Is Uniformity one of the key elements to justify God's existence, siyo? Good, sasa hapo mwanzo biblia yako inatuambia hakukuwa na dhambi. Mungu Aliumba viumbe vyake vyote akiwemo Malaika Mkuu wake Lusifa a.k.a. Shetani wa leo akiwa mkamilifu. Ila ghafla bin vuu bwana mkubwa huyu akaota kiburi na kutaka kujifananisha na Muumba wake! Is this what you refer to be uniformity, one of your poor proofs of God's existence?
Give it another name, this is not what uniformity is. uniformity is well clarified in my post. So read it again!
Okay, following the same trend, Mungu Alijua kuwa Ulimwengu aliouumba baadaye ungetumbukia dhambini, sasa akaandaa mpango mkubwa, mgumu, wa gharama kubwa na tena usiofikirika eti wa kumkomboa mwanadamu kutoka dhambini! Sasa two issues to be addressed here:-Ikiwa ni kweli kuwa Mungu Alimpa mwanadamu uhuru wa kuchagua mema na mabaya (sawa na wewe Baba/Mama unavyoweza kumpa uhuru mwanao aende Mzumbe Secondary au Ikinabushu Secondary), iweje tena Baba/Mama huyu huyu aanze kumtishia mwanaye kuwa ukichagua kwenda Ikinabushu Secondary nitakufukuza kwangu tena na kukuchoma moto?
Umekosa kitu cha msingi hapa, acha nikusaidie. Upendo una maana ya chaguo. Ukioa (kama bado) utajua kuwa mke wako atakuwa ana chaguo la kufanya chochote, ikiwemo kukuacha wewe. Haya yote yamo ndani ya chaguo. Na akiisha kuchagua, madhara ya chaguo yanafuata. Hivi sio vitisho, ila ni madhara ya kimantiki kabisa ya chaguo husika. akikuacha kuna vitu atapoteza pia kama madhara ya chaguo lake.
Mfano rahisi kabisa huu nakupa. Una chaguo la kuruka toka ghorofa ya 17 PPF towers kama ukiataka au unaweza usiruke. lakini once ukiruka, madhara yake hayakwepeki. Huwezi sema "law of Gravity" inakutishia... la!
Next time usitumie mifano isiyoendana. Mfano uliotoa hauna moral implication a unaulinganisha na kitu ambacho kina moral implications. Absurd example!
Back to Uniformity: Kama mwanadamu naye alikuwa mkamilifu, baadaye akaasi na mpango wa kumuokoa kutoka dhambini ukasukwa, sasa tuna uhakika gani kuwa mwanadamu yule yule atakayekuwa ameokolewa dhambini hataasi tena ktk paradise/akhera/mbingu/dunia ijayo?
Simple! Mungu aliyeona na kujua kabla hayajatokea unayoeleza hapo juu ndiye aliyesema haitatokea. Na kwa kuwa anajua yote, "I rest assured". Wewe kwa upande wako huna cha kuegemea ila kutegemea bahati nasibu. Haua assurance yeyote kwa kuwa utupu hautegemewi.... you are doomed!
Kwa nini hapa usione kuwa kuna Non-uniformity katika plans za huyo Mungu wako? Iweje Duniani pa likuwa Patakatifu, Kisha Dhambi na Tunaambiwa Baadaye tena patakuwa Patakatifu lakini hatuelezwi kuwa yawezekana ikaja kuwa tena Dhambi na kufanya iwe Loop inayoonyesha hiyo Uniformity yako? Sasa Utakatifu >>> Dhambi >>> Utakatifu ndio hiyo Uniformity unayoizungumzia hapa?
What you are talking about is going in circle not uniformity. I cannot believe you do not understand what it is even after writing it in simple manner. Go and read it again!
Na ni nini mpango wa Mungu endapo tena mwanadamu atakuja kuasi akifika huko mbinguni? Maana hapo mwanzo Mungu Alijua kuwa kiumbe wake mkamilifu angeasi, akajiandaa, lakini this time tunaambiwa kuwa huko mbinguni hakutakuwa na dhambi wala kifo tena (just as it was in the beginning) lakini hatuambiwi nini kitatokea endapo hali ikigeuka kuwa ndivyo sivyo! Au wanadamu watakaokuwepo kule hawatakuwa tena na uchaguzi wa kuamua njia waitakayo kama wale wa awali walivyopewa fursa hiyo? If that is the case, ina maana huyo Mungu atakuwa amewafunga watu wake wasiwe na any other choice except him? Na kama hivi ndivyo basi huyo Mungu hajiamini, ni dikteta wa hali ya juu na hajali athari za mabavu yake kwa watoto wake mwenyewe maana kama angelikuwa na upendo basi asingewanyima uhuru wao kama ule aliowapa hapo mwanzo!
God who knows all have settled this issue once for all. Amesema hakutakuwa na uove tena baada ya dunia hii na mbingu hizi kupita. So you either trust Him or trust your limited thinking that ends no where. There is no other choice there. Sasa unataka Mungu aandae mpango wa kitu ambacho hakitatokea? What for? God is best at economics
🙂
-
By the way, wewe (Mungu) ni Mwalimu wa Sanaa (Arts), unafundisha wanafunzi, kutunga mitihani, kusahihisha na mwisho kutoa matokeo. Sasa iweje tena wewe huyo huyo ulazimishe kutoa matokeo ya wanafunzi waliofanya somo la Hisabati ilhali halikuhusu, hukusomea, hukuwafundisha na wala hukutunga mtihani huo? Maana yangu ni kwamba, kwanini Mungu asi-deal na wale wanaofuata sheria zake tu (yaani awalinde, awatunze, awahudumie na hatimaye siku atakayoona inafaa awapeleke anakotaka yeye basi) na badala yake ana-cross over na kuwafuata wale wasiomuamini na kujifanya ndiye Jaji wao? Kwanini wale wasiomuamini (kwa maana nyingine ni wafuasi wa Mzee Mzima Shetani) asiwaache nao walindwe, watunzwe, wahudumiwe na hatimaye wapelekwe kule ambako Master wao atataka wawe halafu mwishoni ndio atoe ushuhuda kuwa Niliwaambia hamkusikia, oneni jinsi uchaguzi wenu ulivyowagharimu? Hayo ya Ngoswe yanamhusu nini yeye huyo Mungu wenu? Mbona huyo Kiongozi wa hilo kundi lingine (Shetani) yuko kimya tu, hajatangaza adhabu kwa wale wasiomtii (kama wewe unayejidai ni mfuasi wa Mungu)? Iweje huyu muungwana (Shetani) asiwe na noma kwenu nyie mnaokesha na kumtukana mchana na usiku kucha lakini kinyume chake huyo Mungu wenu mnayempamba ni mwenye haki na upendo atangaze shari kwa wasiomfuata? Yaani ni sawa na Kikwete (Rais wa Nchi na Watz wote + M/Kiti wa Magamba) atangaze kiama na majanga kwa watu wote wasio wafuasi wa Magamba lakini Dr. Slaa/Mbowe/Lipumba/Cheyo/Mrema/Mbatia/Mtikila/et al wao wabaki kimya wala hawawalalamikii watu ambao hawawaungi mkono/ni wafuasi wa Magamba, sasa kati ya pande hizi mbili ni upi unaoonekana kutenda haki na uungwana kwa standards za kibinadamu? Sasa iwapo kwa stabdards za kibinadamu imekuwa hivyo, habari gani kwa standards za huyo Mungu? Kwanini isiwe hivyo?????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mfano wako uko na matatizo lukuki. Nitakuelewesha kitu ambacho aidha hukijui au umefumbia macho. Mungu sio mwalimu wa sanaa,. Mungu ni Mfalme wa Ulimwengu na Hakimu wa Ulimwengu huu. Mungu ni mmiliki halali wa watu wote, mimi wewe na yule.
Akiwa kama mfalme ana haki ya kuamua chochote. Akiwa kama hakimu ana mamlaka ya kuhukumu wote bila kujali anamwamini au la. Na akiwa kama mmiliki ana mamlaka ya kufanya chochote na mali zake. Sheta si mfalme bali mi kiumbe chini ya Mfalme. Shetani si hakimu bali mhalifu, na wafuasi wake ni waasi, wahalifu tu. Shetani hana anachomiliki bali ni mwizi. Kumlinganisha shetani na Mungu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu sana!
-
Kwa hali ya kibinadamu, wanasema wengi wape. Ninyi licha ya Shetani kutolalamika wala kuomba kutukuzwa kama vile Mungu wenu anavyotaka atukuzwe mchana na usiku kucha, lakini hata hivyo watu wengi (naamini na wewe ukiwemo) mnaimba mko kwa Mungu lakini matendo yenu hayana tofauti na ya Mzee Mzima Shetani! Hata huyo Yesu wenu aliwahi kukiri, kuwa vinywa vyenu vinaimba Mungu lakini miondoko na midundo ya matendo yenu ni ya Mzee mzima ambaye mnakesha mchana kutwa mkimpiga vijembe! Hii ina maana gani?????? Maana yake ni kwamba huyo Mungu wenu kimantiki hayupo maana kaweka vigezo vigumu sana vya kumfikia, na hata yeye mwenyewe anakiri kuwa njia yake ni nyembamba na waionao ni wachache! Yohana aliona idadi ya watakaourithi ufalme wa mbinguni ni mia moja arobaini na nne elfu tu! Sasa kati ya Watu zaidi ya 2 billion tuliopo, wateule ni sawa na asilimia 0.0072 tu! Anyway, sasa kama hivyo ndivyo itakavyokuwa, kwa nini nisiamini kuwa kitendo cha Mungu kuamua kuja kuchoma moto dunia hii (na wakati wa Nuhu kugharikisha dunia nzima) ni wivu tu baada ya Sera zake kukataliwa na watoto wake wa kuumba yeye mwenyewe? Kwanini isiwe hivyo iwapo hata kule mbinguni alivyotaka kupima ubavu na Lusifa Mzee Mzima alijinyakulia theluthi 1 ya malaika wote tena kwa mkupuo pasipo kufanya kampeni? BY LOGIC: Iwapo hao malaika na hata Lusifa mwenyewe aliyekuwepo kule mbinguni na akawa karibu sana na huyo Mungu waliasi, habari gani wewe Mnyalukolo mwenzangu ambaye hukuwahi hata kwenda juu ya haya mawingu tunayoyaona ujiaminishe kiasi hicho kuwa Mungu wako unayemtumainia ni mwenye upendo, huruma na msamaha? Hivi mwanao akikaidi ushauri wako na akaamua kufanya maamuzi yake anayoona ni sahihi kwake utamwadhibu au utamsikitikia na kumuonea huruma kwa kitakachompata? Sasa iweje kwa standards za Mungu JEHANAMU ndio iwe kusudio kwa wale watakaomkataa badala ya kuwahurumia, kuwasikitikia na ikiwezekana kuwaepushia majanga hayo????? Hivi bado tu hujaona mantiki hapa, au unaendelea kuimba na kukariri tu kama ambavyo wajanja fulani waliwataka muendelee kuamini hivyo milele? Unachekesha aiseee!!!!!!!!!!!
Hapa basically kuna maswali mawili tu: Moja kwa Mungu hakuna kitu kama Wengi wape. Mungu sio Kaisari wa Rumi na mambo ya "vox populi, vox dei". Kwa Mungu hata wote tukaamua dhambi ni sawa kwake itabaki kuwa dhambi na wote tutahukumiwa tu!
Pili, hizo assumption zako sio kitu ambacho Biblia inafundisha. na kwa kuwa ni tatizo la kutafsiri vibaya, sitaendelea zaidi. kama unataka kujua nini hasa Biblia inasema, fungua uzi wake. uzi huu una malengo na sio "one stop" ya mambo yote ya Biblia. Stick to the topic
-
MWISHO: Eti kuna Mungu au Shetani ni nadharia tu zisizo na mantiki wala mashiko yoyote katika viwango viwavyo vyovyote vile, hata iwe ni kwa kutumia akili ndogo kabisa za kibinadamu maana hata yasemwayo kuhusu hao wawili hayawezi kuthibitishwa pasipo kuacha chembe ya shaka! So, what for? Leave this Topic alone, don't waste your precious time at all!
-
Waoo! Asante kwa kuhakikisha nilichosema ktk post yangu ya kwanza. Ya kuwa ninyi watu hamna ushahidi wowote wa kupinga uwepo wa Mungu, uwe wa kisayansi au kimantiki. Ila imani katika dini yenu ya "hakuna Mungu". Imani hii imewafanya mshindwe kabisa kufikiri sawasawa kwa hofu ya kukiuka misingi ya dini yenu hii na hivyo kutumia "rhetorics" kama kichaka cha kujificha.
Rudi katika uzi na ujibu hoja za msingi sana hizi. Kumbuka issue kubwa hapa ni kuwa Mungu yupo na kuna implications zake kama utamwamini na zawadi yake ya Wokovu au utamkataa. Kwa hiyo the bottom line is not arguments but consequencces of the choice....choose carefully!