Musoma: Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bunda apandishwa Kortini kwa kuongoza Genge la Uhalifu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,659
Reaction score
90,151
Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bunda mkoani Mara nchini Tanzania, Karoli Mganga amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma akikabiliwa na mashtaka 178, likiwemo la kuongoza genge la uhalifu.

Mbali na padri huyo, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni aliyekuwa mhasibu wa kanisa hilo Jimbo la Bunda, Gerald Mgendigendi.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumanne Agosti 6, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Aloyce Katemana na kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Akiwasomea mashtaka hayo, Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Mara, Amoscsye Erasto amedai walitenda kosa la kughushi nyaraka, kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16, marejeo ya mwaka 2022.

Amedai washtakiwa hao wakiwa watumishi wa kanisa hilo, waliiba fedha Sh1.7 bilioni pamoja na fedha za kigeni, ikiwepo Dola zaidi ya 100,000 na Euro zaidi ya 20,000.

Amedai jumla wanakabiliwa na mashtaka 178, yakiwemo ya kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji fedha pamoja mashtaka mengine mengi.

Hata hivyo, baada ya kusomewa mashtaka hayo hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo. Kesi itatajwa tena Agosti 20, 2024 na washtakiwa wamepelekwa rumande.

Soma pia: Bukoba: Kauli ya kanisa juu ya Padri anayedaiwa kuhusika kifo cha Mtoto mwenye Ualibino.

My Take
Hawa ndio eti wanawawekea sijui mikono sijui Sakramenti Ili mpigwe vizuri 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Dini iliwaaminisha waumini kwamba hawa ni watakatifu, watu wanaosamehe na kuondoa dhambi ndio maana watu wanaenda kuungama mbele zao ila ni vibaka kama vibaka wengine. Imagine kuna watu walikua wanaenda kuungama mbele ya tapeli kama huyo wakiamini dhambi zao zimesamehewa.

Dini ni utapeli mkubwa kuwahi kutokea kwenye maisha ya binadamu hapa Duniani.
 
Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bunda mkoani Mara nchini Tanzania, Karoli Mganga amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma akikabiliwa na mashtaka 178, likiwemo la kuongoza genge la uhalifu.

Mbali na padri huyo, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni aliyekuwa mhasibu wa kanisa hilo Jimbo la Bunda, Gerald Mgendigendi.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumanne Agosti 6, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Aloyce Katemana na kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Akiwasomea mashtaka hayo, Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Mara, Amoscsye Erasto amedai walitenda kosa la kughushi nyaraka, kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16, marejeo ya mwaka 2022.

Amedai washtakiwa hao wakiwa watumishi wa kanisa hilo, waliiba fedha Sh1.7 bilioni pamoja na fedha za kigeni, ikiwepo Dola zaidi ya 100,000 na Euro zaidi ya 20,000.

Amedai jumla wanakabiliwa na mashtaka 178, yakiwemo ya kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji fedha pamoja mashtaka mengine mengi.

Hata hivyo, baada ya kusomewa mashtaka hayo hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo. Kesi itatajwa tena Agosti 20, 2024 na washtakiwa wamepelekwa rumande.

Soma pia: Bukoba: Kauli ya kanisa juu ya Padri anayedaiwa kuhusika kifo cha Mtoto mwenye Ualibino.
 
Hizo Bado ni tuhuma na kwa sababu padri wa Mahalia ni accounting officer lazima watatuhuniwa, ukizingatia fedha za parokia ndio zimepotea.
 
Waliingiwa tu na shetani.walitakiwa tu waombewe ili huyo shetani aondoke na kuwa wema.wamekosea sana kuwashitaki maana hata bibilia inasema usilipe kisasi Bali mpende jirani Yako kama unavyojipenda wewe.
 
Inasikitisha Sana.....Yaani so called watumishi wa mungu,manabii ,wachungaji etc ni Wezi na matapeli.
mbele za Mungu hakunaga kiongozi
wote tupo sawa, ni binadamu watenda dhambi, that is why wote Yesu akatufia
ni vile tu ujinga wetu tunaenda kuungama na kutubu mbele ya binadamu wenzetu
 
Back
Top Bottom