Muuguzi ajinyonga hadi kufa, Polisi wasema ni kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na madeni

Muuguzi ajinyonga hadi kufa, Polisi wasema ni kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na madeni

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, David Mtaita (30) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ikiwa ni baada ya kujichoma sindano ya kutuliza maumivu.

Akizungumza leo Alhamisi Aprili 29, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa katika uchunguzi wa awali wamebaini muuguzi huyo alijinyonga juzi saa 12 jioni kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na madeni.

Amesema kabla ya kujinyonga alijichoma sindano ya kutuliza maumivu kwa kuwa ilikutwa pembeni ya mwili wake.

“Alifanya kitendo hicho katika nyumba aliyokuwa anaishi eneo la Singisi wilayani Arumeru,” amesema na kubainisha kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Chanzo: Mwananchi
 
Angekuwa hana hiyo sindano ya ganzi asingedhubutu kujitia kitanzi! 😬😬
 
Kwa umri wake usikute alikua anajitolea tu na kulipwa kidogo jambo lililopelekea kuwa na madeni mengi. Yaani unafahamika kama dotor halafu unaishi kwa mlo mmoja.
Haya maisha hatari sana. Asubuhi unaenda kazini unarudi jioni. Ndugu zako wakikuomba hata 10, 000 hauna unafikiri umewanyima hela.
Kila siku unatengeneza matatizo tu unaona bora ufe ili uondoe lawama kbsa.
 
Ala kumbe ni muhimu kujichoma sindano kwanza eeee kupunguza uchungu wa kifo - kuna wengine wanasema ukitaka kufa vizuri badi kunywa aspilini kama 30 hivi - ukilala mazima.
 
Back
Top Bottom