Bondpost
JF-Expert Member
- Oct 16, 2011
- 7,019
- 10,455
Labda nikusaidie kitu kwa manufaa ya uliowamislead. In short, Mufilisi ni mtu au kampuni inayosimamia ufilisi wa kampuni nyingine kusimamia Mali na madeni kabla kampuni iliyofilisiwa haijafungwa rasmi.Kampuni zote za Musiba zilishafilisika hata mishahara hawezi kulipa, na anadaiwa na watumishi wake kitambo.
Hivyo hizi amri za kulipa aliowac hafua pesa hazitekelezeki sababu kampuni zake lilishaishiwa pesa.
My take; Tusikenue meno tukadhania amepatikana kumbe hakuna chochote atakachopoteza.
Kuna aina mbili ya ufilisi moja ni wakurugenzi au directors wanafanya maamuzi (board resolution) kwa hiari (voluntary liquidation) au kwa njia ya wadai kupitia Mahakama kulazimisha kuifunga kampuni ili madeni yao walipwe ( involuntary/Court liquidation).
Hivyo basi, anayeweza kutamka kwamba kampuni fulani imefilisika ni Mahakama pekee.
Pia sio kila mtu anaweza kuwa Mufilisi, sheria ya makampuni imewataja watu wawili, either awe Wakili au Auditor na watateuliwa na Mahakama hata kama ni involuntary liquidation lazima upeleke jina la mtu mnayependekeza awe liquidator au kama ni involuntary basi walioomba hiyo liquidation watapewa kulingana na mtu aliyependekezwa na kama Mahakama itaridhika nae.
Sasa ukisema Musiba ni mifilisi naona umejichanganya lakini kama ulimaanisha amekuwa bankrupt, hiyo haina tatizo Ila ni mpaka wanaomdai wakiamua kuomba Mahakama itoe amri ya kumfilisi ili alipe hayo madeni yake na sio lazima alipe yote Ila ukiacha madeni ya kisheria ambayo kwanza ni Kodi then anajilipa Mufilisi halafu wengine ndio wanaendelea. Hapo akina Membe wakiwahi kimfilisi ndio watakuwa wamecheza bingo.
However, kama amefilisika, bado wanaweza kuamua kupeleka maombi Mahakamani kutaka musiba afungwe hela kama Civil Prisoner na hii watu wengi huwa hawajui kwamba deni linaweza kukufunga miezi sita sita mpaka utakapolipa Ila anayekuweka ndani anapaswa kukuhudumia tu. Hii situation ilimkuta Marehemu mchungaji Mtikila alikuwa anadaiwa milioni nane akawa anasumbua kulipa mdai akapeleka kesi Mtikila awekwe jela as a civil prisoner, alipoona hivyo ikabidi alipe tu maana alikuwa anataka kuleta janja janja.
So, kwa Musiba the saga is not over, wanaweza kuamua kumkomesha tu kama walitaka, naona awahi aombe radhi atafute watu wazima awalilie shida wamtafute mzee Membe na Fatma wayamalize.
Sponsor huwa anakufa jamani.