Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Muujiza wa Kwanza alioufanya Yesu ni kubadili maji kuwa divai. Kwanini Makanisa mengi yanahubiri kuwa pombe ni dhambi?

Ukisoma kwenye kitabu cha Injili ya Yohana sura ya pili, Kuna kisa kinasiimuliwa ambacho kilitokea katika Kana ya Galilaya.

Katikati ya harusi divai ikaisha, Mama Maria Mtakatifu akamfuata Yesu, akamwambia kuwa mzigo wa gambe umeisha.

Yesu akamjibu muda wangu bado, basi akawaagiza Vijana wamletee maji, na walipoyafunua yakawa divai iliyo bora Sana.

Sasa inakuwaje leo makanisani wanasema tusinywe kabisa maji mema?🥃🥂🍻🍺🍷
Hii thread Jumapili naenda kuitolea sadaka kanisani....

Yani ajabu la kwanza kabisa la Masiha ilikuwa kutengeneza ulabu

Tumsifu Yesu Kristo....
 
Ukiondoa kifungu hicho,pia kuna neno linasema "kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi,na sio kimuingiacho".

Tatizo dini zetu ni mapokeo kutoka Kwa wazungu,alafu sisi tunaamini tunaijua(dini/biblia) kuliko wao waliotuletea.

Ndio maana leo makanisa mengi yanahubiri mafanikio,fungu la kumi nk.

Imani na upendo vimewekwa Kandi kama sio msingi wa ukristo,yaani kumjua,kumwabudu na kumtumikia MUNGU sio jambo la msingi.

Mimi naamini kuna mahali tumekengeuka.
Hiki kifungu wanapenda kukitumia kwenye kufakamia kitimoto tu. Kwenye ulabu wanazuga hawakioni

Ngoja niwahi kaunta nikazimue
 
Hata mimi kuna muda najiuliza barua walizoandikiwa mfano waefeso au wakorinto kwa nini tuje tusomewe sisi watanganyika?
Afu yani ni kwanini tufuate maagizo ya Paulo badala ya kufuata ya Mshua mwenyewe?

Cha msingi ni kufuata amri kumi za mshua mwenyewe. Katika amri hizo hakuna inayosema USILEWE

Mwanae alivyokuja akaweka mambo rahisi zaidi. Akasema nawapeni amri mpya PENDANENI...

Bujibuji Simba Nyanaume nyoko hapa unigongee LIKE kudadadadeki. Afu usogee hapa Bunju tupige gambe huku tukitafakari hili neno kuntu
 
Huyo jamaa katengeneza kwani Mungu wetu aliyetengeneza mito ya POMBE huko peponi anakunywa hyo POMBE.
Ndo na Mimi ninemuuliza yesu baada ya kugeuza maji kuwa pombe Kama mnavyosema.
Aya gani inasema yeye yesu mwenyewe alikunywa hyo POMBE?
Kwani ingekuwa kitu haramu Yesu angewatengenezea watu wanywe ili iweje? Kwamba Yeye hakunywa sio issue. Issue ni kwamba kwa kuwa aliitengeneza Pombe na kuwapa watu wanywe, aliihalalisha.
 
Afu yani ni kwanini tufuate maagizo ya Paulo badala ya kufuata ya Mshua mwenyewe?

Cha msingi ni kufuata amri kumi za mshua mwenyewe. Katika amri hizo hakuna inayosema USILEWE

Mwanae alivyokuja akaweka mambo rahisi zaidi. Akasema nawapeni amri mpya PENDANENI...

Bujibuji Simba Nyanaume nyoko hapa unigongee LIKE kudadadadeki. Afu usogee hapa Bunju tupige gambe huku tukitafakari hili neno kuntu
Mshua naye alikuwa anaupiga mwingi sana
Screenshot_20220103-100351_Chrome.jpg
 
Isitoshe alikuwa ana uwezo wa kugeuza maji kuwa maziwa. Lakini yeye akatengeneza ulabu. Yesu alikuwa bonge la genius
Angegeuza maji kuwa Mirinda na Fanta, ila akaona mbali, miaka 2020 ijayo kuwa mabinti wataugeuza huo muujiza kuwa boyfriend
 
Na kwani Kuna sehemu yesu amesema hajawahi kufanya mapenzi?
mbona mnaamini yesu alikuwa bikra?
Wapi na nani amesema Yesu alikuwa bikira? USITULISHE maneno na usitutoe nje ya mada. Mada ya leo ni ulabu

Mambo ya bikira tutaanzisha uzi wake
 
Back
Top Bottom