Hebu pitia kidogo hapa mtumishi.
Kumbukumbu la Torati 14:22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.
23 Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.
24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako;
25 ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako;
26 na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako.
Pombe maana yake ni kinywaji kinacholevya au kileo.
Ni kwamba hakijakatazwa bali kinywewe kwa kiasi na kwa wakati wake na sio kiulevi. kama vile chakula kuepusha ulafi.
Mkuu, niliuliza hilo ili kwanza kabisa tuone ni lipi kusudi la Mungu kuruhusu matumizi ya kileo. Mara zote tuyaache maandiko yajifafanue yenyewe.
Kwanza kabisa ni muhimu kuelewa maana ya aya hii:
Waebrania 10 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Basi torati, kwa kuwa ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo hayo, kwa dhabihu zile zile wanazozitoa kila mwaka daima, haiwezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.
Torati ni kivuli cha mambo yajayo, yaani agano la Kale ni kivuli tu cha agano jipya. Hivyo kitu halisi ni Yesu Kristo mwenyewe, mafundisho yake ndio njia ya wokovu wetu.
Hesabu 28 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁷ Na sadaka yake ya kinywaji itakuwa robo ya hini kwa mwana-kondoo mmoja; hiyo sadaka ya kinywaji, ya kileo, utammiminia Bwana katika mahali hapo patakatifu.
Ni vema kufahamu kuwa Mungu aliwaamuru wana wa Israeli wasongeze mbele zake sadaka ya kileo. Sadaka hii ilikuwa ni kivuli cha mambo yajayo, kivuli cha Roho Mtakatifu kama tutakavyoona mbeleni.
Ukitazama hilo fungu ulilonukuu, Mungu anawaamuru wana wa Israeli kula zaka zao za mwaka wa saba badala ya kuzipeleka hekaluni. Nni sababu hii ndio inapelekea Mungu awakumbushe wasimsahau mlawi aliyepo kwao kwani hana hazina ya vitu hivi kwa kuwa hawavipeleki hekaluni bali wale pamoja naye.
FACT: Mungu hakuruhusu watu wanywe kileo muda wote bali katika mwaka ule wa kuila zaka yao pamoja na watu wao. Hakuna mahali ameamuru waende baa ama kwa wamama wauza mbege kunywa huko, bali tendo hili lilifanyika kama ibada kamili mbele zake:
25 ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako;
Kwa wale mnaosimamia kifungu hiki kuanzia sasa jueni kuwa kileo kitanywewa
MAHALI ALIPOPACHAGUA BWANA, sasa sidhani kama
BAA ama
NIGHT CLUB ni mahali ambapo Mungu ataka kukalisha jina lake!!!
Kumbukumbu la Torati 14 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²³ Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.
Kumbe kusudi la Mungu ilikuwa
kuwafundisha wana wa Israeli kumcha Yeye. Hapo ndipo kilipo kivuli cha mambo yajayo. Pia ukitazama sura mbili nyuma unakutana na agizo hili hili:
Kumbukumbu la Torati 12 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁷ Usile ndani ya malango yako zaka ya nafaka zako, wala ya divai yako, wala ya mafuta yako, wala wazaliwa wa kwanza wa makundi yako, ya ng'ombe wala ya kondoo, wala nadhiri zako uwekazo zo zote, wala sadaka zako za hiari, wala sadaka ya kuinuliwa ya mkono wako;
¹⁸ lakini hivyo mtakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako, wewe, na mwanao mume na mke, na mtumwa wako mume na mke, na Mlawi aliye ndani ya malango yako; nawe furahi mbele za Bwana, Mungu wako, katika yote utakayotia mkono wako.
Kileo hakikunywewa kwenye makazi ya kila siku bali Mungu aliteua mahali maalumu kwa ajili ya wanawe kufurahi mbele zake.
Baada ya kuona mafungu haya, leo hii tunaweza kusema mahali alipopateua Mungu ili apakalishe jina lake ni kwenye Kanisa. Hapo ndipo utapaswa kunywa na kufurahi katika Bwana. Kwa nini nasema hivi?
Mathayo 26 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁶ Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu
²⁷ Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki;
²⁸ kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.
²⁹ Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.
Hapo Yesu aliwapa mkate (ndilo neno lake) na divai (ndio Roho Mtakatifu), kileo ambacho walikunywa wakati wa Agano la Kale sasa anakinadili kuwa damu yake au Roho Mtakatifu. Hapa hatuongelei tena divai bali damu ya Yesu. Ili kuthibitisha hili Yesu Kristo mwenyewe anasema:
²⁹ Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.
Yesu anasema HATOKUNYWA KABISA kileo hiki mpaka siku atakapokunywa MPYA kwenye ufalme wa Mungu pamoja nao. Hiyo divai MPYA ni Roho Mtakatifu ambaye hutuingiza kwenye ufalme wa Mungu. Wale wana wa ufalme huketi pamoja na Kristo wakinywa divai mpya, bali wana wa giza huketi pamoja na Ibilisi kwenye mabaa wakijipa furaha ya duniani. Ona unabii kuhusu Yohana Mbatizaji:
Luka 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁵ Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.
Badala ya kufurahi katika divai na kileo nabii huyu atajazwa Roho Mtakatifu. Umeona kuwa divai na kileo kilikuwa ni kivuli cha Roho Mtakatifu? Yesu Kristo alitimiliza hilo siku ya Pentekoste ndipo hata mataifa mwanzoni waliwashutumu wanafunzi wa Yesu kuwa wamelewa kileo, lakini Petro aliwathibitishia kuwa huyo ni Roho Mtakatifu.
Pia tumesoma hapo juu kwamba wana wa Israeli walikula mbele za Bwana (ndio kivuli cha ufalme wake) ili wafurahi na pia wajifunze kumcha Yeye. Hii tunaipata katika Roho Mtakatifu na sio baa kwenye koloni:
Warumi 14 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁶ Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya.
¹⁷ Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
Sisi tunakwenda mahali ALIPOPACHAGUA Mungu yaani kwenye ufalme wake na huku tunakula na kufurahi katika Roho Mtakatifu, sio mbege.
Yapo mengi sana ambayo twaweza kuyasema kadri Roho Mtakatifu anavyotufunulia, mfano ukuhani wa Lawi, yote yakihusiana na kileo, lakini kwa sasa naweka tamati hapa tuone kama kuna hoja mbadala.
Amina