MUONGOZO: Mambo ya kuzingatia unaponunua gari lililotumika ndani ya Tanzania

Baada ya kusikia watu wengi 'wakiumizwa' na 'kupigwa' wakiwa kwenye harakati za kutafuta usafiri uliotumika nchini, nimeona sio mbaya nikitoa ushauri ni jinsi gani unaweza kuepuka majanga kwenye zoezi hilo.

Naandika kama mnunuzi au muuzaji wa aina hio ya magari, kwahio siegemei upande wowote na ninachokiandika hapa sio sheria naweza kuwa sahihi au nisiwe sahihi ila ni imani yangu lipo litakalosaidia baadhi ya watu.

Njia muhimu za kufuata ili kupata gari unalotaka ni kama ifuatavyo:

1.Fanya utafiti mdogo juu ya gari unayoitaka: Uliza ujue gari unayoitaka inauzwa kiasi gani[makadirio]. Ukiweza kujua bei ya showroom au ukiagiza mwenyewe Japan halafu linganisha na bei utakayopewa hapa. Hili ni muhimu kwa sababu nimeshuhudia watu wananunua magari yaliyotumika Tanzania kwa bei ambayo ukiagiza mwenyewe unalipata kutoka japan au ukiongeza kidogo tu unapata la showroom.

2.Usiwe na haraka: Usiwe na haraka kabisa kwenye kutafuta gari. Utaletewa kila aina ya gari na usipokuwa makini utanunua gari bovu. Angalia taratibu angalau magari matano tofauti kwenye chaguo lako ndipo uamue, madalali watakusumbua ili mradi tu wapate cha juu.

3.Epuka madalali: Kama unaweza epuka madalali. Tafuta gari kwa kuuliza watu ulio karibu nao, ndugu jamaa na marafiki au unaofanya nao kazi au biashara. Hii ni nzuri chochote kikitokea una pa kuanzia. Madalali wengi hawajali maslahi yako wala ya muuzaji cha muhimu kwao ni cha juu tu. Gari ya 4m dalali atakuuzia 5-6m.

4.Tafuta Fundi: Ukilipenda gari lolote tafuta fundi akusaidie kulikagua,hata kama una idea na magari kuna vitu hutaviona ila fundi atakusaidia. Kuwa makini kuna mafundi huwa wanabonyezwa wakufiche hitilafu halafu baadae wanarudi kupewa chao ukishauziwa kanyaboya.

5.Epuka gari iliopigwa rangi: Epuka gari iliopigwa rangi siku chache kabla ya kuwekwa sokoni, wazoefu wanajua gari za aina hio ndio umuhimu wa fundi unapokuja. Gari inaweza kuwa imegongwa hivyo imenyooshwa na wanakuzuga kwa rangi inayong'aa. Siku hizi rangi hata 200,000 unapiga gari nzima ila ukinunua hilo baada ya mwezi rangi inababuka yote.

6.Epuka gari iliooshwa engine:Ukikagua gari ukiona imeoshwa engine ogopa sana. Mara nyingi gari zinaoshwa engine kuficha 'leakage',yaani oil na vitu vingine vinavyovuja kutoka sehemu mbalimbali za engine.

7.Jaribu gari wewe mwenyewe: Ni muhimu kuendesha na kuijaribu gari wewe mwenyewe hata ukienda na fundi. Ipitishe njia mbovu usikie jinsi ilivyo chini,chochote kinachogonga kuwa makini,usisikilize ukiambiwa ni tatizo dogo, kwanini hakurekebisha. Ingawa yapo matatizo madogomadogo ila kuwa makini.

8.Usiangalie Namba: Usibabaishwe na namba, eti hii C, D etc. Kuna gari namba A ziko vizuri kuliko namba C. Muhimu ni hali ya gari husika kwa muda huo.

9.Nenda TRA kujiridhisha: Ni muhimu kujua ukweli na status ya gari na mwenye gari. Jiridhishe anaekuuzia ndio mwenye gari. Akuonyeshe nyaraka zote halisi hata za kodi aliolipia.

10.Mwisho kabisa ukilipenda gari fanyeni makabidhiano kwa kuandikishana kwa mwanasheria. Ukiweza lipia benki na ubaki na risiti kama ushahidi wa malipo kupitia akaunti yake. Epuka kubeba cash kumpelekea muuzaji mahali alipo.

Haya machache naamini yanaweza kuwa msaada kwa watu wanaonunua magari yaliyotumika nchini,wengine mnaweza kuongezea mawili matatu na kurekebisha nilipokosea.
asante mkuu tumekuelewa!
 
Mi breki ya kwanza ilikuwa Bagamoyo. Mafuta niliweka Full Tank. Nimefika Bagamoyo,napata bia huku funguo za gari nazichezea mezani. Kurudi nikajaza tena Full Tank ndo nikapaki. Gari mpya kwanza kumiliki nani kakudanganya inapakiwa bila wese la kutosha?? Afu kabla hujapaki shurti ulifutefute lisije kulala na mivumbi...... Mkwala wote huo gari yenyewe Toyota Starlet. Utanitaka....:smile-big::smile-big::smile-big:
hahahaah ahahahaha ahahahaa safi sana mkuu ndio chako tena mwendo w kuvimba tu.
 
Sahihi kabisa ila shortcut ya documents ni TRA INVESTIGATION DEPARTMENT FLOOR NO 4 ROOM NO 1 TRA HEADQUARTERS, binafsi nina kesi inaendelea hapo ila sitaweka details zozote mpaka itakapokwisha
Kupitia kesi yangu hii nimejifunza mengi sana, ndio maana nikasema huu uzi una faida tupu kwa wale watakaosoma na kuzingatia kila mchango
Pole mshana, ngoja mimi nishehe na wanabodi kilichowahinikuta, mwaka 2004 Nilinunua Hiace Bomba tu kwa jamaa mmoja, akanipa copy ya kadi, aliniahidi kuwa atanipeleka TRA Kwenda kufuatilia kadi original, Sikuona taabu kwa kuwa mwenyewe namfahamu. Siku ya siku nikafunga mpaka TRA baada ya kuwa jamaa tunapishana pishana, kufika pale nikaambiwa kadi ya hiyo gari ipo kwenye kampuni ambayo muhusika(Alikuwa mkuu tu) ameiacha pale baada ya kukopa hiyo gari!!, aisee uelekeo ukabadilika, nikajagundua kuwa jamaa aliyeniuzia na yeye alipatishwa shida sana na mkuu yule,Nilikomaa nilikuja kuipata kwa shiida, baada ya mwaka.
 
Kuna mdau fulani anahusika sana na magari aliniambia kama unataka gari ya kununua hapa bongo bora ununue kwa wahindi au waarabu wa kkoo. Wale jamaa wanatunza sana magari yao halafu pia hayapati dhoruba sana kama haya mengine. Utakuta gari inazunguka hapohapo kkoo au posta na upanga.

Na pia hao jamaa wanauza gari nzuri sana kwa bei chee kwasababu wanataka kuleta nyingine mpya zaidi.
Hata hao wa kidongo chekundu wanachukua kwa wahindi na waarabu kwa bei ndogo alafu wanakuuzia ww
 
Wakuu, heshima kubwa kwenu!!

Ninataka kununua gari kwa mtu ambaye tumekutana nae www.kupatana.com , ni mambo gani ninapaswa kuyazingatia ili nisije kuvalishwa mkenge kwa kuuziwa gari la wizi?
 
Mimi ushauri wangu usinunue gari,speeding fines,hela ya kusafishia viatu vya traffic,parking fees zinazoongezeka kila kukicha,nk.
 
Nadhani ukimalizana na TRA,kuna haja ya kutafuta mtu wa karibu mwenye uzoefu wa magari ili akague gari,usichukue hawa mafundi njaa,atapewa hongo na kukukanyagisha mkangafu..
 
Huo mtandao wamejaa matapeli, utakuja kulia kilio cha mbwa mwizi. Shauri yako
 
Gari ipo toyota wish imesimama bei resornable kabisa hakuna kuporojoa 'best deal ever'
 
RRONDO mkuu naomba unisaidie Nataka kuagiza Mitsubishi airtrek ,unaizungumziaje hii gari sina utaalam nayo ,ahsante
 
Mi breki ya kwanza ilikuwa Bagamoyo. Mafuta niliweka Full Tank. Nimefika Bagamoyo,napata bia huku funguo za gari nazichezea mezani. Kurudi nikajaza tena Full Tank ndo nikapaki. Gari mpya kwanza kumiliki nani kakudanganya inapakiwa bila wese la kutosha?? Afu kabla hujapaki shurti ulifutefute lisije kulala na mivumbi...... Mkwala wote huo gari yenyewe Toyota Starlet. Utanitaka....:smile-big::smile-big::smile-big:
hahhahahaha mpaka unaona hapakuchi siku hiyo.
 
usha
Baada ya kusikia watu wengi 'wakiumizwa' na 'kupigwa' wakiwa kwenye harakati za kutafuta usafiri uliotumika nchini, nimeona sio mbaya nikitoa ushauri ni jinsi gani unaweza kuepuka majanga kwenye zoezi hilo.

Naandika kama mnunuzi au muuzaji wa aina hio ya magari, kwahio siegemei upande wowote na ninachokiandika hapa sio sheria naweza kuwa sahihi au nisiwe sahihi ila ni imani yangu lipo litakalosaidia baadhi ya watu.

Njia muhimu za kufuata ili kupata gari unalotaka ni kama ifuatavyo:

1.Fanya utafiti mdogo juu ya gari unayoitaka: Uliza ujue gari unayoitaka inauzwa kiasi gani[makadirio]. Ukiweza kujua bei ya showroom au ukiagiza mwenyewe Japan halafu linganisha na bei utakayopewa hapa. Hili ni muhimu kwa sababu nimeshuhudia watu wananunua magari yaliyotumika Tanzania kwa bei ambayo ukiagiza mwenyewe unalipata kutoka japan au ukiongeza kidogo tu unapata la showroom.

2.Usiwe na haraka: Usiwe na haraka kabisa kwenye kutafuta gari. Utaletewa kila aina ya gari na usipokuwa makini utanunua gari bovu. Angalia taratibu angalau magari matano tofauti kwenye chaguo lako ndipo uamue, madalali watakusumbua ili mradi tu wapate cha juu.

3.Epuka madalali: Kama unaweza epuka madalali. Tafuta gari kwa kuuliza watu ulio karibu nao, ndugu jamaa na marafiki au unaofanya nao kazi au biashara. Hii ni nzuri chochote kikitokea una pa kuanzia. Madalali wengi hawajali maslahi yako wala ya muuzaji cha muhimu kwao ni cha juu tu. Gari ya 4m dalali atakuuzia 5-6m.

4.Tafuta Fundi: Ukilipenda gari lolote tafuta fundi akusaidie kulikagua,hata kama una idea na magari kuna vitu hutaviona ila fundi atakusaidia. Kuwa makini kuna mafundi huwa wanabonyezwa wakufiche hitilafu halafu baadae wanarudi kupewa chao ukishauziwa kanyaboya.

5.Epuka gari iliopigwa rangi: Epuka gari iliopigwa rangi siku chache kabla ya kuwekwa sokoni, wazoefu wanajua gari za aina hio ndio umuhimu wa fundi unapokuja. Gari inaweza kuwa imegongwa hivyo imenyooshwa na wanakuzuga kwa rangi inayong'aa. Siku hizi rangi hata 200,000 unapiga gari nzima ila ukinunua hilo baada ya mwezi rangi inababuka yote.

6.Epuka gari iliooshwa engine:Ukikagua gari ukiona imeoshwa engine ogopa sana. Mara nyingi gari zinaoshwa engine kuficha 'leakage',yaani oil na vitu vingine vinavyovuja kutoka sehemu mbalimbali za engine.

7.Jaribu gari wewe mwenyewe: Ni muhimu kuendesha na kuijaribu gari wewe mwenyewe hata ukienda na fundi. Ipitishe njia mbovu usikie jinsi ilivyo chini,chochote kinachogonga kuwa makini,usisikilize ukiambiwa ni tatizo dogo, kwanini hakurekebisha. Ingawa yapo matatizo madogomadogo ila kuwa makini.

8.Usiangalie Namba: Usibabaishwe na namba, eti hii C, D etc. Kuna gari namba A ziko vizuri kuliko namba C. Muhimu ni hali ya gari husika kwa muda huo.

9.Nenda TRA kujiridhisha: Ni muhimu kujua ukweli na status ya gari na mwenye gari. Jiridhishe anaekuuzia ndio mwenye gari. Akuonyeshe nyaraka zote halisi hata za kodi aliolipia.

10.Mwisho kabisa ukilipenda gari fanyeni makabidhiano kwa kuandikishana kwa mwanasheria. Ukiweza lipia benki na ubaki na risiti kama ushahidi wa malipo kupitia akaunti yake. Epuka kubeba cash kumpelekea muuzaji mahali alipo.

Haya machache naamini yanaweza kuwa msaada kwa watu wanaonunua magari yaliyotumika nchini,wengine mnaweza kuongezea mawili matatu na kurekebisha nilipokosea.
ushauri mzuri sana kwa wengine ambao tuna ndoto siku moja kununa gari hapa nimepata pa kuanzia .asante sana mkuu
 
Nina bajeti ya 4m nataka Suzuki carry, Prondo vipi siwezi kupata?
 
Hili ni darasa zuri sana, nashukuru.
 
Back
Top Bottom