Habari za usiku wana jamii forums,kama kichwa cha habari kinavyosema
Muuguzi Ajinyonga Hadi Kufa!!
Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, David Mtaita (30) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ikiwa ni baada ya kujichoma sindano ya kutuliza maumivu.
Arusha. Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, David Mtaita (30) amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ikiwa ni baada ya kujichoma sindano ya kutuliza maumivu.
Akizungumza leo Alhamisi Aprili 29, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa katika uchunguzi wa awali wamebaini muuguzi huyo alijinyonga juzi saa 12 jioni kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na madeni.
Amesema kabla ya kujinyonga alijichoma sindano ya kutuliza maumivu kwa kuwa ilikutwa pembeni ya mwili wake.
“Alifanya kitendo hicho katika nyumba aliyokuwa anaishi eneo la Singisi wilayani Arumeru,” amesema na kubainisha kuwa uchunguzi bado unaendelea.
Ushauri: Kwa mtazamo wangu naona Sio jambo sahihi mtu kujitoa uhai kutokana na matatizo mtu anayopitia ,hata kama unapitia matatizo kiasi gani cha msingi nikuangalia namna ya kusolve.!!Kuomba ushauri kwa wenye hekima
Mfano mimi huwa nikiwa na matatizo ni ngumu kukata tamaa sababu naamini kuna watu wenye matatizo zaid yangu Yaan chungu nzima !kuna watu wako Jalalani,hawana pakulala wala pakulaaaa , ,kuna watu hawana wazazi wote wawili and they manage To live despite How hard The life is,Kuna watu wapo polisi kwa kesi za ajabu mfano kuna rafiki yangu alipelekwa Kituoni Sasa tukajiandaa kwenda Kumtoa tunafika kituoni tukaskia kuna mtu ndani kashikwa Kwa sababu Yakumshika mdada ambaye ni Mfanyakazi mwenzake Tako [emoji28][emoji28] kibaya zaid yupo hapo Kwa zaid ya 40 days .
Lets try To agree our situations and always Smile while solving them because when we commit suicide no one will look at our family.
Maestro de Quimica !!OP