Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu je ukikuta gari showroom mileage inasoma 162,310. Je hii si inamaanisha imesha tembea sana na pengine ishaanza kuchoka? Au ikoje hapo!Hilo linafanyika sana! Lakini mileage nyingi sio issue as long as gari limehudumiwa vizuri! Wengi wanauziwa magari mabovu kwa kuangalia low mileage,kuna vitu vingi vya kuangalia zaidi ya odometer readings.
Nenda na fundi wako aikague. Inaweza kuwa high mileage lakini well maintained. Nina gari sasa hivi ina 218,000km na iko vizuri inaenda popote muda wowote.Mkuu je ukikuta gari showroom mileage inasoma 162,310. Je hii si inamaanisha imesha tembea sana na pengine ishaanza kuchoka? Au ikoje hapo!
Nashukuru mkuu kwa majibu. Wiki mbili zilizopita nilitembelea showroom 1 nikakuta aina ya gari niliyokuwa naihitaji ina km. 162,310. Nikadhani huu ushakuwa mkweche. Ila mmiliki wa yard aliniambia yeye hana tabia ya kushusha kilomita. Zipo kama alivyoiagiza toka japan.Nenda na fundi wako aikague. Inaweza kuwa high mileage lakini well maintained. Nina gari sasa hivi ina 218,000km na iko vizuri inaenda popote muda wowote.
Wauzaji wanashusha kms kwasababu wanajua akili ya wateja wakiona few kms wanajua ni gari nzuri and vice versa.
Sio lazima iwe imegongwa. Quality ya rangi aliyopiga huwezi kuijua. Unaweza kushangaa baada ya mwezi linafubaa,rangi inapauka au inakauka na kukatikakatika.Prondo hapo kwenye rangi mmh, mm niliponunua gari miaka kadhaa toka Jpn niliona lina little scratch nikaona aaghr nipige rangi lote. Rangi ilikua ni zellallic black, ilinigharim karibu 1.3m. Sio kila mpiga rangi anakua amegongwa
GoodBaada ya kusikia watu wengi 'wakiumizwa' na 'kupigwa' wakiwa kwenye harakati za kutafuta usafiri uliotumika nchini, nimeona sio mbaya nikitoa ushauri ni jinsi gani unaweza kuepuka majanga kwenye zoezi hilo.
Naandika kama mnunuzi au muuzaji wa aina hio ya magari, kwahio siegemei upande wowote na ninachokiandika hapa sio sheria naweza kuwa sahihi au nisiwe sahihi ila ni imani yangu lipo litakalosaidia baadhi ya watu.
Njia muhimu za kufuata ili kupata gari unalotaka ni kama ifuatavyo:
1.Fanya utafiti mdogo juu ya gari unayoitaka: Uliza ujue gari unayoitaka inauzwa kiasi gani[makadirio]. Ukiweza kujua bei ya showroom au ukiagiza mwenyewe Japan halafu linganisha na bei utakayopewa hapa. Hili ni muhimu kwa sababu nimeshuhudia watu wananunua magari yaliyotumika Tanzania kwa bei ambayo ukiagiza mwenyewe unalipata kutoka japan au ukiongeza kidogo tu unapata la showroom.
2.Usiwe na haraka: Usiwe na haraka kabisa kwenye kutafuta gari. Utaletewa kila aina ya gari na usipokuwa makini utanunua gari bovu. Angalia taratibu angalau magari matano tofauti kwenye chaguo lako ndipo uamue, madalali watakusumbua ili mradi tu wapate cha juu.
3.Epuka madalali: Kama unaweza epuka madalali. Tafuta gari kwa kuuliza watu ulio karibu nao, ndugu jamaa na marafiki au unaofanya nao kazi au biashara. Hii ni nzuri chochote kikitokea una pa kuanzia. Madalali wengi hawajali maslahi yako wala ya muuzaji cha muhimu kwao ni cha juu tu. Gari ya 4m dalali atakuuzia 5-6m.
4.Tafuta Fundi: Ukilipenda gari lolote tafuta fundi akusaidie kulikagua,hata kama una idea na magari kuna vitu hutaviona ila fundi atakusaidia. Kuwa makini kuna mafundi huwa wanabonyezwa wakufiche hitilafu halafu baadae wanarudi kupewa chao ukishauziwa kanyaboya.
5.Epuka gari iliopigwa rangi: Epuka gari iliopigwa rangi siku chache kabla ya kuwekwa sokoni, wazoefu wanajua gari za aina hio ndio umuhimu wa fundi unapokuja. Gari inaweza kuwa imegongwa hivyo imenyooshwa na wanakuzuga kwa rangi inayong'aa. Siku hizi rangi hata 200,000 unapiga gari nzima ila ukinunua hilo baada ya mwezi rangi inababuka yote.
6.Epuka gari iliooshwa engine:Ukikagua gari ukiona imeoshwa engine ogopa sana. Mara nyingi gari zinaoshwa engine kuficha 'leakage',yaani oil na vitu vingine vinavyovuja kutoka sehemu mbalimbali za engine.
7.Jaribu gari wewe mwenyewe: Ni muhimu kuendesha na kuijaribu gari wewe mwenyewe hata ukienda na fundi. Ipitishe njia mbovu usikie jinsi ilivyo chini,chochote kinachogonga kuwa makini,usisikilize ukiambiwa ni tatizo dogo, kwanini hakurekebisha. Ingawa yapo matatizo madogomadogo ila kuwa makini.
8.Usiangalie Namba: Usibabaishwe na namba, eti hii C, D etc. Kuna gari namba A ziko vizuri kuliko namba C. Muhimu ni hali ya gari husika kwa muda huo.
9.Nenda TRA kujiridhisha: Ni muhimu kujua ukweli na status ya gari na mwenye gari. Jiridhishe anaekuuzia ndio mwenye gari. Akuonyeshe nyaraka zote halisi hata za kodi aliolipia.
10.Mwisho kabisa ukilipenda gari fanyeni makabidhiano kwa kuandikishana kwa mwanasheria. Ukiweza lipia benki na ubaki na risiti kama ushahidi wa malipo kupitia akaunti yake. Epuka kubeba cash kumpelekea muuzaji mahali alipo.
Haya machache naamini yanaweza kuwa msaada kwa watu wanaonunua magari yaliyotumika nchini,wengine mnaweza kuongezea mawili matatu na kurekebisha nilipokosea.
Mkuu nahitaji Gari iliotumika hapa Tanzania kwa Mtu...sio yard.Karibu tuwasiliane kuhusu kuagiza magari japan, dubai na S.A.
Vilevile ukihitaji gari second hand ya Tanzania hapa
Mkuu Brondo ninahitaji gari aina yaSio lazima iwe imegongwa. Quality ya rangi aliyopiga huwezi kuijua. Unaweza kushangaa baada ya mwezi linafubaa,rangi inapauka au inakauka na kukatikakatika.
Bajeti yako naona nyembamba kidogo hio ni bei ya gx100 mkuu.Mkuu Brondo ninahitaji gari aina ya
Toyota Runx,Passo,Funcargo nina 4m Mkuu
sio yard,kwa mtu unaemjua hapa Tanzania,Then taratibu za manunuzi zote tunafuata..katika kujiridhisha.
AM VERY SERIOUS ON THIS KAKA....
Nitaongeza hata 1 iwe 5m Mkuu.Bajeti yako naona nyembamba kidogo hio ni bei ya gx100 mkuu.
Nakapendaga xana kastarlet mkuu,hamna m2 anaweza nibadilishaMi breki ya kwanza ilikuwa Bagamoyo. Mafuta niliweka Full Tank. Nimefika Bagamoyo,napata bia huku funguo za gari nazichezea mezani. Kurudi nikajaza tena Full Tank ndo nikapaki. Gari mpya kwanza kumiliki nani kakudanganya inapakiwa bila wese la kutosha?? Afu kabla hujapaki shurti ulifutefute lisije kulala na mivumbi...... Mkwala wote huo gari yenyewe Toyota Starlet. Utanitaka....:smile-big::smile-big::smile-big:
Niungeni na mimi 0785290580Jaman kwa nn kusiwepo na grup watsapp hvyo vyote vfanyike humo n km lipo naomba admn wa grup naomba mniadd
unawapataje haoKuna mdau fulani anahusika sana na magari aliniambia kama unataka gari ya kununua hapa bongo bora ununue kwa wahindi au waarabu wa kkoo. Wale jamaa wanatunza sana magari yao halafu pia hayapati dhoruba sana kama haya mengine. Utakuta gari inazunguka hapohapo kkoo au posta na upanga.
Na pia hao jamaa wanauza gari nzuri sana kwa bei chee kwasababu wanataka kuleta nyingine mpya zaidi.
Sijui kwakweli. Unahitaji connection nao kweli.unawapataje hao