Kama hiyo ndo argument yake basi Msukuma ndo anajichanganya kwa sababu matakeo ya huo anaoita utafiti ni kwamba corona ilisambaa hadi kwa mbuzi, mapapai na mafenesi.Mbunge wa Geita vijijini mh Joseph Kasheku aka Msukuma amesema maprofesa wa Tanzania wanafeli sana na hii inasikitisha ndio maana aliwaripua bungeni.
Msukuma amesema kwa mfano tafiti za Corona zilizofanywa na maprofesa wakati wa hayati Magufuli wakitumia mapapai mbuzi, sungura, mafenesi na oil ilionyesha Tanzania hakuna Corona lakini alipoingia Rais Samia maprofesa walewale wameshauri tuanze kuchomwa " masindano" na kuvaa mabarakoa.
Msukuma anajiuliza hawa maprofesa wetu wamesoma kweli?
Msukuma amemshauri Rais Samia kutumia wanasayansi wa nje kama anaona hawa wa kwetu wamejaa longo longo.
Chanzo: Clouds Digital
Sasa kama ugonjwa uligundulika hadi kwa wanyama na mimea na yeye mwenyewe alipiga nyungu kujitibia huo ugonjwa kwanini asichanjwe? Au anaogopa sindano?