Mussa Zungu: Tutegemee mengi magumu yatakuja. Asema kupanda kwa bei hakujatengenezwa na Serikali

Serikali ndiyo inayokusanya na ku-allocate resources.Inaweza ku-allocate resources vibaya au vizuri,kwa hiyo ni upunguani kufikiri kuwa serikali haiplay role katika umasikini au katika maendeleo ya nchi.

Akina Ford na magari yao ili walete maendeleo katika Taifa ni lazima serikali iweke sera nzuri katika ukusanyaji kodi na katika matumizi ya kodi hiyo katika maendeleo.Unapokuwa na akina Ford halafu ukawa na Serikali ya Mapaka kama ya Tanzania Taifa haliwezi kufua dafu katika maendeleo.
 

Ivi kazi ya serikali ni nini? Maana Naona na serikali nayo inalalamika haya nayo ni maajabu walahi.....

inchi hii hakuna raisi, na aliyeshiba hawezi kumkumbuka mwenye njaa....
 
hawa wanafaidi milions ya hela kwa mwezi hawana maumivu na utafutaji wa juani.Sasa wananchi tunaishi kama kuku wa kienyeji.Hatuoni thamani kubwa kwa wawakilishi wetu.
 
Bravo. Sophomore

 
Hawa watu wameshatuona sisi wajinga sana, wameshiba hela wanaongea tu wanavyotaka, eti tutegemee magumu, sasa serikali maana yake nini?
Issue hapa ni ku mobilise resource kukabiliana na hii hali baadhi ya tozo zitolewe miradi mingine isimame kwanza. Sawa tunajenga madarasa ya kufundisha nini ili watoto wakimaliza wazalishe badala kukaa tu nyumbani na mitaani with nothing to do.
Je, hizo pesa zingetumika kwanza kuimarisha miundo mbinu ya kilimo uchumi usingekua kisha ukajenga madarasa. Tungeweza kutoa ruzuku ya mbolea. Madawa, zana za kilimo, umwagiliaji nk. Na baada ya mwaka tu kilimo kingetoa tija kubwa.
Unamkopesha kijana asome akimaliza unamwambia ajiajiri na bila mkopo itawezekana kweli?
Unampeleka mtu kusoma injinia halafu anamaliza kisha anakaa miaka kumi bila ku practise, huo uinjinia bado upo kweli na bado unamwambia ajiajiri huku wewe hujiajiri unafukuzia vyeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…