Uchaguzi 2020 Musoma: Tundu Lissu alala Butiama nyumbani kwa Mwalimu Nyerere

Hawana cha kupoteza kwani hawanamabiashara yanayohitaji kulindwa na nguvu ya kisiasa wao ni mafukara wenye utu na hawakupenda jinsi maharamia walivyomtendea Lissu na wao wanapenda Tanzania yenye kuheshimu sheria na katiba kuanzia Butiku na all entire family
 
Uko sahihi lakini nasikia 'Jamaa' ni 'Bingwa' wa 'Visasi' hata kuliko 'Mtangulizi' wake Yule wa 'Msoga' ambaye 'anakuumiza' huku 'anakuchekea' tu.
Hahahaha yule wa msoga nae alikuwaga mtata sana [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Anaweza choma sindano halafu anacheka cheka hivi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sema Jamaa alikuwa Muungwana sana aisee unless upite kwenye mitikasi yake ya ndani ndani saaana[emoji12]
 
Mama Maria alichana mkeka[emoji1787][emoji1787]
 
Iyo nyumba ni ya wote ndio maana ikaitwa nyumba ya baba wa taifa kwaiyo hata wewe unaweza kwenda kulala tu
 
ajiandae kisaikoilojia kazi ya kufanya baada ya 28 oct. 2020
 
Waligombea kura za maoni watu wa jimbo hilo wakawanyima kura Makongoro alipata kura tano mwiingine huyo madaraka alipata kura tatu naona wana hasira

Kura wakose wao hasira wazioyesheee kwa kumlaza Lisu kwao!!!!!!
Nyie vijana kwa kweli Jiwe amewaharibu akili, siasa si uadui na katika awamu zote nne hakuwahi kuwa na uadui wa kisiasa. Jiwe ana matatizo sana.
 
Huku ni kukuza Mambo. Huyo Tundu hapo yupo lodge ya mwitongo. Ni mteja ameenda kutaka huduma, aseme tu nilikala lodge ya mtoto wa mwalimu, na sio eti nyumbani KWA baba wa Taifa
 
Kwani kwa Nyerere ni kwenu? Mnawapangia wageni wa kuwakaribisha?
 
Ameenda kufanya nn wakati ali alimtukana mwl?? Au mmesahau??
 
Mgombea wa Urais wa CHADEMA amelala Nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa

Kwa heshima anayopewa Baba wa Taifa ndani ya CCM na nchi kwa Ujumla hii haina madhara kwa familia na Chama?

Kalala kwenye lodge ambayo ni biashara ya familia kwa wale wanaokwenda kutembelea maktaba na kaburi la Mwalimu, na Breakfast etc ni sehemu ya ukaribisho joy na kupiga picha etc
 
PALEMwitongo Lodge jamani
 
Na hilo jimbo la Butiama ( Zamani Musoma Vijijini ) lilikuwa na mbunge wa Upinzani kutoka NCCR, uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995.

Tena alifanyiwa kampeni na Nyerere mwenyewe.
Alikuwa ni balozi Paulo Ndobho.
 
Sidhani kama angelala angepata usingizi maana alishawahi mtukana mwenye hiyo nyumba.
 
Ukiacha picha uliyoipost hapo, zipo nyingine tatu(ambazo najua kwa maksudi hujazipost) ambapo moja inaonyesha uhalisia kwamba alipolala Lissu ni Lodge ambayo ipo jirani na maeneo alipozaliwa nyerere na yapo maneno kabisa kwa juu yanayosomeka LODGE na si nyumbani kwa nyerere

Kumezuka tabia hivi karibuni ya kuwafanya watanzania wote ni mang'ombe kwa ajili tu ya kusaka huruma, hilo halitafumbiwa macho
 
Tunajua propaganda mashine za BAVICA wameongezea chumvi na hiliki nyingi sana kwenye hii taarifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…