Mussa Zungu: Tutegemee mengi magumu yatakuja. Asema kupanda kwa bei hakujatengenezwa na Serikali

Mussa Zungu: Tutegemee mengi magumu yatakuja. Asema kupanda kwa bei hakujatengenezwa na Serikali

Mussa Zungu: Dunia ina matatizo makubwa, bei za bidhaa zimepanda huko zinapotengenezwa na kwakuwa zinapotengenezwa huko, zikija kwetu zinapanda vilevile.

Kwahiyo kupanda kwa bidhaa hizi sio suala la Tanzania, limetengenezwa na watanzania au limetengenezwa na Serikali ya Tanzania, ni suala ambalo limejitokeza kwa matatizo ya kiulimwengu ambayo yapo na hasa vita ya nchi hizi mbili kati ya Ukraine na Urusi.

Tutegemee mengi magumu yatakuja, kikubwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu atunusuru na adha hii, amalize vita hii na dunia na nchi yetu irudi katika hali ya kawaida.

Mimi hivi karibuni nilikuwa Ufaransa, mkate sasa hivi huruhusiwi kununua kama zamani, mwisho ni mikate miwili, mkate umepanda kutoka euro moja sasa unauzwa euro nne, mafuta ya kupikia kutoka euro 2 mpaka 8, petroli euro 1.6 mpaka 7, hiyo ni Ulaya.

View attachment 2182755
Ndio aina ya viongozi wanaotakiwa kuwaongoza watz, kazi yao kubwa ni kulalamika kama wananchi pasipo kuchukua hatua zozote kwa sababu wamepewa madaraka makubwa yaliyowazidi uwezo.
 
Mh huyu ndiye aliyekuja na ubunifu wa tozo. Aje sasa na ubunifu wa kuishauri serikali ifanye nini kupunguza makali ya kupanda kwa bei za bidhaa muhimu yanayo ongeza ugumu wa .maisha kwa wananchi.

Mlala hoi wa ufarasa huku Tanzania ni mtu wa middle class. So kulinganisha madhara ya kupanda gharama za maisha ya kila siku Ufaransa/Ulaya na hapa Tanzania sio sawa. Wananchi wanataka kuona hatua zinazo chukuliwa kukabiliana na hali hii.
 
Kama Naibu Spika anaishauri Serikali ifanye nini kutupunguzia sisi wananchi makali haya ya maisha!!!
 
Kabla hata ya vita bidhaa nchii hii zilikuwa zikipanda kila kukicha,hebu tuwe serious na maisha ya watu.
Hao viongozi wenu bila kumshughulikia mmoja baada ya mwingine wataendelea kuwachezea sana akili na hisia zenu.
 
Dkt Magufuli angefukuka hawa wote wangekaa pembeni. Hivi kuna sifa kweli kutangaza inflation kwenye nchi masikini?? Yaani dah inasikitisha sana
Sijaangalia video , sijui hata kama ametoa neno kuhusu Serikali iige nchi nyingine kwa kupunguza matozo ili bei ziwe afadhali kidogo kwa wananchi wao.
 
Angetuambia,serikali wana mikakati gani kupunguza makali kwenye situation hii

Ova
 
Mpumbavu huyu walipewa pesa ya kupunguza madhila ya coronavirus wakajengea madarasa, sijui waliwaza nini. Sasa wanatupa story wakati walitwambia tozo za simu watajengea madarasa sijui wanawaza nini wanatuona hamnazo

USSR
Jiwe alipochukua misaada ya tetemeko Kagera aliifanyia nini?
 
Back
Top Bottom