Duh mimi si mpenzi wa bongo music hata kidogo lakini nimeumia sana kuona hiyo picha kwani mwaka Jana Chid Benz alifanya show Kakola Kahama akiwa na mwili wenye afya kabisa!! Sasa masikitiko yangu ni watu hapa jamii forum wanavyomtukuna maskini wa mungu anayeomba msaada hata wa kimawazo tu kwa Watanzania na wasamaria wema. Duh Watanzania roho mbaya hadi wengine wamegusia kuwa alikuwa anamtukana Lowassa!!! Mimi mwenyewe nilikuwa team lowassa na hadi leo namkubali mzee lkn chuki za kwenye siasa siwezi kuzileta kwa mtu anayehitaji msaada. Duh Tanzania nchi niliyoaminishwa ina watu wenye mioyo mizuri lkn kwa sasa hawana tofauti na Mazombi ya Shein Zanzibar. Chid Benzi nakuombea kwa mungu kuanzia leo katika kipindi hiki cha Kwaresma taweka sala maalumu kwa ajili yako. Nakupenda kama kaka na kama mwana mpotevu ambaye umekumbuka makosa yako na kurudi kuomba msamaha kwa Watanzania wakusaidie ila bahati mbaya wengi washakuwa kama kundi la ISIS kwa mioyo ya kishetani. Mungu aliyekuumba hatakuacha uteseke na hakuna lisilowezekana ukimtumaini mungu atakuponya.
Sawa, lakini unawajua hawa na majibu yao wakiwa bado wana kijiafya ila madude wajayatumia..??
Angalia akina TID na wengine...
By the way kasema stress... umemsikia akitamka unga kwamba ndo umemuathili....??
Kweli ni vibaya kumsema sasa lakini ujuwe hujawahi kutana na Chid akiwa na afya yake Dar tena pale vijana kinondoni....
Hawa wasanii waone tu wakiwa wanaimba.. maisha yao halisi ni kuringa kujidai kudharau na kwa wakati wakiwa wazima huwa HAWASHAURIKI....
NA MBAYA ZAIDI WAKATI WAKIWA HAWASHAURIKI NI OMBAOMBA WA BIA ILE MBAYA.... nenda vijana ndo utanielewa..
Wapo wanajielewa lakini wachache sana na katika hao CHID HAYUMO...
wanakujaga kusumbua ndugu jamaa na marafiki wakifika hali kama hiyo...
MBAYA HAKUNA ANAYEKUBALI DIRECTLY KWAMBA WANABWIA UNGA..NI K
MPAKA WAKAMATIKE...
NA MOSTOF THEM BADO WANAISHI KWA NDUGU MARAFIKI NA WANA..
HUO NDO UKWELI KAMA HUAMINI FUATILIA