Must see Movies

Must see Movies

Kwa Wazungu, filamu za Afrika zinazoshinda ni zile zinazoelezea matatizo yanayowapata waafrika...Disgusting!!!

Kwao, sisi Afrika ni shida, tabu, adha, kadhia, matatizo, dhahama, mapito na maneno yanayofananana na hayo. I dont buy that!!

Waafrika tunaishi kwa kupendana (nakubali tuna matatizo ya hapa na pale)...Lakini tunathaminiana sana....na zikitengenezwa filamu za Mshikamano, utakuta zinakamata mkia... To hell with their rating!!

Hapa mkuu licha ya ujumbe pia tukiangalia upande wa viwango bongo movie ni sifuri kabisa, sauti mbaya, position za camera mbaya, rangi hovyo kabisa, uvaaji wa uhusika pumbafu kabisa, location za kijingajinga,na wanapoigiza mapigano (action) ndio wanakuwa pumbaaafu kabisa...
 
zetu sio filamu bali ni maigizo.

Tunashindwa kutofautisha majukumu katika utengenezaji wa filamu, wenzetu kuna mtu anatunga story tu alafu kuna wengine kazi yao ni kucheza na wengine kuongoza, kwa mtaji huu lazima picha iwe kali na kuangalia maslahi kwa Taifa sio kama hawa jamaa zetu wanatengeneza filamu ambazo kwa sie tuliopo huku kijijini Ihayabuyaga tunaamini mjini maisha ni mazuri kwa kuwa wanachojua wao ni kucheza picha kwenye majumba mazuri mazuri wakati wengi hawana maisha kama hayo. (Mtu anaandika stori anacheza alafu na anaongoza filamu hapo lazima awe na bias)
 
Mi nashangaa,hivi kibisa cha akina Wema Sepetu mnaita film?Na ndo mnategemea mpewe tuzu kweli?
 
Kichwa cha mwenda wazimu,Shamba la bibi,Eti ziwa nyasa cyo letu,twende kushangaa magorofa na mahekalu Omani,Migomo na maandamano kla sehemu.Nchi ya 3 kwa kuomba misaada,Police Kuua raia na HATA KWENYE FILMS?.Laana ya namna gani ndgu zangu?Ngoja tuhamie kwenye digital labda hali itakuwa nzuri.
 
Kichwa cha mwenda wazimu,Shamba la bibi,Eti ziwa nyasa cyo letu,twende kushangaa magorofa na mahekalu Omani,Migomo na maandamano kla sehemu.Nchi ya 3 kwa kuomba misaada,Police Kuua raia na HATA KWENYE FILMS?.Laana ya namna gani ndgu zangu?Ngoja tuhamie kwenye digital labda hali itakuwa nzuri.
 
Hapa mkuu licha ya ujumbe pia tukiangalia upande wa viwango bongo movie ni sifuri kabisa, sauti mbaya, position za camera mbaya, rangi hovyo kabisa, uvaaji wa uhusika pumbafu kabisa, location za kijingajinga,na wanapoigiza mapigano (action) ndio wanakuwa pumbaaafu kabisa...

Upo sahihi sana mkuu.kwangu hata geti hazivuki hizo! nyingi zimesheheni UFIRAUNI
 
I've to watch Flight this weekend. Django was cool.....Life of Pi was good.
BAK Vipi wewe? what's next??
 
  • Thanks
Reactions: BAK
hii The confession ya 2011 lakini nilii-watch jana nikamuhurumia sana huyu padre. Vitubio vingine noma, lol!
 
Last edited by a moderator:
MV5BMTUxMzQyNjA5MF5BMl5BanBnXkFtZTYwOTU2NTY3._V1._SX500_SY740_.jpg


The Green Mile (1999)...




wapendwa hii ni movie safi sana yenye kuhusisha matukio yenye maadhi ya drama, uhalifu na fantancy!

Uvutiaji wake unaanzia pale Jitu kubwa Jeusi la Miraba minne John Coffey linapokamatwa huku mikononi mwake likiwa na vibinti viwili vilivyo bakwa na kuuawa.
Mahakama ikampata na hatia hivyo kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa katika Gereza la Green Mile!

Paul (Tom Hanks) akiwa incharge wa maaskari Jela katika Gereza hilo amekuwa na maambukizi ya damu na anakuwa na tatizo ambalo madaktari walionekana kulishindwa, hivyo amekuwa katika mateso ya zaidi ya miezi kadhaa mkojo anakojoa kwa mateso sana na haki ya ndoa kwa mkewe hawezi kushiriki.......

Siku ya muujiza;
Alipokuwa akitoka maliwatoni kwa haja ndogo Paul maumivu yalimzidia hadi akaanguka kwenye sakafu ambayo kwenye corridor iliyo mkabala na cell za wafungwa….


  • Kitu cha pekee kuhusu Jitu Kubwa
John Coffey ni Jitu Kubwa sana, ambalo toka siku linaingia gerezani watu wote walilishangaa na kuliangalia kwa kulihofia.
Lakini kitu cha ajabu sana tofauti na sura yake na namna alivyo kimaumbile John Coffey, ni mtu mwema na aliyeweza kuling’amua hilo mapema kabisa ni Afande Incharge Paul, na kuna namna ya mvuto aliuona kwa John.
……Paul wakati anagalagala pale chini kwenye sakafu, John aliweza kumuona kutokea kwenye Cell yake na akamuita, Paul alijikongoja mpaka kwa John, John jitu kubwa lilimkamata kwa nguvu huku likimtaka atulie, Paul baaada ya kutapatapa na kutaka kupeleka mkono ilipo bastola yake, John akawa amemuwahi na kumsihi kuwa atulia kwakuwa ameyaona mateso yake (Paul ya ule ugonjwa), baada ya hayo maneno Paul alitulia.
John alipeleka mkono mpaka kwenye maeneo ya kiuno na mpaka chini kwenye korodani za Paul mithiri ya Mtu aliyekuwa akiombea lakini ilikuwa kimya-kimya, baada ya dakika kadhaa akamuachia Paul.
Hakikuwa kitu cha kuamini kwa Paul ila ndio ulikuwa ukweli kuwa amepona….!
Na alirudi nyumbani kwake siku ile my wife wake hakulala kwa rigwaride alilompa kiu cha mwaka mzima asikwambie mtu.
Swali pekee alilobaki nalo kujiuliza Paul ni nini siri ya Jitu hili kubwa lenye maupendo na miujiza ya namna hii?
Ni kweli alivibaka na kuviua vile vitoto?

Na labda swali utakalojiuliza wewe ambaye hujaiona movie hii, Je kuna muujiza mwingine John Coffey alifanya?, Mkubwa kiasi gani huo muujiza? Unasisimua? Unavutia??
Je alinyongwa kama wahalifu wengine?

Najua tunakimbizana na wakati na kila mtu angependa kuangalia movie mpya ila nakwambia kuna movie za zamani kama hizi lakini ukija kuitazama kama ni mpenzi wa movie za mahadhi haya ni utajuta na kujiuliza ulikuwa wapi siku zote, ni movie moja nakushauri kuwa lazima uiangalie sio uungwana kuikosa.

cc: @FP, paulss, Mtambuzi, AshaDii, BelindaJacob, BAK.

NB: Invisible au Mod yeyote wa Jukwaa hili nisaidie kuweka sawa hiyo pic katika ukubwa wenye kiwango naona browser yangu imefail ku-paste image ..... Natanguliza shukrani!!
 
Last edited by a moderator:
Hii ni kati ya movie chache alizoact Tom Hanks nilizozipenda (Nyingine ni Saving Private Ryan, You've got a mail & Catch me if you can)..mpaka leo ninayo kwenye movie library yangu...!
Thanks kwa kukumbushia na kwa hii video yake mkuu jouneGwalu ...Uwe na weekend njema!!!
 
Last edited by a moderator:
Usingizi umekimbia BJ!? au unasafari? maana ni mapema hata majogoo hayajawika lol!

Hii ni kati ya movie chache alizoact Tom Hanks nilizozipenda (Nyingine ni Saving Private Ryan, You've got a mail & Catch me if you can)..mpaka leo ninayo kwenye movie library yangu...!
Thanks kwa kukumbushia na kwa hii video yake mkuu jouneGwalu ...Uwe na weekend njema!!!
 
Back
Top Bottom