Muswada wa Sheria ya Kutenganisha Msikiti wa Makonda na Serikali Huu Hapa

Deus Jovin

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2013
Posts
250
Reaction score
201
1791104219413.png

Mpendwa Msomaji,

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Arusha Mjini, Paul Makonda, ametangaza mpango wa kujenga msikiti mkubwa jijini Arusha ambao utatumika kwa ibada na kuwa kivutio cha utalii.

• Gharama: Makadirio ya awali ya ujenzi yanatajwa kuwa kati ya dola za Marekani milioni 80 hadi 100 (zaidi ya Shilingi za Kitanzania bilioni 210).

• Eneo: Eneo la ujenzi tayari limeshapatikana kupitia viongozi wa dini.

• Lengo: Kujenga msikiti wa kisasa utakaowezesha wageni na waumini kutalii na kujifunza historia na utamaduni wa Arusha mbali na kuswali pekee.

• Hali ya Sasa: Paul Makonda bado anaendelea na jitihada za kutafuta wadau na wafadhili kwa ajili ya kugharamia mradi huo mkubwa

Ni maoni yangu kwamba, sera hii inapingana na Katiba ya Nchi yetu, hasa ibara ya 3(1) inayosema kuwa Tanzania ni nchi isyo na dini ya kiserikali.

Tamko la Makonda halina tofauti na lile Tamko la hayati Rais Mwinyi lililofuta sera ya kitaifa kuhusu sare ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Tamko hili liliiondolea sekta ya elimu jukumu lake la msingi la kujenga tawasifu ya kitaifa (national identity) vichwani mwa wanafunzi wanaoendelea kukua.

Hivyo, nimeamua kuwasilisha kwako Muswada wa Sheria ya Ushirikiano na Utengano Kati ya Dini na Serikali ya Mwaka 2026.

Ni kwa ajili ya kuchochea mjada mpana utakaohitimishwa kwa kutunga sheria mahsusi kwa ajili hii.

Sheria hii inayopendekezwa inaweka mfumo wazi na wenye usawa wa kusimamia uhusiano kati ya taasisi za dini na serikali.

Inafafanua mipaka muhimu ili kulinda misingi ya kikatiba ya utengano, huku ikitengeneza njia za kisheria za ushirikiano wenye tija katika masuala ya kijamii, elimu, na misaada ya kibinadamu.

Malengo makuu ya muswada huu ni:

1. Kulinda uhuru wa kuabudu na kuhakikisha serikali haifungamani na upande wowote wa kidini.

2. Kuweka mipaka ya wazi ili kuzuia serikali kuingilia mambo ya dini na kinyume chake.

3. Kuunda mifumo rasmi ya ushirikiano wa uwazi katika miradi ya maendeleo na ustawi wa jamii.

Pamoja na barua hii, nambatanisha:

1. Nakala kamili ya muswada huu pamoja.

2. Muhtasari wa Muswada huu kwa ufafanuzi (dokezo).

Nitafurahi kupata fursa ya kujadiliana nawe kuhusu pendekezo hili kupitia jukwa hili au vinginevyo.

Ahsante kwa muda wako,

Wako mwaminifu,

Raia Mwema.
 
Attachments

View attachment 3683498

Naunga hoja mkono, lazima tutenge mambo ya dini na serikali katika nchi.
 
vipi kuhusu dua pale bungeni, mtizamo upo vipi
 
Dah!
Hiyo nimesahau tu.
Inabidi iongezwe.
Hata dua kwenye mikutano ya siasa za kitaifa haifai.
Maboresho yanahitajika.
Nimeyafanya tayari
Tazama maboresho hapa chibu
Big up!
 
Attachments

Dah!
Hiyo nimesahau tu.
Inabidi iongezwe.
Hata dua kwenye mikutano ya siasa za kitaifa haifai.
Maboresho yanahitajika.
Big up!
Ile Bungeni si inaitwa Dua jamani
Au umesahau spika huwa anaanzaje kuitaja
Dua ya kuombea taifa letu na bunge.
By the way ile dua ni natural (mkirsito, muislam na mpagani pia anaitamka.
 
dua inamuomba Mwenyezi Mungu, mpagani ana ushirika gani hapo?
 
Makonda tangu agunduwe deal la jezi za Taifa stars hana chake, TTF na Sunderland walishamalizana sasa amekuwa kama kichaa.

Sasa hapi comeback yake anataka kupiga pesa za DP World ambao mambo kama ni ndugu katika imani.

Kwa hili Bashite yuko mbele ya muda lazima apige mzigo wake makombo atawabwagia ndugu katika imaan Inshaallah.
 
dua inamuomba Mwenyezi Mungu, mpagani ana ushirika gani hapo?
Sio wapagani wote hawaamini uwepo wa Mungu.
Kasome aina za upagani halafu pia ukatofautishe kutokuamini Mungu na Upagani
Upagani ni dini ambayo ndani yake kuna madhehebu yao na imani na desturi zao kama walivyo wakristo na waislam.
Kasome aina za upigani zipo kama hivi.

Kasome wapagani na tafsiri zao
Polytheism
Pantheism
Duetheism
Henotheism

Wapagani wanatawaliwa na nguvu ya asili, hawaamini kitabu (Quran au Biblia).
 
Mpendwa Msomaji,

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Arusha Mjini, Paul Makonda, ametangaza mpango wa kujenga msikiti mkubwa jijini Arusha ambao utatumika kwa ibada na kuwa kivutio cha utalii.

• Lengo: Kujenga msikiti wa kisasa utakaowezesha wageni na waumini kutalii na kujifunza historia na utamaduni wa Arusha mbali na kuswali pekee.

Ni maoni yangu kwamba, sera hii inapingana na Katiba ya Nchi yetu, hasa ibara ya 3(1) inayosema kuwa Tanzania ni nchi isyo na dini ya kiserikali.

Raia Mwema.
Arusha inabahati sana kupata Mbunge, sio tuu mwenye upako wa Mungu., bali pia ni Mkristo, mlokole, mwenye upendo na Waislamu wa Arusha, alipokuwa RC, akajulishwa kuwa sheikh wa mkoa hana gari, alimpatia gari jipya la maana. Sasa anawajengea Msikiti wa hadhi ya Arusha.
Maendeleo ya Arusha jiji, yatapaa.

P
 
Sawa, serikali haina dini, lakini viongozi wake wana imani zao wanazozifuata.

Sasa mtawatenganisha vipi hawa watu na imani zao?

Kwamba tunataka viongozi wa serikali wawe wapagani kwenye hiyo katiba mpya,

au

Kiongozi akishakuwa wa serikali aikane imani yake?
 
Sio wapagani wote hawaamini uwepo wa Mungu.
Kasome aina za upagani halafu pia ukatofautishe kutokuamini Mungu na Upagani
Upagani ni dini ambayo ndani yake kuna madhehebu yao na imani na desturi zao kama walivyo wakristo na waislam.
Kasome aina za upigani zipo kama hivi.

Kasome wapagani na tafsiri zao
Polytheism
Pantheism
Duetheism
Henotheism

Wapagani wanatawaliwa na nguvu ya asili, hawaamini kitabu (Quran au Biblia).
usitake kutorokea kwenye mlango wa semantics,
 
View attachment 3683498
Mpendwa Msomaji,

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Arusha Mjini, Paul Makonda, ametangaza mpango wa kujenga msikiti mkubwa jijini Arusha ambao utatumika kwa ibada na kuwa kivutio cha utalii.

• Gharama: Makadirio ya awali ya ujenzi yanatajwa kuwa kati ya dola za Marekani milioni 80 hadi 100 (zaidi ya Shilingi za Kitanzania bilioni 210).

• Eneo: Eneo la ujenzi tayari limeshapatikana kupitia viongozi wa dini.

• Lengo: Kujenga msikiti wa kisasa utakaowezesha wageni na waumini kutalii na kujifunza historia na utamaduni wa Arusha mbali na kuswali pekee.

• Hali ya Sasa: Paul Makonda bado anaendelea na jitihada za kutafuta wadau na wafadhili kwa ajili ya kugharamia mradi huo mkubwa

Ni maoni yangu kwamba, sera hii inapingana na Katiba ya Nchi yetu, hasa ibara ya 3(1) inayosema kuwa Tanzania ni nchi isyo na dini ya kiserikali.

Tamko la Makonda halina tofauti na lile Tamko la hayati Rais Mwinyi lililofuta sera ya kitaifa kuhusu sare ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Tamko hili liliiondolea sekta ya elimu jukumu lake la msingi la kujenga tawasifu ya kitaifa (national identity) vichwani mwa wanafunzi wanaoendelea kukua.

Hivyo, nimeamua kuwasilisha kwako Muswada wa Sheria ya Ushirikiano na Utengano Kati ya Dini na Serikali ya Mwaka 2026.

Ni kwa ajili ya kuchochea mjada mpana utakaohitimishwa kwa kutunga sheria mahsusi kwa ajili hii.

Sheria hii inayopendekezwa inaweka mfumo wazi na wenye usawa wa kusimamia uhusiano kati ya taasisi za dini na serikali.

Inafafanua mipaka muhimu ili kulinda misingi ya kikatiba ya utengano, huku ikitengeneza njia za kisheria za ushirikiano wenye tija katika masuala ya kijamii, elimu, na misaada ya kibinadamu.

Malengo makuu ya muswada huu ni:

1. Kulinda uhuru wa kuabudu na kuhakikisha serikali haifungamani na upande wowote wa kidini.

2. Kuweka mipaka ya wazi ili kuzuia serikali kuingilia mambo ya dini na kinyume chake.

3. Kuunda mifumo rasmi ya ushirikiano wa uwazi katika miradi ya maendeleo na ustawi wa jamii.

Pamoja na barua hii, nambatanisha:

1. Nakala kamili ya muswada huu pamoja.

2. Muhtasari wa Muswada huu kwa ufafanuzi (dokezo).

Nitafurahi kupata fursa ya kujadiliana nawe kuhusu pendekezo hili kupitia jukwa hili au vinginevyo.

Ahsante kwa muda wako,

Wako mwaminifu,

Raia Mwema.

Ujenzi wa Msikitini yeye kaja na nia wazo tu pesa ya Ujenzi sio ya Serikali

Kuna mgongano gani apo kati Serikali na Dini usika!!

Kwani Viongozi wa Serikali mbona tunawaona wakishiriki kwenye Ujenzi wa Misikitini na Makanisa mbali mbali

Mtoa Mada punguza Chuki ya Kidini kunywa maji mengi utapona ugunjwa wako
Unaokusumbua

Msikitini wa kitalii kwa faida ya Taifa zima litapokea wageni kushangaa jiji la Arusha na vivutio vyake

kama Msikitini mkubwa mzuri
lkn pia tutawavutia Watalii wa kidini kutoka Duniani Kote!!!

jiandae kuchangia kwa imani yako yoyote ili Arusha ipendeze!!

Naunga mkono wazo zuri na Waziri wetu mhe Paul Makonda
 
View attachment 3683498
Mpendwa Msomaji,

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Arusha Mjini, Paul Makonda, ametangaza mpango wa kujenga msikiti mkubwa jijini Arusha ambao utatumika kwa ibada na kuwa kivutio cha utalii.

• Gharama: Makadirio ya awali ya ujenzi yanatajwa kuwa kati ya dola za Marekani milioni 80 hadi 100 (zaidi ya Shilingi za Kitanzania bilioni 210).

• Eneo: Eneo la ujenzi tayari limeshapatikana kupitia viongozi wa dini.

• Lengo: Kujenga msikiti wa kisasa utakaowezesha wageni na waumini kutalii na kujifunza historia na utamaduni wa Arusha mbali na kuswali pekee.

• Hali ya Sasa: Paul Makonda bado anaendelea na jitihada za kutafuta wadau na wafadhili kwa ajili ya kugharamia mradi huo mkubwa

Ni maoni yangu kwamba, sera hii inapingana na Katiba ya Nchi yetu, hasa ibara ya 3(1) inayosema kuwa Tanzania ni nchi isyo na dini ya kiserikali.

Tamko la Makonda halina tofauti na lile Tamko la hayati Rais Mwinyi lililofuta sera ya kitaifa kuhusu sare ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Tamko hili liliiondolea sekta ya elimu jukumu lake la msingi la kujenga tawasifu ya kitaifa (national identity) vichwani mwa wanafunzi wanaoendelea kukua.

Hivyo, nimeamua kuwasilisha kwako Muswada wa Sheria ya Ushirikiano na Utengano Kati ya Dini na Serikali ya Mwaka 2026.

Ni kwa ajili ya kuchochea mjada mpana utakaohitimishwa kwa kutunga sheria mahsusi kwa ajili hii.

Sheria hii inayopendekezwa inaweka mfumo wazi na wenye usawa wa kusimamia uhusiano kati ya taasisi za dini na serikali.

Inafafanua mipaka muhimu ili kulinda misingi ya kikatiba ya utengano, huku ikitengeneza njia za kisheria za ushirikiano wenye tija katika masuala ya kijamii, elimu, na misaada ya kibinadamu.

Malengo makuu ya muswada huu ni:

1. Kulinda uhuru wa kuabudu na kuhakikisha serikali haifungamani na upande wowote wa kidini.

2. Kuweka mipaka ya wazi ili kuzuia serikali kuingilia mambo ya dini na kinyume chake.

3. Kuunda mifumo rasmi ya ushirikiano wa uwazi katika miradi ya maendeleo na ustawi wa jamii.

Pamoja na barua hii, nambatanisha:

1. Nakala kamili ya muswada huu pamoja.

2. Muhtasari wa Muswada huu kwa ufafanuzi (dokezo).

Nitafurahi kupata fursa ya kujadiliana nawe kuhusu pendekezo hili kupitia jukwa hili au vinginevyo.

Ahsante kwa muda wako,

Wako mwaminifu,

Raia Mwema.
Mhe Mbunge ili usilete mjadala kuhusu wema wako kwa waislamu itakuwa jambo jema uachie ubunge na ujikite kwenye kujenga misikiti ya kitalii.
Mungu ni Mwema,
Ubarikiwe na uzidishiwe mara dufu
 
Ujenzi wa Msikitini yeye kaja na nia wazo tu pesa ya Ujenzi sio ya Serikali

Kuna mgongano gani apo kati Serikali na Dini usika

Kwani Viongozi wa mbona tunawaona wakishiriki kwenye Ujenzi wa Misikitini na Makanisa mbali mbali

Mtoa Mada Chuki ya Kidini ndio
inamsumbua

Msikitini wa kitalii kwa faida ya Taifa zima
jiandae kuchangia ili Arusha ipendeze!!
Naunga mkono wazo zuri na Waziri wetu mhe Paul Makonda
Hakuna udini hapo kwa kuwa mhe Makonda ni Kafir anajitolea kutumia Ubunge wake ili amshukuru mama na kumpendekezea 10 tena kwani anatosha.
 
Back
Top Bottom