Allen Puntermkuu
Member
- Aug 23, 2023
- 5
- 8
Ina maana hii gharama inakuwa na makato ya kuagizia unapoipokea au hiyo ni bei yake yenyewe tu ? Mlolongo wake upo vipi mpaka umeipata labda imechukua muda gani?84,000/=
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ina maana hii gharama inakuwa na makato ya kuagizia unapoipokea au hiyo ni bei yake yenyewe tu ? Mlolongo wake upo vipi mpaka umeipata labda imechukua muda gani?84,000/=
Ndio inawezekana bila shida,Chief-Mkwawa Nimenunua SATA SSD nikaweka kwenye pc yangu sasa katika kuweka nimeona kuna slot ya kuweka NVMe. Je' naweza kuiongeza nayenyewe? Yaan ziwe zote kwa pamoja Sata SSD na NVMe?
Kwa windows mkuu uweke windows za zamani ama vyema uweke Linux Nyepesi, utafanya kazi za kawaida kama kubrowse, kucheki movies, simple video/image editing etc.Intel(R) Core(TM)2 CPU T5500 @1.66GHz
Hii vp, naweza kupiga kazi zipi?
Hii ni gharama hadi ya kusafirisha, kwanza kusafirisha AliExpress ni bure kabisa hasa hizo SSD.Ina maana hii gharama inakuwa na makato ya kuagizia unapoipokea au hiyo ni bei yake yenyewe tu ? Mlolongo wake upo vipi mpaka umeipata labda imechukua muda gani?
Boss kwemaa aise samahaniComputer nyingi tunazonunua huwa zinatumia processor za intel au amd, lakini ni intel ambaye ametawala sana kushinda amd kwenye computer zetu. Leo nimeamua niandike uzi huu kuhusu hizi processor za intel na namna ya kuzichagua ili kuwasaidia watu wanapotaka kununua laptop/desktop mpya wafanye maamuzi sahihi.
Processor ni nini?
Labda utakuwa unajiuliza kwa nini ukitaka kununua laptop mpya unatakiwa uangalie processor? Nini cha muhimu kuhusu hii processor?
-Kwa lugha rahisi processor ni kifaa ndani ya computer yako kinachobeba maagizo ya program za computer. Maagizo hayo yanaweza kuwa ya kimahesabu, kimantiki, maagizo yanayoingia kwenye computer na yanayotoka.
-jinsi processor inavyokuwa na speed kubwa ndio jinsi maagizo yatakavyofanywa haraka na ndio jinsi program za computer zitakavyofanya kazi upesi.
![]()
Familia ya processor za intel
Intel wana processor za aina nyingi na ni ngumu kuzitaja kwa pamoja, ila wameturahisishia kwa kuzipanga processor zao kwenye familia. Na hii ndio familia yao.
1. Atom processor- processor hizi hutumika kwenye vimini laptop na tablet ni ndogo kiumbo ndio maana hata vifaa vyake ni vidogo, processor hizi hazina nguvu sana na vifaa vyake hukaa sana na chaji.
2. Celeron processor- Haina tofauti sana na atom ila hii ina afadhali kidogo. Inatumika kwenye vifaa vikubwa kuliko atom kama vile laptop kubwa na desktop
3. Pentium- hii ina speed kuliko celeron na atom pia inatumika kwenye vifaa vikubwa.
4. Core 2 duo- hii ni maarufu kwa perfomance yake ya multitasking, inauwezo wakufanya mambo mengi kwa wakati mmoja ila nyingi ni za kizamani.
5. Core i3- hii ni processor latest za intel ni dual core lakini core zake zina perfomance kubwa na pia inakuwa na thread 2 kwenye kila core, ni nzuri kwa wanaotaka perfomance kubwa kwa bei rahisi.
6. Core i5- ya laptop ni dualcore na ya desktop ni quadcore isiyokuwa na thread, software nyingi kubwa duniani zimekuwa optimized kutumia core kama za i5, ni nzuri sana kwa watu wanaotumia software zinazodemand perfomance lakini hawafanyi multitasking.
7.Core i7- hii inakuwa na quadcore processor na thread 8 kwenye desktop na pia inaweza kuwa dualcore kwenye laptop. Hii ndio processor nzuri zaidi kwa watu wa kawaida na inafanya multitasking hata kama software zinademand sana.
8. Xeon- hii ndio processor yenye speed zaidi kwenye processor za intel lakini imekuwa designed kufanya kazi kwenye computer kubwa kama vile server. Unapohost website processor kama hii ndio inayoprocess webpages.
Generation ya processor(muhimu)
Ni muhimu sana kujua processor inatokea generation ipi kuna processor zenye i7 ya 2010 ambazo zipo slow vibaya mno, na pia kuna uwezekano i3 kuipita i7 kwenye perfomance kama zinatoka generation tofauti. Hivyo eneo hili inabidi uwe makini kuepuka kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hivyo unaponunua laptop/desktop ni lazima ujue ipo generation gani la sivyo upo hatarini na hivi ndio namna ya kujua.
- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu nne ni fourth generation(4xxx)
Mfano Intel i3-4130.
- Processor yenye namba inayoanziwa na elfu tatu ni third generation (3xxx)
Mfano i3-3130.
- Processor inayoanziwa na elfu mbili ni second generation(2xxx)
Mfano i3-2140
Sishauri kabisa kununua processor ya first generation, mtu unatakiwa atleast ununue ya second generation na pia bei inatakiwa iwe ndogo kwa hii second compare na third/fourth.
Processor ndogo kama atom na celeron zina generation zake ambazo ni
-clover trail
-bay trail
Processor za zamani za atom zilikuwa mbaya sana na zipo slow ila baytrail ikaja kuzipa nguvu na kuzifanya ziwe na perfomance kubwa, hivyo kama unataka kifaa cha atom/celeron make sure processor yake iwe inatoka generation ya baytrail.
Herufi za mbele ya processor(muhimu)
Kama umechunguza mbele ya processor kunakuwa na herufi mbali mbali hizi pia ni muhimu sana kuzijua kwani usipozizingatia unaweza kujuta.
Mfano processor inaweza kuitwa i5-4000m au i5-4000u au i5-4000y je nini kinatofautisha hizi processor?
1. Herufi kwenye processor za desktop.
Bila herufi – hii inakuwa na speed halisi ya processor mfano i7-4770
K- herufi hii inamaanisha processor ipo unlocked na unaweza kui over clock na kuongeza speeed. Processor yenye 3.5ghz unaweza kui overclock ikafika 4ghz. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770K. ni nzuri sana kwa wanaocheza magame na kufanya rendering.
R- herufi hii inamaanisha processor hii ni ndogo sana na inaweza kutumika kwenye videsktop vyenye umbo dogo hali ya kuwa ina graphic kubwa kama iris pro. Jina lake linakuwa mfumo huu i7-4770R hii ni nzuri kwa wale wenye ofisi ambazo ni safi hawataki mawaya mengi na desktop kubwa kukaa kwenye meza. angalia picha hapo chini uone desktop ndogo.
![]()
S- herufi hii inamaanisha hiyo proceesor wame optimize perfomance mara nyingi wanai underclock kuzuia processor kupata joto sana. Mfano i7-4770 ina 3.4ghz lakini i7-4770S ina 3.1ghz tu, ina maana hapa wamepunguza 300mhz kutoka stock kuja S.
T- herufi hii inamaanisha processor inatumia power ndogo, kwa wale wenzangu wanaotumia luku kama unataka desktop isiokula umeme basi hii ndio yenyewe ila perfomance nayo itapungua kidogo. Mfano wa jina ni i7-4770T
2. Herufi mbele ya processor za laptop(mobile)
Tumeshaona herufi mbele ya desktop, sasa hivi tuangalie herufi mbele ya processor za laptop ambazo pia zinaweza kutumika kwenye home theatre pc (htpc) au wengine wanaita mini desktop.
M- herufi hii inamaanisha hio processor ni mobile, ndio herufi common kwenye processor za laptop mfano i5-4000M
U- herufi hii inamaanisha processor ya laptop inatumia power ndogo hizi processor zinatumika sana kwenye vilaptop vyembamba (ultrabook). Kwa sababu zinakaa na chaji kutokana na kutumia power ndogo, perfomance yake nayo pia ni ndogo. Mfano i5 4250U
Y- hii ni ultra low power yaani inakula umeme mdogo kushinda hata U lakini vile vile perfomance inazidi kushuka nayo mfano i7-4610Y
HQ- herufi hii inamaanisha high perfomance, zinauzwa bei ghali sana na power yake inashindana na desktop. Usije ukajaribu kuieka kwenye mapaja laptop ya design hii maana zinashika moto upesi sana kutokana na quality ya processor. Ni nzuri kwa wale wanaopenda kucheza game, kutumia software kubwa wakiwa kitandani. Mfano ni i7-4700HQ
MQ- herufi hii inamaanisha hio procesor ni quad core. Kama umesoma vizuri juu i5 na i7 za desktop ni quadcore lakini za laptop ni dualcore, hivi processor hii inamaanisha unaweza tumia quadcore kwenye laptop yako kama unataka mfano i7-4900MQ
MX- herufi hii inamaanisha ni xtreme edition, processor hii unaweza kui over clock kama vile K series ya desktop na ina perfomance kubwa sanaaa, ila kuwa makini na mapaja tu.
Mfano i7-4940MX
Huu ndio muongozo wa kununua processor za intel, kama kuna sehemu hujapaelewa unaweza kuuliza nitaelezea zaidi.
Ninazo hizi hapa.Mkuu ile pc yangu ya core i3 1005g1 nimeiongezea RAM na ninajipanga niiongezee SSD ya 256, sijui inauzajwe Sata ssd mkuu.
Kwann hukuchukua M2 NVME hata kama ni 512? Maana the way unavyoona generation za ssd zinatofautiana ndo performance inatofautiana pia. Hyo speed unayosema ni kali sana kwa ssd ya sata 2.5 ukiilinganisha na speed ya NVME zimetofautiana MkuuChief-Mkwawa Nimenunua SATA SSD nikaweka kwenye pc yangu sasa katika kuweka nimeona kuna slot ya kuweka NVMe. Je' naweza kuiongeza nayenyewe? Yaan ziwe zote kwa pamoja Sata SSD na NVMe?
Ni nzuri mkuu itafanya mambo yote bila shida kasoro tasks ambazo zinataka Gpu kubwa. Gen ya 12 hio.Boss kwemaa aise samahani
Hii imekaaje kaka iko vzr?
Budget?Chief-Mkwawa Naomba unisaidie specification za both Laptop na Desktop Information kuanzia Cpu,Graohics (GPU) pamoja na Ram na information zingine ikikupendeza...
Nataka kuanza kufanya kazi za Coding (advance coding ikiwemo Large Language kama python,php na java na zingine nyingi) na hili litaaambatana na Kazi za Graphix kam video editing and rendering amd multi tasking duty...
Sasa nauliza ni computer yenye vigezo gani itafaa kwNgu kuitumia naomba nisaidie ili nikazichukue DEKSTOPS NA LAPTOPS VIJANA WANGU WAANZE KAZI
For 1 laptop nafikiri li ntahitji kuichukua kwa pesa isizidi 1.5mil na for Desktop isizidi 800kBudget?
Nimesha ambiwa na Chief-Mkwawa kuwa naweza weka NVMe na ninampango niagize 1TB, nimechukua hiyo nikwasababu pc yangu ilikuwa iiminiletea Blue Screen of Death hvyo ikabidi niagize hiyo Sata. Nataka niagize hiyo, kumbe NVMe inanguvu kuliko sata?Kwann hukuchukua M2 NVME hata kama ni 512? Maana the way unavyoona generation za ssd zinatofautiana ndo performance inatofautiana pia. Hyo speed unayosema ni kali sana kwa ssd ya sata 2.5 ukiilinganisha na speed ya NVME zimetofautiana Mkuu
Kwa desktop used gen ya 8 unapata around laki 4, hizi unapata maduka ya kawaida kariakoo, tumia kiasi kilichobaki ku upgrade ram, ssd na Gpu. Kwa issue zako Gpu angalau gtx 1050. Option uliyonayo ni gtx 1050, 1050ti, 1650ti, rtx A2000. Ila kwa budget yako ni kati ya 1050 hadi 1650 ndio uhalisia.For 1 laptop nafikiri li ntahitji kuichukua kwa pesa isizidi 1.5mil na for Desktop isizidi 800k
Sata Ssd nyingi Max ni 500MBps hizi Nvme nyingi ni 3.5GBps na zipo za kisasa hadi 12GBpsNimesha ambiwa na Chief-Mkwawa kuwa naweza weka NVMe na ninampango niagize 1TB, nimechukua hiyo nikwasababu pc yangu ilikuwa iiminiletea Blue Screen of Death hvyo ikabidi niagize hiyo Sata. Nataka niagize hiyo, kumbe NVMe inanguvu kuliko sata?
View attachment 2745840
Mkuu Generation ya 11 kwa Core yoyote Au specifally niance na coreI5 na coreI7 au ni processor yoyote ila generation ya 11Kwa desktop used gen ya 8 unapata around laki 4, hizi unapata maduka ya kawaida kariakoo, tumia kiasi kilichobaki ku upgrade ram, ssd na Gpu. Kwa issue zako Gpu angalau gtx 1050. Option uliyonayo ni gtx 1050, 1050ti, 1650ti, rtx A2000. Ila kwa budget yako ni kati ya 1050 hadi 1650 ndio uhalisia.
Changamoto hizi gpu ngumu kupata huku kwetu ni za kuagizishia, online naziona around laki 2 mpaka 3 used ebay.
Kwa laptop around 1m mpaka 1.5m unapata mtumba ambayo ina gen ya 11 kupanda amba ryzen 5000 kupanda na gpu ndogo kama Nvidia Mx 450.
Alternative kitu chepesi kama Laptop unaweza Agizishia Amazon.
Minimum i5 mkuu, kwenye laptop utofauti wa i5 na i7 ni mdogo sana.Mkuu Generation ya 11 kwa Core yoyote Au specifally niance na coreI5 na coreI7 au ni processor yoyote ila generation ya 11
Ooh thankx Sana MkuuMinimum i5 mkuu, kwenye laptop utofauti wa i5 na i7 ni mdogo sana.
Dah shukrani nilijaribu kununua hapa Laptop nilichokutana nacho huko nisaidie mkuu 🤣🤣🤣 maana kimenitoa ushamba nimeenda kwenye filter nashangaa nimeandika core i5 nikaulizwa with hiw much procesor count sasa ikanichanganya kidogo so ukitoa generation kwamfano...Minimum i5 mkuu, kwenye laptop utofauti wa i5 na i7 ni mdogo sana.