Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Ukisoma kwenye kitabu cha Injili ya Yohana sura ya pili, Kuna kisa kinasiimuliwa ambacho kilitokea katika Kana ya Galilaya.

Katikati ya harusi divai ikaisha, Mama Maria Mtakatifu akamfuata Yesu, akamwambia kuwa mzigo wa gambe umeisha.

Yesu akamjibu muda wangu bado, basi akawaagiza Vijana wamletee maji, na walipoyafunua yakawa divai iliyo bora Sana.

Sasa inakuwaje leo makanisani wanasema tusinywe kabisa maji mema?🥃🥂🍻🍺🍷
 
Ukiondoa kifungu hicho,pia kuna neno linasema "kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi,na sio kimuingiacho".

Tatizo dini zetu ni mapokeo kutoka Kwa wazungu,alafu sisi tunaamini tunaijua(dini/biblia) kuliko wao waliotuletea.

Ndio maana leo makanisa mengi yanahubiri mafanikio,fungu la kumi nk.

Imani na upendo vimewekwa Kandi kama sio msingi wa ukristo,yaani kumjua,kumwabudu na kumtumikia MUNGU sio jambo la msingi.

Mimi naamini kuna mahali tumekengeuka.
 
Pombe sio dhambi.
Ulevi ndio dhambi

Na Ulevi ni pamoja na,
1. Kunywa pombe usiyoruhusiwa na mamlaka, yaani serikali eg. Gongo,

2. Kunywa pombe muda wa kazi.

3. Kunywa pombe kupita kiasi cha nguvu zako.

4. Kunywea pombe bajeti ya jambo lingine kama, ya chakula cha watoto nyumbani, Ada ya mwanafunzi, pesa ya ujenzi, matibabu nk.
Nk.

Na hapo ni sawasawa na Ulafi, unaokatazwa ni Ulafi na sio kula chakula.
Na ulafi unafanana na ulevi kama nilivyoelezea hapo juu.

Ukichoma nyama ya mbuzi na kula ukiwa Bar huku watoto wanakula Ugali na Nguru umefanya dhambi ya Ulafi.

Pombe ni moja ya kazi njema ya Mwenyezi Mungu na haijakatazwa mahali popote katika Maandiko ya Biblia.
Lakini inatakiwa inywewe kwa kiasi na kwa wakati wake kwa lengo la kujiburudisha.

Furaha ya kwenye karamu ya Pombe yazidi furaha zote za hapa duniani.
 
Naona umekaririshwa kuwa alichokitengeneza Yesu ni pombe.
Sasa leo ninakukaririsha kitu kingine, bangi, mirungi, cocaine na heroin ni mimea iliyoumbwa na Mungu, na kwakuwa Mungu aliumba vitu vizuri, vipi kwanini wakuu wa dini waseme haramu?
 
Nawashangaa wanaoiogopa pombe zaidi ya zinaa.

Wakati maandiko yanasema kimuingiacho mtu sio najisi ila kimtokacho.

Wengi wanaona bora kuishi kwa tamaa za mwili vichwani hata kama wamefunga ndoa, hawajui sio kuzini tu, bali hata amtazamaye kwa kuntamani huyo amekwisha zini kiroho.
 
Naona umekaririshwa kuwa alichokitengeneza Yesu ni pombe.
Sasa leo ninakukaririsha kitu kingine, bangi, mirungi, cocaine na heroin ni mimea iliyoumbwa na Mungu, na kwakuwa Mungu aliumba vitu vizuri, vipi kwanini wakuu wa dini waseme haramu?
Ni haramu kwakuwa wataalamu wa afya wamejiridhisha kuwa hiyo mimea haistahiri kutumika kama ulivyoeleza hapo juu.

Na sio kwamba haina matumizi kwa Binadamu bali ina matumizi mengine.

Ndio maana hata Petroli inalewesha lakini haikutengenezwa kwa madhumuni ya kunywa kama
kileo.

Hiyo mimea inatumika kutengenezea pamoja na madawa ya wanyama na Binadamu.

Ile Nusu Kaputi ya ganzi wakati wa kufanyiwa upasuaji hospitalini ni mojawapo katika dawa zinazotokana na hiyo mimea.

Unapo sikia neno Drug abuse sio kwamba hayo madawa hayana matumizi.

Bali yametumika kinyume na yanavyotakiwa kutumika.

Utashangaa Heroine na Cocaine zinamika vizuri tu katika shughuli nyingine na kuleta matokeo chanya.
 
Naona umekaririshwa kuwa alichokitengeneza Yesu ni pombe.
Sasa leo ninakukaririsha kitu kingine, bangi, mirungi, cocaine na heroin ni mimea iliyoumbwa na Mungu, na kwakuwa Mungu aliumba vitu vizuri, vipi kwanini wakuu wa dini waseme haramu?

tusikatae kwanza ukweli kwamba alitengeneza pombe,divai inalevya kwahiyo ni pombe.

sasa tetea hoja kwanini alitengeneza siyo kutaka kusema divai siyo pombe
 
Ukisoma kwenye kitabu cha Injili ya Yohana sura ya pili, Kuna kisa kinasiimuliwa ambacho kilitokea katika Kana ya Galilaya.

Katikati ya harusi divai ikaisha, Mama Maria Mtakatifu akamfuata Yesu, akamwambia kuwa mzigo wa gambe umeisha.

Yesu akamjibu muda wangu bado, basi akawaagiza Vijana wamletee maji, na walipoyafunua yakawa divai iliyo bora Sana.

Sasa inakuwaje leo makanisani wanasema tusinywe kabisa maji mema?🥃🥂🍻🍺🍷
Je, divai ni pombe?
 
Ukisoma kwenye kitabu cha Injili ya Yohana sura ya pili, Kuna kisa kinasiimuliwa ambacho kilitokea katika Kana ya Galilaya.

Katikati ya harusi divai ikaisha, Mama Maria Mtakatifu akamfuata Yesu, akamwambia kuwa mzigo wa gambe umeisha.

Yesu akamjibu muda wangu bado, basi akawaagiza Vijana wamletee maji, na walipoyafunua yakawa divai iliyo bora Sana.

Sasa inakuwaje leo makanisani wanasema tusinywe kabisa maji mema?[emoji1634][emoji1635][emoji482][emoji481][emoji485]

Kunatofauti Kati Ya Divai na K Vant
 
Tatizo pombe na sadaka sawa na kibaka na kituo cha polisi!

Ila Imeandikwa!
[emoji116][emoji116]
SIRA 31:24-31
24Mchoyo wa chakula atasemwa kijijini kote,
na maoni yao juu ya uchoyo wake ni kweli.
Pombe iliumbwa kumfurahisha mtu
25Usijioneshe kuwa hodari wa kunywa pombe,
maana pombe imewaangamiza wengi.
26Tanuri hupima ugumu wa chuma,
na pombe hupima mioyo katika shindano la wenye kiburi.
27Pombe ni kama uhai kwa mtu ukinywa kwa kiasi.
Maisha yafaa nini bila pombe?
Imeumbwa iwafurahishe watu.
28Kunywa pombe wakati wake na kwa kiasi,
kwaleta shangwe moyoni na furaha rohoni.
29Lakini kunywa pombe kupita kiasi,
kunaleta kuumwa kichwa, uchungu na fedheha.
30Ulevi huongeza hasira ya mpumbavu akajiumiza mwenyewe;
humdhoofisha na kumwongezea majeraha.
31Usimkaripie jirani yako kwenye pombe,
wala usimdharau anapofurahia karamu.
Usimwambie neno la kumwonya,
wala usimsumbue kwa kumtaka alipe deni
 
Back
Top Bottom