SI KWELI Muonekano wa Mabasi mapya ya Mwendokasi yaliyoletwa na DART

SI KWELI Muonekano wa Mabasi mapya ya Mwendokasi yaliyoletwa na DART

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Inadaiwa Mwendokasi mpya zimefika leo kwenye roro.

Je, zitadumu?

mwendokasi_mpya1.jpg

mwendokasi_mpya2.jpg

Mwendokasi_mpya4.jpg
 
Tunachokijua
Mei 25, 2024, baadhi ya akaunti kwenye mitandao ya Kijamii kwa nyakati tofauti zilichapisha taarifa inayodai kuwa Serikali imeingiza nchini mabasi mapya yaendayo haraka, maarufu kama mwendokasi. Baadhi ya akaunti hizo ni hii, hii na hii.

Pamoja na mambo mengine, taarifa hii inadai mabasi haya yameletwa ili kuondoa changamoto ya usafiri jijini Dar es salaam.

Ukweli wake upoje?
JamiiCheck imezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), William Gatambi aliyekanusha taarifa hizo.

"Inawezekana labda yanasafirishwa kwenda nchi nyingine, sisi hatuna taarifa hayo mabasi kama ni ya kwetu, tumeona picha zikisambaa Mtandaoni lakini hatuna taarifa rasmi juu ya Mabasi hayo" amesema Gatambi.

Aidha, Taarifa za ukakika kutoka vyanzo vya Bandarini ambazo JamiiCheck imezipata ni kuwa mabasi hayo yalikuwa safarini kuelekea Nchi nyingine na yalishushwa hapo ikiwa wakati wa mchakato wa kushusha mizingo mingine kisha yakarejeshwa ndani ya meli husika.

Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa mujibu wa tangazo la serikali No. 120 la tarehe 25 Mei 2007 chini ya sheria No. 30 ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997 na marekebisho yake.
View attachment 3027985
View attachment 3028003
Kama kweli haya Mabasi yaliyopo bandarini ni mali ya UDART,

Basi miongoni mwakazi muhimu za PPP itakuwa ni haya magari mapya ambayo ni full AC wale wakupanda na samaki kutoka Feri mjitafakari.

Tayari yameingia zaidi 80 wakati mengine zaidi 100 yako njiani,

Kwa mara ya kwanza Tanzania tunaanza kuona faida za PPP-Cetre kama kweli haya ni Mabasi yetu.

Kwamambo mazuri kama haya tunamwachaje Samia 2025?​
Hii taarifa wameshasema ni ya kupotosha na wewe unazidi kuchochea uongo
 
Hao wanao panda na samaki waangaliwe
Watokaje ferry na Samaki? Kiwandani ukiagiza gari unatoa specs zote unazohitaji, ni ujinga kuagiza mzigo huku unajua kabisa kuna hitaji la wenye mzigo kama samaki na vyakula vingine.
Mbona wazee na wasiojiweza kuna viti vyao vinekuwa reserves?
Wanafeli kabla ya kuanza.
 
Hoja murua sana hii
 
Nashauri Mwendo Kasi ibinafsishwe. Kwa mtindo huu bado kutakuwa na changamoto.
 
View attachment 3027985
View attachment 3028003
Kama kweli haya Mabasi yaliyopo bandarini ni mali ya UDART,

Basi miongoni mwakazi muhimu za PPP itakuwa ni haya magari mapya ambayo ni full AC wale wakupanda na samaki kutoka Feri mjitafakari.

Tetesi ni kwamba tayari bandarini yameingia Mabasi zaidi 80 Je, ni yetu?

Kwa mara ya kwanza Tanzania tutaanza kuona faida za PPP-Cetre kama kweli haya Mabasi yatakuwa ni mali yetu.

Kama Mabasi haya si yetu basi PPP wachukue mfano huu wa Mabasi kwani unavutia sana.

Tanzania, kama ni kweli Mabasi haya ni yetu au yale yetu yaliyoko njiani na kwa mambo mazuri kama haya ya bandari yetu tunamwachaje Rais Samia 2025?​
Bandari yetu inafanya kazi nzuri sana
 
Kwan pesa anatoa ktk mfuko wake huyo mama Samia? Pesa zinatoka kwa wanachi wenyewee. Lol
Kuna watu walichukua Hela zetu kuhonga wapinzani na kuua watanzania wenzetu. Mama ameonyesha njia.
 
View attachment 3027985
View attachment 3028003
Kama kweli haya Mabasi yaliyopo bandarini ni mali ya UDART,

Basi miongoni mwakazi muhimu za PPP itakuwa ni haya magari mapya ambayo ni full AC wale wakupanda na samaki kutoka Feri mjitafakari.

Tetesi ni kwamba tayari bandarini yameingia Mabasi zaidi 80 Je, ni yetu?

Kwa mara ya kwanza Tanzania tutaanza kuona faida za PPP-Cetre kama kweli haya Mabasi yatakuwa ni mali yetu.

Kama Mabasi haya si yetu basi PPP wachukue mfano huu wa Mabasi kwani unavutia sana.

Tanzania, kama ni kweli Mabasi haya ni yetu au yale yetu yaliyoko njiani na kwa mambo mazuri kama haya ya bandari yetu tunamwachaje Rais Samia 2025?​
Nimepita mtandao fulani hivi habari ya haya mabasi kumilikiwa na udart zimekanushwa.
 
Back
Top Bottom