Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Hapa kwenye hili suala kila mtu atatetea upande wake unaomvutia kwa kigezo cha mistari ya biblia na kuna watakaosema baadhi ya mistari ya biblia ni fumbo

Cha msingi kila kitu kina kiasi chake

Unaetumia usiwakere wasiotumia na usiotumia pia usiwakere watumiaji

IMANI YAKO ITAKUPONYA
 
Ukisoma kwenye kitabu cha Injili ya Yohana sura ya pili, Kuna kisa kinasiimuliwa ambacho kilitokea katika Kana ya Galilaya.

Katikati ya harusi divai ikaisha, Mama Maria Mtakatifu akamfuata Yesu, akamwambia kuwa mzigo wa gambe umeisha.

Yesu akamjibu muda wangu bado, basi akawaagiza Vijana wamletee maji, na walipoyafunua yakawa divai iliyo bora Sana.

Sasa inakuwaje leo makanisani wanasema tusinywe kabisa maji mema?🥃🥂🍻🍺🍷
Tunaangamia kwa kukosa Maarifa

Mithali23
29 Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole?
Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno?
Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu?
Ni nani aliye na macho mekundu?
30Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo;
Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
31Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu;
Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
32Mwisho wake huuma kama nyoka;
Huchoma kama fira.
33Macho yako yataona mambo mageni;
Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
34Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari;
Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.
35 Utasema, Wamenichapa wala sikuumia;
Wamenipiga wala sina habari;
Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
 
-Ujue Mvinyo hutengenezwa kwa kukamua maji ya mzabibu kisha hutokea juisi divai
-Divai inaweza kuwa juisi isiyolewesha na divai inaweza kuwa pombe iliyokaa mda mrefu na hii huitwa mvinyo.
-Yesu alitengeneza juisi ya mzabibu na sio pombe, angefanya hivyo angekinzana na maandoko mengi katika biblia na hivyo leo hii tungesema Yesu hakuwa mtii kwa maandiko.

31 Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
32 Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira. (Mithali 23:31-32)
 
11 "Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao! " Isaya 5:11


"Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;"Waefeso 5:18
 
Unataka kusema YESU ALIKUWA CHAPOMBE?
Ukiondoa kifungu hicho,pia kuna neno linasema "kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi,na sio kimuingiacho".
Tatizo dini zetu ni mapokeo kutoka Kwa wazungu,alafu sisi tunaamini tunaijua(dini/biblia) kuliko wao waliotuletea.
Ndio maana leo makanisa mengi yanahubiri mafanikio,fungu la kumi nk.
Imani na upendo vimewekwa Kandi kama sio msingi wa ukristo,yaani kumjua,kumwabudu na kumtumikia MUNGU sio jambo la msingi.
Mimi naamini kuna mahali tumekengeuka.
 
Aya ya 9.
Muwe mnasoma maandiko yenu jamani.
Pombe sio dhambi.
Ulevi ndio dhambi

Na Ulevi ni
1. Kunywa pombe usiyoruhusiwa na mamlaka, yaani serikali eg. Gongo,

2. Kunywa pombe muda wa kazi.

3. Kunywa pombe kupita kiasi cha nguvu zako.

4. Kunywea pombe bajeti ya jambo lingine kama, ya chakula cha watoto nyumbani, Ada ya mwanafunzi, pesa ya ujenzi, matibabu nk.
Nk.

Na hapo ni sawasawa na Ulafi, unaokatazwa ni Ulafi na sio kula chakula.
Na ulafi unafanana na ulevi kama nilivyoelezea hapo juu.

Ukichona nyama ya mbuzi na kula ukiwa Bar huku watoto wanakula Ugali na Nguru unamefanya Ulafi.

Pombe ni moja ya kazi njema ya Mwenyezi Mungu na haijakatazwa mahali popote katika Maandiko ya Biblia.
Lakini inatakiwa inywewe kwa kiasi na kwa wakati wake kwa lengo la kujiburudisha.

Furaha ya kwenye karamu ya Pombe yazidi furaha zote hapa duniani.
Screenshot_20220103-093358.jpg
 
Tunaangamia kwa kukosa Maarifa

Mithali23
29 Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole?
Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno?
Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu?
Ni nani aliye na macho mekundu?
30Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo;
Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
31Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu;
Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
32Mwisho wake huuma kama nyoka;
Huchoma kama fira.
33Macho yako yataona mambo mageni;
Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
34Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari;
Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.
35 Utasema, Wamenichapa wala sikuumia;
Wamenipiga wala sina habari;
Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
Kwanini Yesu muujiza wake wa kwanza uwe kubadili maji kuwa divai? Alitaka kutufundisha nini?
 
Unajua divai/wine ni pombe fulani yenye kilevi kidogo tu just kuchangamsha,, lkn kupitia andiko hili wachaga(sio wote) hapa ndio wanahalalisha double kiki, k vant, gongo etc.
 
Back
Top Bottom