Mungu Yupo: Majibu kwa Wasioamini

Status
Not open for further replies.
Ungekuwa umejibu maswali na kusoma maelezo yangu kwenye ile post niliyojiquote kisha nikakuambia kuna maswali ambayo unatakiwa uyajibu hapo usingekuja na hizi ngano zako hapa!
 
Hakika hakuna mungu aliyehai wala aliye kufa. Hakuna ushahidi wowote wa uwepo wa mungu, na hata mleta uzi hakuna sehemu hata moja uliyothibitisha uwepo wa mungu pasipo na shaka, zote ulizoandika ni porojo tu ili kutetea unachokiamini. Aidha, kutokuwepo ushahidi kuwa hakuna mungu (no god) hakumaanishi uwepo wa huyo mungu unayemsema.....HAKIKA HAKUNA MUNGU.
 
This is ridiculous, kwani nani aliyekuambia kuwa ili kujua JEMA na BAYA ni sharti ukubali kuna Mungu?
Kwanini unadhani nahitaji kuambiwa kitu na yoyote?
Kama hutumii kanuni ya Mungu niambie umewezaje kutofautisha au kujua hili ni Jema na hili ni baya?
Bado hujaniambia hilo
Una uthibitisho wowote kuwa chanzo cha JEMA ni Mungu??????????? Ulete hapa huo ushahidi!
Stop right there,
Kabla mimi sijathibitisha kuwa Ili kuwe na jema na baya ni hadi Mungu awepo wewe unatakiwa uthibitishe kauli yako kwanza kuwa Jema au baya sio lazima liwe kwa fasiri ya Mungu yupo!
 

Tunaomba ushahidi wa kutokuwepo Mungu!

Au kukosekana kwa ushahidi wa kuwepo Mungu[kwa mujibu wa madai yenu] ndio uthibitisho wa kutokuwepo kwake?

Halafu hata hujaielewa mada wewe!
 
Hapo hakuna Ligi yoyote mkuu, maana kiukweli hakuna cha Timu A (Yesu) wala Timu B (Mungu), sasa hapo ligi itakuwa ni ya Nani V/s Nani?

Umefanya utafiti ukakuthibitishia hayo?
Kama umefanya tuletee hapa utakuwa umetusaidia sana

Pia kuna tuzo kubwa sana itakuwa inakusubiri maana miaka zaidi ya elf 2 watu wamehangaika kutafuta uthibitisho wa kukanusha hilo wameshindwa

Tusaidie tafadhali!
 
Huo ndio uthibitisho?

Hata hivyo,je unakubali kuwa binadamu kaumbwa ili tuanzie hapo kutafuta majibu kama aliemuumba nae kaumbwa?
 
Tunaomba ushahidi wa kutokuwepo Mungu!

Au kukosekana kwa ushahidi wa kuwepo Mungu[kwa mujibu wa madai yenu] ndio uthibitisho wa kutokuwepo kwake?

Halafu hata hujaielewa mada wewe!

unaongozwa na emotion zaidi kuliko uhalisia, kama unadhani sijaelewa topic nieleweshe mbuzi. imani zenu za ki-p.umbavu hizo kuwa kuna mungu ndio zinawapotosha. wewe unaweza kuprove uwepo wa huyo mungu? hakuna ushahidi wowote wa uwepo wa mungu wala kutokuwepo kwake....
 
Ungekuwa umejibu maswali na kusoma maelezo yangu kwenye ile post niliyojiquote kisha nikakuambia kuna maswali ambayo unatakiwa uyajibu hapo usingekuja na hizi ngano zako hapa!

Ungekuwa umesema maswali ni yapi ungejibiwa.

Kuna maswali yashajibiwa kabla, nimekueleza hilo, nimekuambia unioneshe specifically maswali yapi yanayohitaji majibu nikuletee majibu yake, umeshindwa.
 
Enyi msioamini uwepo wa Mungu, yatafakarini haya machache japo kidogo;

  • Jinsi solar system ilivyo, sayari hazigongani, wala hazitoki kwenye orbit zake,
  • Majira mbali mbali tuliyonayo yanayotuwezesha kulima na kuvuna, wanyama kupata majani, nk
  • Mimea mbali mbali itoayo matunda, maua nk
  • Wanyama wa aina mbali mbali, wakali na wapole na wote hawa wanapata chakula chao. Wala nyama wamepewa viungo vya kuwawezesha kufanys hivyo, na wala mimea kadhalika.
  • Wanyama wadhaifu wamepewa namna ya kujilinda, mfano, kinyonga ili awakwepa adui zake, anabadilika randi ili asionekane, kobe kapewa gamba gumu kwa ajili ya kujificha nk
  • Chunguza viungo mbali mbali vya mwili wa binadamu au mnyama mwingine vivyofanya kazi, eg ubongo, moyo, figo nk.

Hapa haya yote hayawezi kuwa yalitokea by CHANCE, ni by DESIGN. and therefore there is a DESIGNER

Kwa hiyo mtu yeyote ambaye yupo objective kabisa, ni rahisi kuamini kuwa kuna source ya haya mambo yote kuliko kudhani yalitokea tu kwa bahati. Kwa sababu ukiamini hakuna aliye DESIGN, unakuwa huna kitu cha kuegemea imani yako hiyo tofauti na anayeamini.
 

Kwa kuongezea,

Kama mungu hayupo, ninategemea kusiwe na ushahidi wa yeye kutokuwepo.

Kwa sababu hayupo.

Hatuna ushahidi wa vitu ambavyo havipo kwamba havipo.

Kwa sababu havipo.

Hatuna ushahidi kwamba juu ya mlima Kilimanjaro hakuna babu mwenye macho matatu anaye control dunia.

Kwa sababu hayupo.

On the other hand. Vitu vilivyopo vinaweza kutafutwa na kupatiwa ushahidi.

Kwa sababu vipo.

Kwa hiyo, kujibu suala hili conclusively, wanaosema mungu yupo ni wajibu wao kuleta ushahidi kwamba yupo.

Wanaobishia kwamba yupo, hata wakikosa ushahidi, wanaweza kusema wamekosa ushahidi kwamba hayupo kwa sababu hayupo.

Huwezi kuwa na ushahidi kwamba kitu hakipo, kwa sababu hakipo.
 
Ungekuwa umesema maswali ni yapi ungejibiwa.

Kuna maswali yashajibiwa kabla, nimekueleza hilo, nimekuambia unioneshe specifically maswali yapi yanayohitaji majibu nikuletee majibu yake, umeshindwa.

Ugoigoi wako huu unatupa kazi kubwa sana sisi
Haya maswali haya hapo,kumbuka sio maswali tu unatakiwa usome ni hadi hayo maelezo!


Halafu ili uelewe vizuri maana wewe una tatizo la kuelewa,fungua page no 5 utakuta nimekuquote ulichokisema kisha nikajibu na kukuuliza ili uone ni kwanini nimesa hiki au kile!!!!!!!!
 

Argument from design tushaichakaza mara mia kidogo hapa.

Kama complex systems ni lazima ziumbwe, kinachoumba hizo complex systems ni complex zaidi ya hivyo vinavyoumbwa.

Na kwa kuwa kitakuwa complex zaidi, na chenyewe itabidi kiwe kimeumbwa (kumbuka first principle yetu ni kwamba complex systems ni lazima ziwe zimeumbwa)

Kwa hiyo ukileta argument from design, basically itakufunga useme kwamba mungu naye kaumbwa, na aliyemuumba kaumbwa, na aliyemuumba aliyemuumba naye kaumbwa, ad infinitum, ad absurdum.

Sijui kama umeelewa ninachoandika.

Huwezi kusema kiti ni lazima kiwe kimeumbwa, halafu jumbo jet lmeweza kutokea lenyewe tu na kupaa angani.

Huwezi kusema binadamu na solar system lazima ziwe zimeumbwa (kwa sababu ni complex systems), halafu kitu kilichoziumba hizi systems ambacho ni complex zaidi (mungu) hakijaumbwa.

Logic yako mwenyewe inakufunga!
 

Hata ku quote tabu, sijui kipi kasema nani, kwa sababu ya quote mbovu.

Goigoi kati yangu na wewe unayeshindwa hata ku quote ni nani sasa?
 

Hata mtoto mdogo wa miaka 4 anaweza kuona ni nani anaeongozwa na hisia kati yangu na wewe!
 
Hata ku quote tabu, sijui kipi kasema nani, kwa sababu ya quote mbovu.

Goigoi kati yangu na wewe unayeshindwa hata ku quote ni nani sasa?
Kabla hujaispot hiyo tayari nimeshaiona zamani sana
Na tayari nimesharekebisha
Au huoni kama kuna tofauti?
Hii inaonesha namna unavyokurupuka

Unaendelea kuthibitisha ugoigoi wako!
 
Hata mtoto mdogo wa miaka 4 anaweza kuona ni nani anaeongozwa na hisia kati yangu na wewe!

nyie mnaosema kuna mungu mbona hamthibitishi, badala yake mnataka sisi tusioamini kuthibitisha uwepo wake? Thibitisheni kuwa kuna mungu, achaneni na hizo porojo la mleta mada.
 
Argument from design tushaichakaza mara mia kidogo hapa.
Kama complex systems ni lazima ziumbwe, kinachoumba hizo complex systems ni complex zaidi ya hivyo vinavyoumbwa

Sio kweli
Unajua nini maana ya kuumba wewe?
 
nyie mnaosema kuna mungu mbona hamthibitishi, badala yake mnataka sisi tusioamini kuthibitisha uwepo wake? Thibitisheni kuwa kuna mungu, achaneni na hizo porojo la mleta mada.

Wewe umethibitisha nini hapa?
 
Thibitisha hili na lile lingine

Hii mambo yako ya kuleta longolongo inaonesha hata hujui kithibitisha ni nini
Tutakesha hapa!

Thibitisho ni kwamba umeomba uthibitisho.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…