much know
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 11,461
- 17,183
Achana na siasa za kishamba mkuuNa visivyohamishika navyo vimefikwa bei[emoji24]View attachment 2268278
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Achana na siasa za kishamba mkuuNa visivyohamishika navyo vimefikwa bei[emoji24]View attachment 2268278
Hata Mithali 13:12 inasema "Mtu mwema huwaachia Wana wa wanawe urithi[emoji2827][emoji2827][emoji1545][emoji1545]Duuuh, sitaki kuamini.
Ni kweli wote tutakufa na kuzikwa, Ila je kabla hatujafa tunaishije?
Wenzetu wanaifaidi Dunia na wanaandaa mpaka vitukuu vifaidi Dunia!
Wewe unaishije kwa Sasa na mwanao unamwandaliaje maisha yake yasiwe gombania goli?
Hata Mithali 13:12 inasema "Mtu mwema huwaachia Wana wa wanawe urithi".
Nina hofu kuu kila nikitafakari na kuyaangalia mambo yanavyokwenda.. Nawaangalia wanangu kisha roho inaniuma sana! Naona wazi kabisa napaswa, nahitajika kufanya jambo... Jambo kubwa kwa ajili ya kesho njema ya wanangu na wanao pia.. Mimi nawe.. Sio wao na wana wao!
Tunaundiwa tabaka la watawala. Wao na wana wao, wajukuu na vitukuu, vilembwe na vining'ina! Kwamba akitoka mimi ni wewe halafu ni yule na yule walio kati yetu.. Hakuna nje ya tabaka lao atakayeruhusiwa naye kuwa fulani kati yao!
Tunaundiwa tabaka la kimfumo, hesabu zao ziko kamili japo kwa kificho na kuzuga kwingi, wanachongeana njia na vichochoro, wanapeana connection, wanaundiana mitandao, wanachaguana, wanateuana, wanabadilishana na kupeana nafasi.. Kama wewe si mmoja wao hupaswi hata kuwaza utapata lini kwenye nini na nini...!
Tunaundiwa tabaka la elimu.. Elimu ni ufunguo wa maarifa na uwezo wa kufanya maamuzi.. Wamejitenga na mfumo wetu wa elimu unaofubaza bongo za wanetu.. Kamwe hawawezi kukubali wanao wapate maarifa sawa na wana wao,. Elimu ni silaha kubwa kwenye kudai haki ama kutengeneza mfumo! Wa kwao wanasomeshwa shule bora na vyuo bora.. Wanaandaliwa!
Tunaundiwa tabaka la kipato.. Kipato ni silaha pia ya kupambana panapohitaji maamuzi na matumizi ya nguvu.. Kwamba utake usitake lazima hili liwe... Ukikomaa sana kuna mawili wakumalize ama wakulambishe ukae kimya! Hapa kila mmoja kwa nafasi yake anajitahidi kukusanya nyingi awezavyo.. Nyingi nyingi zaidi nyingi kabisa.. Wanatambua nguvu ya shekeli penye udhia[emoji25]
Tunaundiwa tabaka la kijamii, kuna kwao na kuna kwetu, kwao kunatamanisha na kuvutia .. Kwao kuna kila kitu katika mpangilio wake, katika utaratibu wake.. Je kwako hapo kwenu pakoje!? Kamwe hawawezi kukubali kwao pawe kwako na kwenyu pawe kwao.. Hawako tayari kufanya huo ujinga! Huduma za afya, huduma za msingi kuna tofauti kubwa kati yao na yetu
Tunaundiwa tabaka vijakazi wavuja jasho.. Wakamuliwaji, wao ndio wakusanyaji na wapangaji..hawana huruma nawe... Wanachojali ni kukukamua mpaka tone la mwisho! Hawana huruma nawe, hawana mustakabali nawe, wanachojali ni wapate hata kile kidogo ulichobakiwa nacho... Hawa ni chui kwenye ngozi ya kondoo.. Utawekewa kila aina ya kodi na kila aina ya tozo..! Wewe ni punda.. Sema mimi ni punda![emoji24]
Tunaundiwa tabaka la waoga na wenye hofu, wepesi wa kusahau na wepesi wa kusifu na kuabudu... Tunaundiwa utii kwa shuruti.. Hutakiwi kusema LA bali hewala mkuu...! Ukienda kinyume ama ukahoji majina yote mabaya utapewa wewe.. Na ukijitia kushupaza shingo wana mkono wa ken vice kukunyorosha! Mwishowe ni woga , hofu na taharuki kila kona..!
Tunaundiwa taifa la vijana wa hovyo hovyo, wajinga wajinga wapuuzi puuzi. Wasio na maono, wasio na tafakuri, wasio na hekima, wasio na elimu, wasio na maarifa wala mustakabali,. Wanachojua ni uchawa, umbea majungu na mambo mepesi mavazi na starehe huku wakiota ndoto za Alinacha na kusimuliana hekaya za Abunuwasi.. Hakuna ubunifu bali kuiga na kunakili
Wanakushughulisheni na haya yote ili msahau yote yenye tija na yenye kubeba mustakabali wa kesho ya wanao... Vimeondoka vingi tulivyobarikiwa na Mola wetu ... Walisaidia na kusaidiana kubeba vyote vinavyobebeka, vyote vimepigwa mnada kwa vipande vya fedha kidogo na ahadi ya madaraka.. Wametengewa mafungu yao..wanakula mpaka wanavimbiwa.
Sasa ni muda wa kuanza kuchukua na visivyohamishika! Na wakivitaka watavichukua tuu.. Utake usitake...! Nachelea kuwaona wanangu na vizalia vyao wakiwa watumwa kwenye ardhi yao wenyewe! Inaumiza sana! Kwakuwa wameshajijengea miisho yao itakayokoma vizazi na vizazi.. Kazi ipo kwenye vizalia vyako na vyangu.
Kama umenielewa zinduka sasa.. Tukaukomboe wakati kwa manufaa ya wana na wana wa wana wetu...VIZALIA HURU..!!!
Mi sijaongelea mambo ya Mungu na maamuzi yake.Kwenye mizania ya haki.. Nukuu yako ni batili... Mungu kaamua ugomvi mkubwa sana.. !
Mimi Wala sijataja CCMSerikali ya CCM ni Ile Ile ,ni ndumilakuwili , definition ya stupidity ni kurudia method Ile Ile ukitegemea different results , ndio Sisi sasa kuendelea kuwapa madaraka watu wale wale na mfumo ule ule unaojulikana kuwa ndio source ya failure katika mambo mengi nchi hii halafu tunajaa tunaota mabadiliko aisee sijui tumelogwa na Nani ?
Mawazo yako kamanda. Kwa sasa mnalia hakuna la kufanya. Dj analamba asali tu na mchungaji naye anafuata njia.😂😂😂Umeruka moja la mizania ya haki
Steve Nyerere kaingiaje hapaNa visivyohamishika navyo vimefikwa bei[emoji24]View attachment 2268278
Taifa linatengenezwa wawepo wajinga wengiNasoma Huu Uzi mpaka nalia Bro Mshana , ningetamani JF watu wafungue nyuzi nyingi kama hizi ili tutathmini Kwa kina maisha ya mwananchi WA kawaida hii nchi , shukrani Sana kaka.
Hii nchi ni watu wachache Sana wenye hicho la kipekee , Mimi hii Hali nimeiobserve Kwa Kuda mrefu Sana , linatengenezwa Tabaka la vijakazi na watumwa nchi hii amini usiamini ,too bad akili za wengi bado zimedumaa , too blind and dumb to realize the precarious situation that we are in .
Nyimbo nyingi zisikilize midundo kisha soma lyrics utafaidi ujumbe.. MJ was above next levelDuuh kumbe hii ngoma ina ujumbe madhubuti namna hii.
Sidhani kama bongo kuna msanii anaweza kufikisha ujumbe kwa njia hii.
Muziki huunganisha zaidi watu.