Mussa Zungu: Tutegemee mengi magumu yatakuja. Asema kupanda kwa bei hakujatengenezwa na Serikali

Itakua hujaona taifa masikini sana
Hoja kuu hapa siyo masikini sana vs masikini kidogo bali hoja kuu hapa ni kwamba anaebeba lawama kwa Taifa kuwa masikini hadi kushindwa kutoa ruzuku kipindi hiki cha mdhororo wa uchumi ni CCM.
 
Nchi tutaikomboa kwa maandamano tu na si vinginevyo CCM hii haijawah badilika toka aondoke Mwl .Nyerere,tumebakia na watu ambao hawajali kitu chochote wamebaki wanafanya biashara na kupiga deal Basi hakuna kingine,watanzania wengi kwao ni kama mbwa tu.
 
Kazi yake ni kusema serikali inachukua hatua gani sio hayo mengine
 
Mussa Zungu: Dunia ina matatizo makubwa, bei za bidhaa zimepanda huko zinapotengenezwa na kwakuwa zinapotengenezwa huko, zikija kwetu zinapanda vilevile.

Kwahiyo kupanda kwa bidhaa hizi sio suala la Tanzania, limetengenezwa na watanzania au limetengenezwa na Serikali ya Tanzania, ni suala ambalo limejitokeza kwa matatizo ya kiulimwengu ambayo yapo na hasa vita ya nchi hizi mbili kati ya Ukraine na Urusi.

Tutegemee mengi magumu yatakuja, kikubwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu atunusuru na adha hii, amalize vita hii na dunia na nchi yetu irudi katika hali ya kawaida.

Mimi hivi karibuni nilikuwa Ufaransa, mkate sasa hivi huruhusiwi kununua kama zamani, mwisho ni mikate miwili, mkate umepanda kutoka euro moja sasa unauzwa euro nne, mafuta ya kupikia kutoka euro 2 mpaka 8, petroli euro 1.6 mpaka 7, hiyo ni Ulaya.

View attachment 2182755
Huyu ni fisadi miongo na muuza madawa ya kulevya, Ufaransa alikuwa ananunua mafuta ya kupikia akapikie wapi. Uongo umekuwa ugonjwa sugu kwa viongozi wetu
 
Viongozi was kitanzania kila saa visingizio tu, shida Sana nchi haisongi tuna watu wa ajabu sana
 
Mussa Zungu: Dunia ina matatizo makubwa, bei za bidhaa zimepanda huko zinapotengenezwa na kwakuwa zinapotengenezwa huko, zikija kwetu zinapanda vilevile.

Kwahiyo kupanda kwa bidhaa hizi sio suala la Tanzania, limetengenezwa na watanzania au limetengenezwa na Serikali ya Tanzania, ni suala ambalo limejitokeza kwa matatizo ya kiulimwengu ambayo yapo na hasa vita ya nchi hizi mbili kati ya Ukraine na Urusi.

Tutegemee mengi magumu yatakuja, kikubwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu atunusuru na adha hii, amalize vita hii na dunia na nchi yetu irudi katika hali ya kawaida.

Mimi hivi karibuni nilikuwa Ufaransa, mkate sasa hivi huruhusiwi kununua kama zamani, mwisho ni mikate miwili, mkate umepanda kutoka euro moja sasa unauzwa euro nne, mafuta ya kupikia kutoka euro 2 mpaka 8, petroli euro 1.6 mpaka 7, hiyo ni Ulaya.

View attachment 2182755
Kwa hiyo huku kwetu viazi vitamu, magimbi, viazi mviringo nk navyo vikipanda bei mtasingizia vita?? Mfano mafuta ya alizeti bei ilikuwa mbaya hata kabla ya vita je nayo tuzingizie vita?? Haya tuje kwenye petrol na diesel kabla ya vita kuanza bado kodi/tozo kwenye mafuta zilikuwa kibao kiasi kwamba majirani zetu Zambia wanaotoa mafuta bandarini kwetu bei yao iko chini kuliko sisi kwa zaidi ya sh 500!!! Je bado tuzingizie vita? Kama alivyoshauri mbunge Shabiby badilisheni utaratibu wa kuagiza mafuta nje, badala ya kutumia mfumo wa bulb procurement peke yake kampuni binafsi/watu binafsi pia waruhusiwe ili kuwe na ushindani utakopunguza bei.
 
Daah.

Viongozi wetu wamegeuka wanajimu.

Badala ya kutatua changamoto

Wanabakia kupiga ramli.

Haya ndio matatizo ya kurudia watu wale wale miaka yote.

Hawawezi kuwa na jipya.
 
Mussa Zungu: Dunia ina matatizo makubwa, bei za bidhaa zimepanda huko zinapotengenezwa na kwakuwa zinapotengenezwa huko, zikija kwetu zinapanda vilevile.

Kwahiyo kupanda kwa bidhaa hizi sio suala la Tanzania, limetengenezwa na watanzania au limetengenezwa na Serikali ya Tanzania, ni suala ambalo limejitokeza kwa matatizo ya kiulimwengu ambayo yapo na hasa vita ya nchi hizi mbili kati ya Ukraine na Urusi.

Tutegemee mengi magumu yatakuja, kikubwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu atunusuru na adha hii, amalize vita hii na dunia na nchi yetu irudi katika hali ya kawaida.

Mimi hivi karibuni nilikuwa Ufaransa, mkate sasa hivi huruhusiwi kununua kama zamani, mwisho ni mikate miwili, mkate umepanda kutoka euro moja sasa unauzwa euro nne, mafuta ya kupikia kutoka euro 2 mpaka 8, petroli euro 1.6 mpaka 7, hiyo ni Ulaya.

View attachment 2182755
Hayo mafuta ni kwa Lita ngapi? Kama ni kwa Lita moja hapo katuingiza chaka.
 
SASA hivi tukilalamika tunapewa tu reference ya nchi za wenzetu,mara mkate umepanda sijui viberiti vinauzwa buku,sababu kibao.

Hapo tunasetiwa ili tujae tulipuliwe na lingine,ukilalamika tena utaambiwa Marekani mafuta kununua mwisho lita 1,saiv kule n wanakula michemsho tu,Hii nchi sijui.
 
Jamani hvi Urusi na Ukraine ndio chanzo cha haya yote.!???? Kwamba Russia ana nguvu ya kutikisa Dunia kiuchumi....

Au tumedandia tu treni kwa mbele....!??

Maana mswahili always ni mtu wa excuse
 
Nadhani Serikali inatengeneza tatizo.... Ili baadae ije kulitatua kwa mileage za kisiasa....

Yaaani chifu mkuu siku akisema sasa tunapunguza 1,2,3...basi aonekane shujaaaaa.

and the Circle continues
 
Je Malawi, Zambia wamewezaje?
Enyi wafanya siasa mwogeni Mingu
 
Back
Top Bottom