Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Kwamba Yesu Kristo aliruhusu pombe kunywewa wakati kumbe aliondoa pombe na kuweka Roho Mtakatifu.
Unauongeleaje huu mstari?
Screenshot_20221214-131357_Chrome.jpg

Pia soma Luka 7:34
 
Na kwa kuongezea Biblia inawashutumu walevi sio wanywa pombe. Kwa hiyo tuendelee kula kamnyweso ila tusilewe. Sagod hana shida na wanywaji ila walevi tu
 
Ukiondoa kifungu hicho,pia kuna neno linasema "kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi,na sio kimuingiacho".

Tatizo dini zetu ni mapokeo kutoka Kwa wazungu,alafu sisi tunaamini tunaijua(dini/biblia) kuliko wao waliotuletea.

Ndio maana leo makanisa mengi yanahubiri mafanikio,fungu la kumi nk.

Imani na upendo vimewekwa Kandi kama sio msingi wa ukristo,yaani kumjua,kumwabudu na kumtumikia MUNGU sio jambo la msingi.

Mimi naamini kuna mahali tumekengeuka.
Hakika
 
Ukisoma kwenye kitabu cha Injili ya Yohana sura ya pili, Kuna kisa kinasiimuliwa ambacho kilitokea katika Kana ya Galilaya.

Katikati ya harusi divai ikaisha, Mama Maria Mtakatifu akamfuata Yesu, akamwambia kuwa mzigo wa gambe umeisha.

Yesu akamjibu muda wangu bado, basi akawaagiza Vijana wamletee maji, na walipoyafunua yakawa divai iliyo bora Sana.

Sasa inakuwaje leo makanisani wanasema tusinywe kabisa maji mema?🥃🥂🍻🍺🍷
Karibu kumsifu Mungu

Kama mwenye dini yake alikuwa anachapa mma, sisi ni nani hata tukatazwe?
 
Onesha andiko Yesu Kristo akiwa baa. Ndugu, epuka kuandika uzushi, ni heri kuuliza. Yesu Kristo alikuwa akinywa nyumbani mwa Wayahudi pale walipomwalika, mfano Zakayo mtoza ushuru. Huko alikunywa kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi sio kwa sababu ya ULEVI. Kwa waliofika Uingereza wana desturi ya kunywa wine kabla ya mlo ikiwa kama appetizer. Huo ni mfano wa ilivyokuwa nyakati za Yesu.
Inategemea wewe umechukulia neno baa kwa maana gani ...ni swala la iq ....hapa tunaongelea sehemu yoyote ya kupata kinywaji cha ulevi kwa pamoja..hata kama ukiwa ukumbi wa harusi kwani ujaona baa zinafanyika harusi hata hapa tz
 
Ukisoma kwenye kitabu cha Injili ya Yohana sura ya pili, Kuna kisa kinasiimuliwa ambacho kilitokea katika Kana ya Galilaya.

Katikati ya harusi divai ikaisha, Mama Maria Mtakatifu akamfuata Yesu, akamwambia kuwa mzigo wa gambe umeisha.

Yesu akamjibu muda wangu bado, basi akawaagiza Vijana wamletee maji, na walipoyafunua yakawa divai iliyo bora Sana.

Sasa inakuwaje leo makanisani wanasema tusinywe kabisa maji mema?🥃🥂🍻🍺🍷
Divai siyo pombe. Konyagi ndiyo pombe.
 
Divai mpaka saiv si inatumika kama chakula cha bwana lakin pitia mithal uone na zaburi jinsi zinavyopinga ulevi
 
Back
Top Bottom