Baada ya mafanikio ya kujenga vituo vya daladala kwa kutumia mamia ya mamilioni ya shilingi katika sehemu kadhaa za jiji la Dar ea Salaam . Swali kuu ni :
JIJI LA DAR ES SALAAM WANA UBAVU WA KUSITISHA USAJILI MPYA WA BAJAJ?
Ni wakati wa madiwani kupitisha azimio kuratibu bajaji na bodaboda ili fedha zilizojenga vituo vya daladala jijini Dar es Salaam zisipotee bure.
Madiwani wa jiji la Mbeya wameweza kufanya maamuzi magumu kudhibiti bajaji na sasa hawa madiwani wa Dar es Salaam jiji kubwa kabisa katika Afrika ya Mashariki nao wachukue uamuzi haraka.
TOKA MAKTABA:
JIJI LA MBEYA WAPIGA MARUFUKU USAJILI WA BAJAJI MPYA
Baraza la Madiwani wa jijji la nyanda za juu kusini la Mbeya waelezea changamoto na kero ya wingi wa bajaj hadi kutapika na kusababisha vurugu, kuegesha bila tahadhari, ajali n.k hivyo kuna umuhimu wa kuratibu idadi ya bajaj ilingane na mahitaji halisi ya jiji.