Musoma: CCM yaizawadia Shule kengele ya Kisasa

Musoma: CCM yaizawadia Shule kengele ya Kisasa

Katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi , Jumuiya ya Wazazi CCM Musoma imetoa zawadi kabambe ya Kengele ya kisasa aina ya Rimu la gari , kwa ajili ya kutumika shuleni hapo .

Wazee hao wanaamini kwamba Wanafunzi wakisikia kengele hiyo watajua Kwamba serikali imeleta Maendeleo .

View attachment 2502651
Hahah mkuu

Hapo rim la gari ungemalizia na "CHAKAVU"
 
Hiyo shule ni yao kwa nn wasipeleke? Alaf mbona hukuripoti kuhusu hayo majengo mazuri yaliojengwa na CCM?
Tukuulize wewe unayesema kwa nini wasipeleke rimu used la Fuso hapo shule!

Kwa akili zako kwa muonekano wa hayo majengo unayoyasifia hapa hiyo rim ilistahili kuwepo hapo?tena na picha mmepiga kana kwamba mnakabidhi kitu cha maana sana,hayo mavyuma wamiliki wa malori huwa wanayaacha bure kwa waziba puncture kwenu mnaona sherehe na yupo mtu kwenye kampeni atasema ktk agenda zake alizotimiza moja wapo ni kutoa kengele ya shule na makofi mtampigia.
 
Tukuulize wewe unayesema kwa nini wasipeleke rimu used la Fuso hapo shule!

Kwa akili zako kwa muonekano wa hayo majengo unayoyasifia hapa hiyo rim ilistahili kuwepo hapo?tena na picha mmepiga kana kwamba mnakabidhi kitu cha maana sana,hayo mavyuma wamiliki wa malori huwa wanayaacha bure kwa waziba puncture kwenu mnaona sherehe.
Kwani utampangia mtu vitu au fenicha za kuweka kwenye nyumba alioijenga yeye? Hata akiweka kuu kuu nyumba si yake? Kuna shida?
 
Mimi ninawashangaa wanaoshangaa....

Kwamba Zawadi ni nini (mtu unachagua zawadi ya kupewa)

Labda kaona hakuna Kengele na nadhani Kengele hii inafanya kazi kuliko hata ya umeme ambayo baadhi ya watu wanasema angetoa (Je umeme ukikatika jambo ambalo ni la kawaida kwa hii nchi ya giza)

Ninarudia yupo sahihi ingawa sio issue ya kutangaza kila mtu ajue kama vile isivyo issue / busara kila mtu anapotoa msaada kutangazia jamii...
 
Kwani utampangia mtu vitu au fenicha za kuweka kwenye nyumba alioijenga yeye? Hata akiweka kuu kuu nyumba si yake? Kuna shida?
Halafu wewe Ahmad Abdurahman unaonekana dhahiri ni mtoto wa Kinana,una-sound kisiasa siasa sana.

Nikuulize,unadhani rim used ya Fuso inafaa kweli kuwakusanya watoto wa maskini kuja kumpigia makofi mbunge?huu ni udhalilishaji kwa nchi hayo makengele watu wameacha kutumia 19 century huko leo wapo digital wewe upo hapa unasema kwa sababu ni mali ya ccm,ndo mtujengee sifa mbaya duniani?

Grow up!!!
 
Back
Top Bottom