao. Wanaenda kidini zaidi na sio kisayansi wala kimantiki!
 
The problem of evil remain unanswered.

I need not go further until this problem is solved.
Whooa! Thanks for proving my point, that you atheist do things by faith, blind faith actually!
You have not answered any of posed question and you keep singing problem of evil.

Evil and good have to be differentiated under a basis and the basis must transcend humans if that basis is to be honored and enforced to humans. And that basis must come from a Being, transcendent and Personal. You deny the being and there by you loose the basis and so in your religion of No God there is no such thing as good nor evil.

That being said what is your question?
 
What is evil in the world where there is no standard to differentiate good from evil?
Are you saying you have standards?
What are they?
Who sets them?
By what authority?

For the sake of argument, let's use your very god and his ten commandments.

Anawaambia watu "usiue". Let's say kuua ni an evil thing. Kwa nini yeye kaumba ulimwengu ambao kifo kinawezekana? Kwa nini anampa mama ujauzito halafu mtoto anakufa stillborn? Kwa nini mungu anaruhusu kifo?

Huwezi sema kuhusu mabaya na ilhali katika dini unayoamini ya "hakuna Mungu"

Mimi sitaki kuamini, ndiyo maana nauliza maswali. Ningetaka kuamini nisingeuliza maswali.

hakuna jema wala baya.

Kuna secular humanists wana standards nzuri tu za mema na mabaya. Kuliko za waumini. Wanafanya hata bila kutumaini ahadi ya pepo wala kuogopa moto.

Kuna watu kibao Asia hawaamini kwamba mungu yupo na hilo halisababishi wafanye maovu zaidi.

Na kuna watu wapo na vyeo vikubwa vya kanisa, lakini wanafanya maovu kila siku. Wanalawiti watoto na kukwiba hela.

Kwa hiyo usitake kusema imani ya mungu ndiyo ina monopoly ya kufanya mema.

Lazima ukubaliane uwepo wa Mungu ndipo uhoji habari ya maovu. Vinginevyo swali lako linakosa mantiki yeyote!

Suppose a all powerful, all knowing and all loving god is there, for the sake of argument, why did he create a world with so much evil?

Alikuwa hawezi kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Alikuwa hawezi kuumba ulimwengu ambao mtoto hawezi kuzaliwa na kilema?
 
Whooa! Thanks for proving my point, that you atheist do things by faith, blind faith actually!
You have not answered any of posed question and you keep singing problem of evil.

Evil and good have to be differentiated under a basis and the basis must transcend humans if that basis is to be honored and enforced to humans. And that basis must come from a Being, transcendent and Personal. You deny the being and there by you loose the basis and so in your religion of No God there is no such thing as good nor evil.

That being said what is your question?

Which posed questions, can you point to the specific post?

Some questions have been answered umpteen times hapa, labda wewe umekuja jana hujaona majibu.

Nipe exact post number niangalie kama unataka input yangu.

Ukija na maswali ya "argument from design" tulishayararua kitambo hapa.
 
Which posed questions, can you point to the specific post?

Some questions have been answered umpteen times hapa, labda wewe umekuja jana hujaona majibu.

Nipe exact post number niangalie kama unataka input yangu.

Ukija na maswali ya "argument from design" tulishayararua kitambo hapa.
Well well!
My post have claims and I back the claims. Do you agree with me?
If not then you need to refute them! You have not done so.

Here are the claims:
Kifupi katika uzi huu nimelenga kuonesha kuwa:

  1. Wakristo na wasioamini Mungu wa biblia wote wanafanya haya kwa imani
  2. Imani katika Mungu wa Biblia ni "sound and solid" na inakubaliana na sayansi asilimia zote
  3. Imani ya hawa wandugu ni ya upofu, inayopingana na sayansi na mantiki kwa namna zote

So you have the ball in your court, play it (with all who take no God position of course)
 
Stefano Mtangoo,Nungu akubariki sana kwa somo zuri na lenye mafundisho makubwa sana,nimejifunza kitu kwako mkuu

Labda tu kwa tahadhari ni kwamba huyo jamaa ni mbishi tu ana kawaida ya kuimba nyimbo ambazo tayari zimeshajibiwa,tayari hapo juu nimeshaona ameanza mambo yake wakati majibu na maswali ambayo alitakiwa ajibu yapo kwenye mada

Pia kuna wale wengine wanaofuata mkumbo wa huyo jamaa nao hao wana vichekesho vyao
Mtu anakuja na kusema "mtu ameshasema anaamini basi sina swali zaidi,mimi nataka kujua sitaki kuamini" mtu kama huyu sijui utamuweka kundi gani

Ukimuuliza huko kusema "Mungu hayupo" ni nini?
Ujuzi au kitu gani hakujibu,anabaki anazunguka tuu bila kutoa majibu

Wakaaa kuimba wimbo problem of evil bila kujua hata huko kusema evil ni kutokana na utambuzi wao wa evil na ni matokeo ya kuwepo sheria na hata huyo aliyeweka hizo sheria hawamjui,sijui wanakananje kuwa hiyo nayo sio Imani

Mkuu ngoja niwe mtazamaji kwa sasa maana naona hawa unawatosha kabisa

Ubarikiwe kwa baraka za Mungu wetu mwenye upendo usiopimika!
 
Last edited by a moderator:
Kitu gani umejifunza, labda wengine tumekimiss, please do share.

Mkulima,ulishindwa kuchomoka kwenye ile mada nyingine
Unadhani na hii utachomoka?

Zile mbinu zako za kuondoka na kurudi kuuliza maswali yaleyale ambayo yameshajibiwa hapa hazina mashiko
Jibu swali kisha uulize swali

Kazi yangu hapa ni kukukagua tu,ukijidai hamnazo umeisha!
Tunasubiri majibu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom