Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Una uthibitisho gani hiyo Divai ilikua na Kilevi (Alcohol)?
Yeye mwenyewe pia alikuwa anakunywa hiyo divai.
Mathayo 11:19 Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.
 
Mkuu hiyo Divai unayoisema, nithibitishie kwamba ilikua na kilevi (Alcohol).
 
Mkuu hiyo Divai unayoisema, nithibitishie kwamba ilikua na kilevi (Alcohol).
Kwani angekuwa anakunywa non alcoholic wine wange mzushiaje kuwa ni mlevi ?
Au asingekuwa anakula chakula wange mzushiaje kuwa ni mlafi.

Usiwe na mihemuko ndugu.
 
Kwani angekuwa anakunywa non alcoholic wine wange mzushiaje kuwa ni mlevi ?
Au asingekuwa anakula chakula wange mzushiaje kuwa ni mlafi.

Usiwe na mihemuko ndugu.
Hujui kama mtu anaweza kukuzushia tu? Hujui kama zipo taarifa za uzushi tu watu mbalimbali huzushiwa?

Haya tuendelee, naomba nithibitishie hiyo Divai aliyoiombea Bwana Yesu ilikua na kilevi (Alcohol).
 
Hujui kama mtu anaweza kukuzushia tu? Hujui kama zipo taarifa za uzushi tu watu mbalimbali huzushiwa?

Haya tuendelee, naomba nithibitishie hiyo Divai aliyoiombea Bwana Yesu ilikua na kilevi (Alcohol).
Kwani wapi Mungu alizuia kunywa kilevi ?
Hadi ubishe namna hii.

Kinachotakiwa ni kunywa kwa kiasi cha kuto kushindwa kufanya majukumu yako, au kutumia kilevi kumharibu mtu.
Au kunywa kupita kiasi cha kumudu afya yako.
Tumeruhusiwa kunywa bila kufanya Ulevi na kwa wakati usio wa kazi au sala
Ila sio lazima

Ni kama chakula tu Mungu anasema tule kwa kiasi bila kufanya ulafi.

Wewe kwani unasoma kitabu gani ?
 
Hello JF,

Yesu katika majira yake alitumia divai kama damu yake iliyomwagika msalabani kwa ondoleo la dhambi kwa majira ile, lakini alipokuwa anaondoka alisema katika mathayo 26:29 "Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.

Na hiyo damu mpya katika ufalme wa baba yake tunaikuta katika ufunuo 11:6 " Hao wana amri ya kuzifunga mbingu, ili mvua isinyeshe katika siku za unabii wao. Nao wana amri juu ya maji kuyageuza kuwa damu, na kuipiga nchi kwa kila pigo, kila watakapo"

Na katika ufalme wa baba yake Yani Mungu Baba ambaye ndie CHANZO HALISI tunaona katika 1korintho 15:24-28.

Hivyo Pombe hairuhusiwi ila misingi ya dini mingine inaruhusu ila sio kusudi la muumba na yeye hana dini.
 
Kwani wapi Mungu alizuia kunywa kilevi ?
Hadi ubishe namna hii.

Kinachotakiwa ni kunywa kwa kiasi cha kuto kushindwa kufanya majukumu yako, au kutumia kilevi kumharibu mtu.
Au kunywa kupita kiasi cha kumudu afya yako.
Tumeruhusiwa kunywa bila kufanya Ulevi na kwa wakati usio wa kazi.

Ni kama chakula tu Mungu anasema tule kwa kiasi bila kufanya ulafi.

Wewe kwani unasoma kitabu gani ?
Bado haujathibitisha Mkuu, naomba kama una uthibitisho kwamba Divai aliyoiombea Bwana Yesu, ilikua na Kilevi (Alcohol)

Naomba uthibitisho, nasubiri.
 
Bado haujathibitisha Mkuu, naomba kama una uthibitisho kwamba Divai aliyoiombea Bwana Yesu, ilikua na Kilevi (Alcohol)

Naomba uthibitisho, nasubiri.
Kwani kwenye harusi watu wanafurahi wanapokunywa divai ya aina gani ?
Wayahudi walikuwa wanakunywa divai yenye kilevi siku zote.
 
Kwani kwenye harusi watu wanafurahi wanapokunywa divai ya aina gani ?
Wayahudi walikuwa wanakunywa divai yenye kilevi siku zote.
Mkuu, huo uthibitisho unao? Kama unao naomba uutoe kama hauna pia niambie.
 
Mkuu, huo uthibitisho unao? Kama unao naomba uutoe kama hauna pia niambie.
Maji ya mzabibu hayawezi kuitwa divai ikiwa hayana kilevi ndani yake. Divai ni pombe inayotokana na zabibu. Si unashiriki mkate wa Bwana kanisani we uje uwaombe wachungaji chupa ya ile divai halafu uisome uone mwenyewe.
 
Anajua kuwa hadi iitwe divai maana yake inakilevi?
Divai kwa kingereza ni wine ndivyo ninavyo jua.
Na wine zipo zenye kilevi na visivyo na kilevi.
Mfano Divai wanayoitumia Roman Cathoric kanisani ina Kilevi.

Kimaelezo ile ilikuwa divai yenye Kilevi.

Yohana 2:9 Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,

10 akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.

Ni kawaida sio kwa Wayahudi tu hata huku kwetu.
Katika mwanzo wa Sherehe Wahudumu huanza kugawa pombe nzuri kama ya kienyeji basi ni ile iliyo iva na kufikia ubora mzuri.
Watu wakisha anza kulewa lewa basi ndipo inapotolewa ile ya kiwango cha chini badala ya Henken zinaletwa safari kilimanjaro nk.

Juice au soda hazina kiwango utamu ni ule ule. Bei ni ile ile. Hakuna Juice dhaifu.

Wazee wa harusi huko Kana walishangaa divai ilitoseviwa mwanzo ndio ile ile iliyoseviwa baada ya kwisha ile ya kwanza. Walitarajia kuanza kuseviwa divai dhaifu katika mgao wa pili.
 
Mimi mwana wa Adamu nimekuja nikila na kunywa, nao wanasema, ‘Mta zameni mlafi na mlevi; rafiki wa watoza kodi na wenye dhambi!’ Lakini hekima huthibitishwa kwa matendo yake.”
Mathayo 11:8-19
Je? Hapa aliongea walichokuwa wanamsingizia ama walichokuwa wakimuona anafanya?
 
Kwa sababu pombe si matokeo ya maji kugeuzwa kuwa divai
 
Maji ya mzabibu hayawezi kuitwa divai ikiwa hayana kilevi ndani yake. Divai ni pombe inayotokana na zabibu. Si unashiriki mkate wa Bwana kanisani we uje uwaombe wachungaji chupa ya ile divai halafu uisome uone mwenyewe.
Ili kimiminika chochote kiwe Pombe kinataliwa kiwe na % of Alcohol. Pia ili kimiminika chochote kisiwe Pombe hakitakiwi kuwa na % of Alcohol (Non Alcohol), Sasa naomba nithibitishie Divai aliyoiombea Bwana Yesu ilikua ni Pombe, ukinithibitishia ilikua ni Pombe nitakuomba unitajie % of Alcohol ilikua ni ngapi?
 
Divai kwa kingereza ni wine ndivyo ninavyo jua.
Na wine zipo zenye kilevi na visivyo na kilevi.
Hapa nimekuquote umeongea Facts. Kwamba zipo wine zenye kilevi (Alcoholic) na zisizo na kilevi (Non Alcoholic), Sasa turudi kwenye mada Je kuna mwenye uthibitisho kwamba Divai aliyoiombea Bwana Yesu ilikua ni Pombe/Divai yenye Alcohol?
 
Back
Top Bottom