Joseverest
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 52,812
- 71,392
Tunaangamia kwa kukosa MaarifaUkisoma kwenye kitabu cha Injili ya Yohana sura ya pili, Kuna kisa kinasiimuliwa ambacho kilitokea katika Kana ya Galilaya.
Katikati ya harusi divai ikaisha, Mama Maria Mtakatifu akamfuata Yesu, akamwambia kuwa mzigo wa gambe umeisha.
Yesu akamjibu muda wangu bado, basi akawaagiza Vijana wamletee maji, na walipoyafunua yakawa divai iliyo bora Sana.
Sasa inakuwaje leo makanisani wanasema tusinywe kabisa maji mema?🥃🥂🍻🍺🍷
Divai ni wineJe, divai ni pombe?
Ukiondoa kifungu hicho,pia kuna neno linasema "kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi,na sio kimuingiacho".
Tatizo dini zetu ni mapokeo kutoka Kwa wazungu,alafu sisi tunaamini tunaijua(dini/biblia) kuliko wao waliotuletea.
Ndio maana leo makanisa mengi yanahubiri mafanikio,fungu la kumi nk.
Imani na upendo vimewekwa Kandi kama sio msingi wa ukristo,yaani kumjua,kumwabudu na kumtumikia MUNGU sio jambo la msingi.
Mimi naamini kuna mahali tumekengeuka.
Divai ni wine
Pombe sio dhambi.
Ulevi ndio dhambi
Na Ulevi ni
1. Kunywa pombe usiyoruhusiwa na mamlaka, yaani serikali eg. Gongo,
2. Kunywa pombe muda wa kazi.
3. Kunywa pombe kupita kiasi cha nguvu zako.
4. Kunywea pombe bajeti ya jambo lingine kama, ya chakula cha watoto nyumbani, Ada ya mwanafunzi, pesa ya ujenzi, matibabu nk.
Nk.
Na hapo ni sawasawa na Ulafi, unaokatazwa ni Ulafi na sio kula chakula.
Na ulafi unafanana na ulevi kama nilivyoelezea hapo juu.
Ukichona nyama ya mbuzi na kula ukiwa Bar huku watoto wanakula Ugali na Nguru unamefanya Ulafi.
Pombe ni moja ya kazi njema ya Mwenyezi Mungu na haijakatazwa mahali popote katika Maandiko ya Biblia.
Lakini inatakiwa inywewe kwa kiasi na kwa wakati wake kwa lengo la kujiburudisha.
Furaha ya kwenye karamu ya Pombe yazidi furaha zote hapa duniani.
Yes kaka. Jana nilikunywa ALTAR wine (divai ya madhabahunii) nikalewa.Wine ni pombe…!
Kwanini Yesu muujiza wake wa kwanza uwe kubadili maji kuwa divai? Alitaka kutufundisha nini?Tunaangamia kwa kukosa Maarifa
Mithali23
29 Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole?
Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno?
Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu?
Ni nani aliye na macho mekundu?
30Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo;
Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
31Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu;
Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
32Mwisho wake huuma kama nyoka;
Huchoma kama fira.
33Macho yako yataona mambo mageni;
Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
34Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari;
Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.
35 Utasema, Wamenichapa wala sikuumia;
Wamenipiga wala sina habari;
Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
Ulevi ndio umekatazwa. Maana hata Nuhu alikunywa lakini sikuona Mungu akimmind.
Kwanini Yesu muujiza wake wa kwanza uwe kubadili maji kuwa divai? Alitaka kutufundisha nini?
Kwa kubadilisha maji kuwa divai, Yesu alitaka kutufundisha nini?AYA YA 9.
View attachment 2066761
Haha haha hahah Kiribati chapa jogooUnajua divai/wine ni pombe fulani yenye kilevi kidogo tu just kuchangamsha,, lkn kupitia andiko hili wachaga(sio wote) hapa ndio wanahalalisha double kiki, k vant, gongo etc.