Musoma: CCM yaizawadia Shule kengele ya Kisasa

Musoma: CCM yaizawadia Shule kengele ya Kisasa

Katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi, Jumuiya ya Wazazi CCM Musoma imetoa zawadi kabambe ya Kengele ya kisasa aina ya Rimu la gari, kwa ajili ya kutumika shuleni hapo.

Wazee hao wanaamini kwamba Wanafunzi wakisikia kengele hiyo watajua Kwamba serikali imeleta Maendeleo.

View attachment 2502651
Huyo binti hataki kucheka tu hyo zawadi
 
Ili watoto wawahi shule na vipindi vienende kwa mapigo ya kengele.Yupo akay but not alright!Katisha sana.Ni mbunge wa chama gani tuichambue akili yake?😜😜😜😜😜
IMG_20230201_211628.jpg
 
Dah.. makada kama hawa wanachosha kinyama. Wangeenda hata kutoa zawadi ya miche ya miti watoto wapande... kuna wakati JK aliwakataa makada walioenda kwenye sehemu isiyowahusu kisa tu JK alikuwa hapo. WanaCCM tubadilike. Tunawapa point tatu wapinzani kizembe sana.
 
Nilikwenda Ujerumani hivi karibuni, nikatembelea kanisa fulani. Mwenyeji wangu alinitembeza humo kanisani, kitu alichojivunia sana ni kengele iliyo tundikwa kwenye mnara wa hiyo kanisa - ina uzito wa Tani moja na inapigwa na watu watatu wanao vuta kamba ndani ya chumba mahasusi kwa kazi hiyo kila jumapili asubuhi au wakati wa siku muhimu kwa kanisa hilo.
Hivyo, hiyo rimu ya Gari inafaa sana kwa ajili ya kengele ya shule - ina mlio mkali unao fika mbali. Hivyo itatoa na faida kubwa kwa wakazi wa karibu na shule, kusaidia kushiriki katika kuwawajibisha walimu na wanafunzi (mlio wa kengele ya rimu). Pongezi kwa walio liona hilo na kutoa msaada huo. Na wewe kama unayo rimu chakavu hapo nyumbani, usiipeleke kuiuuza kwa vyuma chakavu - donate it to any school. Haimalizi LUKU!

Hivi Kuna watu wanakuita baba?

Khaaa.
 
CHADEMA tangu JPM aende ni kama mmelishwa limbwata mnaacha hoja za msingi kama upinzani mnaanza mipasho.
 
Back
Top Bottom