Muuguzi ajinyonga hadi kufa, Polisi wasema ni kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na madeni

Muuguzi ajinyonga hadi kufa, Polisi wasema ni kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na madeni

Hata nidaiwe vp, nikutane na magumu kiasi gani, siwezi kufikiria kujiua. Haiwezekani na kamwe haitatokea eti siku moja nitingwe na mawazo mpaka kufikia hatua ya kukatisha uhai wangu.
 
Hata nidaiwe vp, nikutane na magumu kiasi gani, siwezi kufikiria kujiua. Haiwezekani na kamwe haitatokea eti siku moja nitingwe na mawazo mpaka kufikia hatua ya kukatisha uhai wangu.
Kula Tano man 👊
 
Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, David Mtaita (30) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ikiwa ni baada ya kujichoma sindano ya kutuliza maumivu.

Akizungumza leo Alhamisi Aprili 29, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa katika uchunguzi wa awali wamebaini muuguzi huyo alijinyonga juzi saa 12 jioni kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na madeni.

Amesema kabla ya kujinyonga alijichoma sindano ya kutuliza maumivu kwa kuwa ilikutwa pembeni ya mwili wake.

“Alifanya kitendo hicho katika nyumba aliyokuwa anaishi eneo la Singisi wilayani Arumeru,” amesema na kubainisha kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Chanzo: Mwananchi
Kwani Marehemu Alikuwa Anasemaje?
 
Kwa umri wake usikute alikua anajitolea tu na kulipwa kidogo jambo lililopelekea kuwa na madeni mengi. Yaani unafahamika kama dotor halafu unaishi kwa mlo mmoja.
Acha kabisa😬😬
 
Back
Top Bottom