Musukuma: Maprofesa wanatuchanganya; wakati wa Magufuli walisema hakuna Corona na wakati huu wa Samia wanasema tuchanjwe

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mbunge wa Geita Vijijini mh Joseph Kasheku aka Msukuma amesema Maprofesa wa Tanzania wanafeli sana na hii inasikitisha ndio maana aliwaripua bungeni.

Msukuma amesema kwa mfano tafiti za Corona zilizofanywa na maprofesa wakati wa hayati Magufuli wakitumia mapapai mbuzi, sungura, mafenesi na oil ilionyesha Tanzania hakuna Corona lakini alipoingia Rais Samia maprofesa walewale wameshauri tuanze kuchomwa " masindano" na kuvaa mabarakoa.

Msukuma anajiuliza hawa maprofesa wetu wamesoma kweli?

Msukuma amemshauri Rais Samia kutumia wanasayansi wa nje kama anaona hawa wa kwetu wamejaa longo longo.

Chanzo: Clouds Digital
 
Form seven ni Shida, yaani yeye anadhani kipindi cha utawala ULE yale maamuzi ya kupinga na Kuficha kuwa Corona haikuwepo yanaweza ku-hold water kwa kiongozi wa sasa mwenye Maono (uongozi sikivu).

Hivi ni kweli huyo form Seven hajui hasara ya kupoteza wapendwa wetu kwa Maamuzi ya ajabu ajabu. Mimi Ilikuja kunizidishia machungu na niliuchukia utawala ule zaidi tena Zaidi pale tu Dada yangu Daktari alipofariki kwa corona and was the only Dr in our family. Baba alikuwa anatuambia alimsomesha kwa gharama kubwa.

Tumwombe tu huyo form seven hasiturudishe matesoni,kwani maamuzi ya uongozi wa sasa kuhusu Corona (task force ya kumshauri SSH kuhusu Corona) ni sahihi na yaheshimiwe.

Anachojifanya hajui ni kuwa, Watawala uliopita Ulikuwa unaogopwa, ulikuwa utawala wa YES BOSS or ONE MAN SHOW kila alichokisema mtawala ndicho wasaidizi wake walikitenda na kutuaminisha kuwa tuko sahihi ili mradi tu Maisha na familia zao vilineemeka na utawala ule.
 
Mbunge wa Geita vijijini mh Joseph Kasheku aka Msukuma amesema maprofesa wa Tanzania wanafeli sana na hii inasikitisha ndio maana aliwaripua bungeni...
Kilichomsababisha yeye kumkimbia Lowassa kwa speed kaliiiiii baada ya kukatwa ndani ya CCM ndicho hicho hicho kinachofanya maprofesa kukosa msimamo kama yeye.
 
Msukuma ana ugomvi mkubwa sana na wasomi sijui kwanini.

Na anageuza habari! Hao maprofesa wakati wa JPM ni lini walifanya utafiti wakagundua Tanzania hakuna korona? Hakukuwa utafiti wowote isipokuwa kulikuwa na matamko kuwa Tanzania hakuna korona
 
Ule wa mapapai ulikuwa ni nini bwashee?
 
Safi sana Musukuma wewe ni akili kubwa kuliko hao madaktari na maprofesa njaa. Wao akili waliyonayo ni kucheza na mindset za watawala ili waandelee kushibisha matumbo yao badala ya kuleta manufaa kwa Taifa.

Sasa walishamsoma mama wakaona hana uhakika juu uwepo au kutokuwepo kwa corona virus nchini ila kwa kuwa kaonesha kutokubaliana baliana na msimamo wa mtangulizi wake juu ya ugonjwa huu hadi kuamua kuwapa wataalam wafanye utafiti wa kisayansi, wao wakaona fursa na wakafanya kweli kama yule wa makinikia.

Yaani hawa hawa walioshindwa kuleta tu mitaala ya elimu inayolenga uhalisia wa mazingira yetu ndo waweze korona-sisi bado sana.
GO GO ON MUSUKUMA
 
Msukuma ana ugomvi mkubwa sana na wasomi sijui kwanini.

Na anageuza habari! Hao maprofesa wakati wa JPM ni lini walifanya utafiti wakagundua Tanzania hakuna korona? Hakukuwa utafiti wowote isipokuwa kulikuwa na matamko kuwa Tanzania hakuna korona
Mjibu kwa hoja.

Kuwa darasa la saba haimaanishi hauna maarifa!
 
Safi sana Musukuma wewe ni akili kubwa kuliko hao madaktari na maprofesa njaa. Wao akili waliyonayo ni kucheza na mindset za watawala ili waandelee kushibisha matumbo yao badala ya kuleta manufaa kwa Taifa.

Sasa walishamsoma mama wakaona hana uhakika juu uwepo au kutokuwepo kwa corona virus nchini ila kwa kuwa kaonesha kutokubaliana baliana na msimamo wa mtangulizi wake juu ya ugonjwa huu hadi kuamua kuwapa wataalam wafanye utafiti wa kisayansi, wao wakaona fursa na wakafanya kweli kama yule wa makinikia.

Yaani hawa hawa walioshindwa kuleta tu mitaala ya elimu inayolenga uhalisia wa mazingira yetu ndo waweze korona-sisi bado sana.
GO GO ON MUSUKUMA
Hahahaaaa. Msukuma ni la 7 lakini anaongoza kwa kujenga hoja mwanana bungeni!
 
Mbunge wa Geita vijijini mh Joseph Kasheku aka Msukuma amesema maprofesa wa Tanzania wanafeli sana na hii inasikitisha ndio maana aliwaripua bungeni.

Msukuma amesema kwa mfano tafiti za Corona zilizofanywa na maprofesa wakati wa hayati Magufuli wakitumia mapapai mbuzi, sungura, mafenesi na oil ilionyesha Tanzania hakuna Corona lakini alipoingia Rais Samia maprofesa walewale wameshauri tuanze kuchomwa " masindano" na kuvaa mabarakoa.

Msukuma anajiuliza hawa maprofesa wetu wamesoma kweli?

Msukuma amemshauri Rais Samia kutumia wanasayansi wa nje kama anaona hawa wa kwetu wamejaa longo longo.

Source: Clouds Digital
Chanjo ya corona ni ufisadi tu. wakowapi wanaoumwa korona Tanzania? Kama korona inawafuta wavaa barakoa hao wa high profile ambao wakati Hayati yupo walikuwa hawavai na wala hawakufa, basi wachanjwe wao.

Yawezekana virusi vinaambatana na mawazo ya kiutawala utawala na ndiyo maana hata chanjo inagusa hadi DNA na RNA ili pengine iwaondolee hisia za utawala ili corona wasiwafuate.

Sisi tusio viongozi hatuna korona na hatuvai mabakkoa na hiyo korona haijatufuata, watuache.

Si rahisi kuelewa mpangi huu ni ufisadi wa aina gani.
 
Msukuma anajiuliza hawa maprofesa wetu wamesoma kweli?

Msukuma amemshauri Rais Samia kutumia wanasayansi wa nje kama anaona hawa wa kwetu wamejaa longo longo.
1622113125563.png
 
Back
Top Bottom