Mussa Zungu: Tutegemee mengi magumu yatakuja. Asema kupanda kwa bei hakujatengenezwa na Serikali

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,712
Mussa Zungu: Dunia ina matatizo makubwa, bei za bidhaa zimepanda huko zinapotengenezwa na kwakuwa zinapotengenezwa huko, zikija kwetu zinapanda vilevile.

Kwahiyo kupanda kwa bidhaa hizi sio suala la Tanzania, limetengenezwa na watanzania au limetengenezwa na Serikali ya Tanzania, ni suala ambalo limejitokeza kwa matatizo ya kiulimwengu ambayo yapo na hasa vita ya nchi hizi mbili kati ya Ukraine na Urusi.

Tutegemee mengi magumu yatakuja, kikubwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu atunusuru na adha hii, amalize vita hii na dunia na nchi yetu irudi katika hali ya kawaida.

Mimi hivi karibuni nilikuwa Ufaransa, mkate sasa hivi huruhusiwi kununua kama zamani, mwisho ni mikate miwili, mkate umepanda kutoka euro moja sasa unauzwa euro nne, mafuta ya kupikia kutoka euro 2 mpaka 8, petroli euro 1.6 mpaka 7, hiyo ni Ulaya.

Your browser is not able to display this video.
 
Kabla hata ya vita bidhaa nchii hii zilikuwa zikipanda kila kukicha,hebu tuwe serious na maisha ya watu.
 
Mpumbavu huyu walipewa pesa ya kupunguza madhila ya coronavirus wakajengea madarasa, sijui waliwaza nini. Sasa wanatupa story wakati walitwambia tozo za simu watajengea madarasa sijui wanawaza nini wanatuona hamnazo

USSR
 
Dkt Magufuli angefukuka hawa wote wangekaa pembeni. Hivi kuna sifa kweli kutangaza inflation kwenye nchi masikini?? Yaani dah inasikitisha sana
 
Huyu hachelewi kushauri tozo nyingine kama ufumbuzi.
 
Bidhaa zimepanda siku nyingi tukiongeza na ile kauli ya vitu vitapanda lazima Wafanyabiasha wapandishe kwani wamepata mamlaka ya kauli kutoka.
Kwani kauli ndo zinatuponza mpaka hapa tulipofikia
 
Mimi hivi karibuni nilikuwa Ufaransa, mkate sasa hivi huruhusiwi kununua kama zamani, mwisho ni mikate miwili, mkate umepanda kutoka euro moja sasa unauzwa euro nne, mafuta ya kupikia kutoka euro 2 mpaka 8, petroli euro 1.6 mpaka 7, hiyo ni Ulaya.
kumbe hapo ufaransa nao wanapitia kipindi kigumu kutokana na vikwazo walivyojiwekea wenyewe
 
Mpumbavu huyu walipewa pesa ya kupunguza madhila ya coronavirus wakajengea madarasa, sijui waliwaza nini. Sasa wanatupa story wakati walitwambia tozo za simu watajengea madarasa sijui wanawaza nini wanatuona hamnazo

USSR
Mtaisoma Namba mpaka Utamke RIVASI kwa KiHadzabe NABADO

CCM hoyeeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…